Kwa kauli hii naanza kuogopa kula Sangara

Kwa kauli hii naanza kuogopa kula Sangara

Moja ya biashara iliyotawaliwa na vitendo vya kishirikina ni "uvuvi". Hakuna mvuvi hata mmoja asiyeamini kwenye ushirikina. Ni kama tu biashara ya uchimbaji madini ilivyotawaliwa na imani za kishirikina. Sasa kwenye uvuvi wa samaki ni mara elfu yake.
Mimi ni mwenyeji wa mkoa wa mara, kijijini kwetu tumepakana na ziwa Victoria, hivyo najua kila aina ya uchafu unaofanywa na wavuvi wa samaki.
Lakini.........kwa elimu niliyonayo, nakataa kabisa kuwa eti, maji ya maiti ni kisababishi cha ugonjwa wa kansa. No! That is not true at all.
Kansa inasababishwa na "kemikali", "mionzi", au "virus". Pia inawezekana aina fulani ya Bacteria wakasababisha kansa, lakini hata kama samaki ana hao Bacteria siyo rahisi kumwambukiza mlaji sababu hakuna Mtanzania anayekula samaki akiwa mbichi.
 
Mnadanganywa bila utafiti wowote tangu lini maji aliyooshewa mtu yakafuata na kansa
Na hayo maji yanawekwa wapi kwa mfano Ziwani?
Sumu na chemicals zinazotumika migodini hamuoni

Kama wataalamu wameongea upuuzi huu basi tuna safari ndefu bado
 
Kumbe wavuvi wa ziwa Victoria wanatumia maji ya maiti kutupatia kitoweo kama alivyotahadharisha Makamu wa Rais Dkt. Mpango baada ya wagonjwa wa saratani kuongezeka huko Mwanza katika ziara yake hapo juzi.

Naunga mkono nasaha za wavuvi kuacha kutumia maji ya maiti kama chambo cha kukamatia samaki. Wakiendelea hivyo wengi tutaangamia na hata nchi zinazonunua minofu Ulaya zitapungua.

Inatisha.
Na mazebaki juu,full kansa.
 
Kama mie [emoji23]

Niliumwaga sana so dokta akaniambia nisitumie hao samaki wa masafa marefu,,,,,nile nyama ya kuku wa kienyeji tu na mayai ya kienyeji,
Toto la kishua

Magonjwa kama ya allergy ni ya ushuani
Sijawahi sikia mwananyamala , au Manzese kuna mtu ana allergy na samaki[emoji16]

Huko wanakula kila kitu kasoro nyama ya mtu tu
 
Mkuu dona ya hotelini inashida gani ?
Mkuu, mahotelini wananunua tu unga. Unga huo unatokana na mahindi ambayo yaliwekwa dawa/sumu ili yasiharibiwe na wadudu mara tu baada ya mavuno. Wasagaji huwa wanasaga tu mahindi yakiwa na dawa badala ya kuosha mahindi kuondoa dawa/sumu kwanza.
 
sasa tuchague lipi? wanapiga dawa ili kuzuia fungi wanao dhalisha sumu ya aflatoxin ambapo ukisaga dona tu we kwisha. sasa kilicho baki ni kuchagua
1. ule unga mweupe usio na sumu ila hauna virutubisho.
2. ule dona kutoka kwenye maindi yasio pigwa dawa yani dona lenye aflatoxin.
3. ule dawa ya viwandani iliopigwa ili kuuwa wadudu.
😂😂 hadi raha
 
Maiti Ni wengi kiasi watosheleze nahitaji ya wavuvi wote lake zone? Kuna kipindi kulitokea uvumi kuwa kuku broiler wanalishwa ARVs eti wanenepe! These are myth busters [emoji1787][emoji1787]
Haijasemwa ni wote,kumbuka athari yake kwa binadamu hata wakifanya kwa uchache inakuwa kubwa sana.
 
Kumbe wavuvi wa ziwa Victoria wanatumia maji ya maiti kutupatia kitoweo kama alivyotahadharisha Makamu wa Rais Dkt. Mpango baada ya wagonjwa wa saratani kuongezeka huko Mwanza katika ziara yake hapo juzi.

Naunga mkono nasaha za wavuvi kuacha kutumia maji ya maiti kama chambo cha kukamatia samaki. Wakiendelea hivyo wengi tutaangamia na hata nchi zinazonunua minofu Ulaya zitapungua.

Inatisha.
Study ifanyike kubaini kama chanzo ni Mecury au hiyo dawa ya maiti, kama ni Mecury watazame kama madhara yameanza kujitokeza Shy na Tabora ambako nao wanatumia maji ya ziwa hilo
 
Ndio umejua Leo,maji Yana siri kubwa, hivi mv bukoba ilipozama miili ilikwenda wapi, samaki walijilia
Dkt Mpango angekaa kimya tu huku hilo suala kama lina ukweli akalifanyia kazi ndani kwa ndani kwa sababu hatuwezi kuachia watu wakafanya uharamia huo na wakati huo huo hatutaki walaji wa nje na ndani wakapata wasi wasi wa hadharani kama huo.Ukiwa mwanasiasa na kiongozi wa nchi lazima mengine uyakalie kimya uwache watu wa mitaani wapayuke mwanzo.
 
sangana ana high level of unsaturated fat(mafuta) ambao hupelekea oxidation samaki huharibika, pia autolytic changes yan self degradation, enzymes zilizo mwilin mwa samaki baada ya samaki kufa hualibu mwili husababisha hatufu mbaya. formaline iliopo kwenye maji ya maiti huxuia wadudu kama izi kukaa mbali na mzoga wenda ni mbaya kwa mlaji.
ww na nxi hamna tofauti kama kwa nxi ni sumu basi hata kwako ni sumu. na wale wa mboga mboga usinunue mboga ambayo haijatobolewa na wadudu hata kidogo unanunua maradhi
Daaa! Hadi mboga mboga??
 
Kumbe wavuvi wa ziwa Victoria wanatumia maji ya maiti kutupatia kitoweo kama alivyotahadharisha Makamu wa Rais Dkt. Mpango baada ya wagonjwa wa saratani kuongezeka huko Mwanza katika ziara yake hapo juzi.

Naunga mkono nasaha za wavuvi kuacha kutumia maji ya maiti kama chambo cha kukamatia samaki. Wakiendelea hivyo wengi tutaangamia na hata nchi zinazonunua minofu Ulaya zitapungua.

Inatisha.
Amefafanua yanatumikaje? Yanapatikanaje? Kwa kiwango gani? Waziri kalishwa matango pori halafu naye akakubali kuyala na kugaia wengine
 
Back
Top Bottom