Kuwakosa Viongozi Wenye Hekima Ndani ya Vyama Vya Siasa, Kunaleta Hatari ya Kuwapata Viongozi Wasio na Hekima Kwenye Serikali.

Kuwakosa Viongozi Wenye Hekima Ndani ya Vyama Vya Siasa, Kunaleta Hatari ya Kuwapata Viongozi Wasio na Hekima Kwenye Serikali.

Bams

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
19,362
Reaction score
48,879
Sote tunajua kuwa mchakato wa kuwapata viongozi wa Serikali unaanzia huko kwenye vyama vya siasa. Chama cha siasa kikishinda uchaguzi, aghalabu, nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Serikali hushikwa na hao viongozi wa chama kilichoshinda uchaguzi. Hii ina maana mkiwa na viongozi wa hovyo ndani ya chama, halafu chama hicho kikashinda uchaguzi, ina maana pia mtakuwa na viongozi wa hovyo ndani ya Serikali.

Leo nimesikia kauli ya viongozi wa vyama vya siasa 13 visivyo na wabunge kuhusiana na utekwaji na mauaji ya watu wanaoikosoa Serikali.

Kwa kweli kwa aina ya viongozi wa vyama hivi, unapata jibu la haraka ni kwa nini vyama hivi haviwezi kupata mbunge hata mmoja kwenye uchaguzi wa haki na huru.

Fikiria kiongozi wa chama analinganisha tukio la kukoswakoswa kwa risasi kwa Rais Trump, na tukio la utekwaji na mauaji ya Ally Kibao!! Unajiuliza, huyu kiongozi kweli ana akili?

Ni ukweli kwamba hakuna nchi yoyote Duniani ambayo ni free from criminals. Lakini umakini na utofauti wa mataifa upo katika namna criminals wanavyoshughulikiwa, na mifumo iliyopo katika kudhibiti criminality.

Angalia kule Marekani, siku Trump alivyoshambuliwa kwa risasi. Mshambuliaji aliuawa pale pale. Ile inathibitisha kuwa mshambuliaji alikuwa ni mhalifu, na vyombo vya dola, licha ya kushindwa kuzuia uhalifu, lakini angalao mhalifu alidhibitiwa na kuuawa. Ule ni ujumbe tosha kuwa kwenye shambulio lile, serikali na vyombo vyake vyote havikuwa na mkono wake kwenye shambulio lile, na ule ulikuwa ni uhalifu wa mtu, siyo uhalifu wa dola dhidi ya Trump.

Lakini linganisha tukio lile na shambulio dhidi ya Lisu na utekaji na kisha mauaji ya Ally Kibao.

Shambulio dhidi ya Lisu, mashuhuda wanasema baada ya shambulio, washambuliaji waliondoka kwa gari lao aina ya Nissan patrol, rangi nyeupe, huku polisi wakiyazuia magari na boda, kupisha gari hilo lipite. Halafu baada ya siku kadhaa, CCTV camera zilizokuwa kwenye nyumba ya Waziri Kalemani, zinazoaminika kuchukua picha za shambulio, polisi walikwenda kuziondoa.

Kwa upande wa utekwaji wa Ally Kibao, baada ya kuchukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi, na ndani ya gari kukiwa na askari polisi, mwenye gari aliripoti tukio kituo cha polisi, familia ya Ally nayo wakaripoti kituo cha polisi na kufungua jalada. Mara baada ya mwenye gari kuripoti polisi, akieleza mazingira yote na magari yaliyotumika kuwa yalikuwa hayana namba, hakuna shuhuda hata mmoja ambaye anaeleza labda sehemu yoyote jijini Dar es Salaam, magari yasiyo na registration number au magari yote yalikuwa yakisimamishwa kwaajili ya kuchunguzwa.

Hivi kama una akili timamu, unawezaje kulinganisha tukio la Trump kushambuliwa na kisha mara moja mshambuliaji kuuawa na vyombo vya ulinzi, Vs haya matukio ya mashambulio ya hapa kwetu Tanzania, ambayo wahalifu wanapewa njia ya kupita?
 
Na kama "...una akili timamu,..." unawezaje kuamini kwamba mwaka huu 2024 kutakuwepo na uchaguzi wa serikali za mitaa, na hapo mwakani 2025 kuna uchaguzi mkuu?

Bottomline' ni hii: CCM wameamua liwalo na liwe, kamwe hawawezi kuruhusu wananchi wawachague viongozi wanao wataka wawaongoze.
Wakati nchi inapofikia hali kama hiyo, ni kipi cha kufanya? Kukaa kimya na kukubali hali hiyo?
 
Ni kosa kiutu kubishana na kulumbana na mtu kichaa kwenye bunduki,
 
Ni kosa kiutu kubishana na kulumbana na mtu kichaa kwenye bunduki,
Utashangaa ukisikia kuwa ninakubaliana na hayo maneno yako; lakini pengine kwa kutoelewa utadhani ninakubaliana na wewe.
Njia sahihi ni kumnyang'anya huyo kichaa hiyo bunduki kwa gharama yoyote ile kabla haja sababisha maafa makubwa zaidi.
 
Tupo pamoja Ila unafiki na tamaa havitotufanikisha.Tuna kasoro nyingi
 
Kwanza kabisa , sio kweli Serikali inaundwa na wanasiasa tu. Usipotoshe.

Pili, hayo mengine yote ni porojo tu

Hivi kama una akili timamu, unawezaje kulinganisha tukio la Trump kushambuliwa na kisha mara moja mshambuliaji kuuawa na vyombo vya ulinzi, Vs haya matukio ya mashambulio ya hapa kwetu Tanzania, ambayo wahalifu wanapewa njia ya kupita?

☝🏿😂😂Cha kushangaza, Trump na majambazi wenzake wanasema matukio ya kushambuliwa kwa wanasiasa, kuuwawa kwa waandishi wa habari, vurugu bungeni, n.k marekani huwa yanatokea Nchi zingine, na sio Marekani.

Wenye Akili Timamu huwa wanafanya wapi ulinganishi😂😂😂😂😂🤡🤡🤡🤡🤡🤡🤡

Wacheni Ugaidi
 
Sote tunajua kuwa mchakato wa kuwapata viongozi wa Serikali unaanzia huko kwenye vyama vya siasa. Chama cha siasa kikishinda uchaguzi, aghalabu...
Ukatili na unyama upo dunia nzima. Hao wamarekani wanaongoza kwa cold cases, watu wanauliwa leo hii kesi inakuwa wazi kwa kipindi cha miaka 15 mpaka 30 bila ya ushahidi kamili kupatikana.

Dunia nzima ukatili unaongezeka kila kukicha, haya yanayotokea hapa TZ ni madogo sana kwa yanayotokea katika mitaa ya Rio De Janeiro au Sao Paulo au kule Bogota.

Tatizo tunapenda mno kulialia, tunapenda mno siasa za malalamiko na ukosoaji mwingi.
 
Sote tunajua kuwa mchakato wa kuwapata viongozi wa Serikali unaanzia huko kwenye vyama vya siasa. Chama cha siasa kikishinda uchaguzi, aghalabu, nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Serikali ...
kuumizwa moyoni na fikra na mawazo tofauti na yako ni kitu mbaya sana na hatari kwa afya ya akili ya binadamu,

ni muhimu kukubali uhuru na haki ya maoni ya wengine kiungwana, kwa usawa na haki ndrugu zango.

Jitahidini kua na hoja zenye mashiko na ushawishi ili kuungwa mkono na watu wengi zaidi ,

sio kujipa umuhimu msiostahili,
huku mmefura kwa chuki, hasira na mihemko kwa walio tofauti na mawazo yenu 🐒
 
Kuna shida kubwa katika kutofautisha uhalifu unaotuhumiwa kufadhiliwa na dola dhidi ya ule wa kawaida wa watu binafsi!
"State sanctioned"

Watu wetu ni mbumbumbu sana, wanafikiria kuwa Serikali ni taasisi takatifu, wakati kuna uwezekano wa yote. Mnaweza kuwa na Serikali yenye dhamira kubwa ya kuwaletea maendeleo, unafuu, furaha na huduma bora wananchi wake, LAKINI mnaweza kuwa na serikali ya kishetani kabisa ambayo ipo kwaajili ya kuwanufaisha wao waliopo Serikalini na wateule wao. Hawa huifanya Serikali kama ni hazina lao. Na yeyote anayepinga au kukosoa matendo yao, hugeuka kuwa adui anayetaka kuwapokonya hazina yao. Hawa ndio huwa tayari kuteka hata kukuua ukionekana unauanika uovu wao, maana wanajua kuwa umma ukielewa uovu wanaoufanya, unaweza kuwaondoa. Hawa hata siku moja hawafikirii juu ya ustawi wa watu, watafanya baadhi ya vitu vizuri siyo kwa sababu ya mapenzi mema bali kwaajili ya kuwapumbaza watu, na watakachokipeleka kwa wananchi itakuwa ni ziada baada ya wao kutosheka.
 
kuumizwa moyoni na fikra na mawazo tofauti na yako ni kitu mbaya sana na hatari kwa afya ya akili ya binadamu,

ni muhimu kukubali uhuru na haki ya maoni ya wengine kiungwana, kwa usawa na haki ndrugu zango.

Jitahidini kua na hoja zenye mashiko na ushawishi ili kuungwa mkono na watu wengi zaidi ,

sio kujipa umuhimu msiostahili,
huku mmefura kwa chuki, hasira na mihemko kwa walio tofauti na mawazo yenu 🐒
Ujinga na kukosa hekima, siyo tofauti ya mawazo. Ukisema 2 x 3 = 5; nikakuambia umekosea, jibu haliwezi kuwa hiyo 2 x 3 = 5, ni fikra zako ambazo natakiwa kuziheshimu. Au ukiniambia embe ni sawasawa na tangawizi, nikisema hupo sawa, jibu haliwezi kuwa niheshimu mawazo yako.

Kwa mtu mwenye akili timamu, kweli unaweza kulinganisha shambulio la Trump na mauaji ya Ally? Yanalingana katika nini?
 
kwamba kuiunga mkono Chadema diyo hekima na Kuiunga mkono CHAUMA sio hekima 🤣

kifo ni kifo tu hakilingani na chochote na siasa nyepesi kama za Tz ni kujifurahisha tu gentleman 🐒
 
Back
Top Bottom