Lakini hakuna sababu ambayo wanaweza kujitetea nayo tukawaelewa!!
Nje na kazi yao nao ni binadamu kama sisi iweje wafanye unyama vile?
Unaongelea Jeshi la Wananchi au Jeshi la Polisi?
Jeshi la Polisi lina makosa ya moja kwa noja kwa kuua wananchi na kushindwa kuwalinda.
Kesi ya polisi iko wazi na ya moja kwa moja.
Kosa la Jeshi la Wananchi Tanzania ni complex kidogo. Kwa sababu wao kimsingi kazi yao ni kulinda mipaka ya nchi, na kulinda raia kutoka maadui wa nje, na ndani ya nchi wanaingilia pale watakapoitwa na polisi.
Kisheria na kikatiba wanajeshi wanatakiwa kufuata amri za viongozi wa kiraia kisiasa.
Na hiki ndicho kitu walichofanya.
Tatizo inaonekana viongozi wa kiraia wamepanga mauaji.
Wanajeshi wangefanyaje? Kulikuwa hakuna jinsi ya kuzuia mauaji yale bila ya wanajeshi (JWTZ) kuanza kupigana vita na polisi na kufanya mapinduzi ya kijeshi.
Na hatujui ingetokea vita kati ya polisi na wanajeshi nchi ingeishia wapi.
Hapa root cause ni uongizi wa kiraia uliopanga mauaji.
Jeshi (JWTZ) lime fail kwenye intelligence, na lime fail kuzuia mauaji, lakini tunategemea vipi lisi fail wakati kikatiba limeamriwa kutii viongozi wa kisiasa ambao ndio waliopanga mauaji?
Let's say Jeshi lina wajibu wa kukagua mizigo inayoingia nchini, likataka kukagua makontena fulani, halafu likaambiwa hii ni mizigo ya Ikulu, haitakiwi kukaguliwa. Likatii amri.
Hapo kama jeshi limeshindwa kugundua silaha zimeingizwa, litakuwa limefanya makosa kutokujua au mfumo wenyewe ndiyo umeioa Ikulu nguvu sana na umelifelisha jeshi?