Kwa dhuluma ambayo Jakaya Kikwete alimfanyia Mzee Lowassa, ataumaliza uzee wake bila amani

Barua ya kujiuzuku kumnusuru bosi na maswahiba utaiandikaje?
Rais A.H Mwinyi alipoandika barua kutokana na mauaji ya Watu hakuwa na kosa. Mwinyi hakuagiza wala hakuwa na ufahamu wa kilichotokea. Katika kuonyesha kwamba serikali inajali alijiuzulu.
Kujiuzulu kwa mwinyi kulimuondolea Rais mzigo kwasababu kinyume chake ingalikuwa tabu.
Barua inaandikwaje? Soma barua ya A.H. Ipo mtandaoni.
Hata ukisema "mimi sina makosa, ila najiuzulu kwa kuinusuru serikali kutoka kwenye matatizo yanayohusiana na mimi kuwapo serikalini" tayari unanuka, tayari umejiweka katika matatizo ya kukufanya uwe untenable. Kuna calculations fulani umekosea hapo.
Hapana , ndiyo maana A.H. Mwinyi alirudi na kuwa Rais wa Zanzibar na Tanzania chini ya Uongozi ulioshuhudia anguko lake. Timu nzima ya kupitisha majina akiwemo RC wa Shinyanga Peter Kisumo ilikuwa ile ile.
Walijua hakutenda, aliwajibika.
Caesar's wife must be above suspicion.
I agreed
Kuhusu Kikwete.
Kwanza kabisa mna uhakika gani Kikwete alikata jina la Lowassa? Kwa uamuzi wake tu. Hizi habari zina uhakiki gani? Was Kijwete realky that powerful?
Kuna habari kutoka kwa 'privy' na mtando mzima. Kumbuka mtandao ulikuwa na watu wengi
Habari zinatoka ''horse's mouth'

Kuna circumstancial evidence pia kuhusu nguvu ya Kikwete
Rais SSH anasema wakati wanachagua nani awe VP baada ya Magufuli kuteuliwa, kamati kuu iliitwa.

Rais Samia anasema, ''sisi tulikaa nje tukinywa chai na biskuti wakati vingunge wameingia na kujifungia' Vingunge si Kamati kuu ni JK na watu wachache sana. Maana yake ni kwamna hata CC haikuwa na nguvu

Pili, unakumbuka ' ...Tunaimani na Lowassa''. Ilikuwa dhahiri wajumbe wa NEC walikuwa na taarifa za nini kimetoke.
Magufuli akathibitisha kwa kusema ''.... walioimba ningewatimua siku hiyo' akionyesha nguvu ya Mwenyekiti.

Tatu, mwaka 1995 Mkapa alipomshinda JK, ilisemwa kura ''hazikutosha'. hii ilikuwa lugha laini tu, tunajua Mwenyekiti wakati huo akiwa na Nyerere walimtaka Mkapa. Unaweza kuona nguvu ya Mwenyekiti kama Kikwete

Nne, Mkapa anathibitisha alitumwa na Nyerere kwenda kwa mzee Kitwana Kondo. Nyerere ndiye alimshawishi achukue Form, tunajua the rest is history
Hapa ndipo pana hoja nzuri sana. Suala ninaloongelea si kukubalika au kutokubalika kwa Lowassa.
Wala siongelei na sikubali kuwa alidhulumiwa Urais.

Ninachosema hapa ni kwamba alidhulumiwa taratibu. Chama kina sifa za mgombea na zinajulikana.
Ikiwa ENL alikuwa hana sifa, Chama kilimpa vipi Form ya kugombea? Chama kiliridhika alikuwa na sifa!

Pili, taratibu zinasema mwenye kura nyingi atasonga mbele. Iwe Kikwete au kundi lote liliondoa jina lake si kwa kukosa kura bali kwa fikra zao, hiyo ni dhuluma. Kikwete au kundi hilo wangemzuia kwa kukosa sifa, na kwa kukosa kura. Kukata jina lake kwa utashi na si taratibu ni dhuluma

Nipo kwenye rekodi, sijawahi kumkubali ENL na hata juzi niliandika machache mazuri na mengi mabaya yake.
Hata hivyo hatuwezi kuacha kusema dhulma aliyofanyiwa! na katikati ya dhulma yupo Kikwete in so many ways.
 
Nimehakikisha kwasababu umeandika kwa kukosea grammar kulikojirudia zaidi ya mara moja. No editing at all.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Haya mengi tumeyagusia awali kwenye uzi

Inaonekana mfumo mzima wa kuteua mgombea CCM una usiri na matatizo mengi.

Ndiyo maana kuna habari hata Kikwete alikuwa victim wa mifumo hii 1995.

Mfumo ni opaque kiasi kwamba ni vigumu kumlaumu Kikwete beyond reasonable doubt, hapa tunapata maneno mengi ya hearsay na innuendo.

Kwangu mimi, the bottom line ni kwamba, Lowassa, kwa kukubali kujiuzulu, alikuwa amejitengenezea doa la narrative kwamba yeye ni mla rushwa kukubalika.

Hii ilikuwa ni "shooting oneself in the foot before starting a marathon".Especially kwenye nfumo wa ki sniper ambao hauna fairness na watu wanaweza kukatana kirahisi. Kama aliona hana kosa angekomaa tu mpaka aondolewe uwaziri mkuu na ku pull a Mrema on them kwa kutumia kuondolewa huko.

By resigning, he took the wind out of his sails himself.
 
Nimehakikisha kwasababu umeandika kwa kukosea grammar kulikojirudia zaidi ya mara moja. No editing at all.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app

That's all? Mtu akikosea kuandika tu, ka panic?

Watu hawakosei kwa kuandika kwa kasi kwenye simu?

Mtu akiandika kwa kasi kwenye simu ka panic?

You are making a dictionary logical fallacy here.

Kukosea grammar au kukosea spelling?

Mimi nakosea spelling kila post na narudia ku edit. Natumia simu.

Kama unataka kuwa secretary wangu kunionesha wapi nimekosea, karibu.
 
Sasa mbona kwangu hukurudia ku edit? Hata nami naandika kwa simu but sikosei mara nyingi kama ilivyo kwako.

Mimi ni mkulima, sijasomea secretarial course. Anyway, endelea na wengine.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Sasa mbona kwangu hukurudia ku edit? Hata nami naandika kwa simu but sikosei mara nyingi kama ilivyo kwako.

Anyway, endelea na wengine.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Ninekuuliza wapi? Hujaonesha.

Inawezekana wewe hu interact na watu wengi kama mimi, hivyo kumsahau mtu si rahisi.

Inawezekana mimi na interact na watu wengi sana, hivyo, kukusahau mtu kama wewe ni rahisi.

Naona umeshindwa hoja, unakosoa muandiko, na hata huo muandiko hujaonesha wapi.
 
Hata salimu ahamed salimu naye atasema alidhulumiwa Haki yake. Uongozi unatoka kwa Mungu na siyo kwa Mwanadamu. Hakuna mwenye haki miliki ya Urais wa nchi hii wala wakusema kuwa mimi ndiye nilistahili kuwa Rais wakati fulani. Huo ni ujinga na utoto. Mtoa mada najuwa hajakomaa akili na anaandika kwa kutumia hisia za uvyama badala ya kuwaza nje ya boksi.
 
Acha umbumbumbu wako. Unaposema alishinda ni alishinda katika uchaguzi upi na kwa ushahidi upi? Tatizo umeandika mada kwa kutumia hisia badala ya kutumia akili.
 
kama hujui historia nyamaza ile ndege ya kwenda dodoma ililipwa na rostam aziz,pia unajua wizi ambao marehemu aliufanya?
 
Magufuli aliko kwenye tanuru la moto wa mkaa wa mawe
 
Lowassa na Rostam Azizi wlitaka kufanya ujanja...wakashindwa kujua kuwa Jakaya ni mtoto wa mjini. Akapindua meza. The rest is known.

Ngosha Mzilamkende akaona Jakaya boya...akamsogeza Lowassa, naye akamleta Rostam Azizi. Ngosha akajenga urafiki na wahuni wamualika kuzindua kiwanda pale Morogoro. Haikupita mwezi, tukatangaziwa msiba!
 
Au ulikuja ku edit baada yangu kukujibu, basi mimi nilipoona tu yale makosa yako ya kiuandishi na kukujibu sikurudi tena kule juu kutazama maendeleo yako, nikaendelea na maisha mengine.

Hapa hoja wala sio tatizo, tatizo nilipokusoma kwa namna ulivyoandika nikaona huyu mtu kama ningekuwa karibu yake angenichapa makofi.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Acha uongo kikwete alikuja na majina kwenye mfuko wa shati mpaka nchimbi na sophia simba wakamwambia kikwete sio utaratibu inaonekana ulikua mdogo sana 2015
 
Naona tunajichanganya tu, mkasa mzima wa Richmond ulishawekwa hapa JF kitambo nabulieleza mkasa mzima jinsi BT alivyousuka nanjumba bovu kumwangikia ENL. Sidhani kama aliomba nadhani mshambulizi yalimzidi ikabidi abwage manyanga. Akasema tatizo ni 'PM. PPP ENL
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…