Benzodiazepine
JF-Expert Member
- Oct 18, 2018
- 1,264
- 2,053
Kwani Uislamu ni nini? na madhehebu yake makuu ni yapi?Wairani wana tamaduni zao ila sio Waislamu, Mashia sio Waislamu
Tatizo lako hujui kufikiri kidhahania.Kwa nini yeye asijue kusoma halafu wengine wajue wakati wapo kwenye mazingira sawa?
Kwa nini wenzie wajue kusoma na yeye ashindwe wakati wapo mazingira sawaHalafu mtoto akishindwa kusoma, utamlaumu mtoto kashindwa kusoma au utamlaumu baba kamuweka mtoto katika mazingira ya kutoweza kujua kusoma?
Kwa nini wenzie wasifanye huo ubaya na yeye aufanyeKati ya aliyeumba uwezo wa ubaya kufanyika, na anayefanya ubaya tu kwa sababu kajikuta yupo katika ulimwengu ambao ubaya unaweza kufanyika, nani ana kosa kubwa hapo?
Kwa nini wenzake wasiue halafu yeye aue na wakati wote wapo ulimwengu mmoja?Kati ya aliyeumba ulimwengu ambao mtu mmoja anaweza kumuua mwingine, ule uwezo wa mauaji kufanyika, na mtu anayefanya mauaji kwa sababu ulimwengu unaruhusu mauaji kufanyika, nani ana kosa kubwa zaidi hapo?
Maswali yako ya "kwa nini wenzie" yanaonesha hujaelewa mfano, hujaelewa swali, hujaelewa chochote cha msingi.Kwa nini wenzie wajue kusoma na yeye ashindwe wakati wapo mazingira sawa
Kwa nini wenzie wasifanye huo ubaya na yeye aufanye
Kwa nini wenzake wasiue halafu yeye aue na wakati wote wapo ulimwengu mmoja?
Uislamu ni dini ya kumtii au kumnyenyekea Allah kwa kufuata maamrisho na makatazo yakeKwani Uislamu ni nini? na madhehebu yake ni yapi?
Ukiweza kujibu hilo, basi hapo tutajua kama Shia ni Islam au sio Islam.
Kwani katika ulimwengu huu ni wote wanafanya mabaya?Kwa sababu hakuna wenzetu walio katika ulimwengu usioruhusu mabaya.
Duuh, kwamba Muslim Iran ni 40% tu 🤔Waislam katika nchi ya Iran ni kama asimilia 40%, Kumbuka hao sio Waarabu wana utanadunia wao wa kale na kale kama Persian culture. Hao unaowaona wanatawala kwa kivuli cha dini ni jamii tu kama BAKWATA kwa hapa bongo ipate madaraka. Kwa hiyo maelezo yako yote ni ya uongo na yamejaa ujinga na kukosa taarifa sahihi.
Ni ujinga kuweka fikra za mtu mmoja kwenye maisha ya watu wengi.. ni mara mia bomu moja linalo vurumshwa na iran kwenda israel likosee njia likaangukie kule mnakoenda kumpiga shetani na kwenye nyumba ya milele ya huyo jamaa yenu ili akili ziwakae sawaMangi kimambi naye anasimama na watu wengine katika kuushutumu utawala wa Kiisilamu wa Irani kusema ni mgumu afadhali ule wa Saudia arabia na baadhi ya inchi zingine za Kiisilamu
Nimeona ngoja niwajibu watu wote waujue Uisilamu wa kweli,Ukisoma historia ya kweli kabisa ya Uisilamu alioishi nao Mtume Muhammad (S.A.W) ndiyo haya maisha halisi wanayoishi wairani,inamaana hakuna kitu kipya walichoingiza kila wanachokifanya ni maelekezo ya Mwenyezi Mungu kwenda kwa Mtume wake Muhammad(S.A.W)na wao wanayafwata na haya yanayotokea leo yalishatokea miaka 1400 huko kabla
Saudia Arabia
Kuna Waisilamu lakini kama inchi haina sifa ya kuitwa inchi ya Kiisilamu sababu tayali imeshajitoa katika misingi ya kiisilamu,wameungana na Waisrael pamoja na inchi za Magharibi wamejikuta wao wanafwata tamaduni zao wakati Mungu anatukataza Waisilamu kukaa mbali na watu kama hao
Mfano leo hizo inchi zinazojiita za kiisilamu zimewakalibisha wazungu zimejikuta zinauza pombe,kuna clabu za malaya nazani hata nyama za nguruwe zinauzwa watu wanatembea uchi kama Dubai na viongozi wao wanaishi maishi ya anasa,
Katika Uisilamu hivyo vitu vimepigwa marufuku sasa mnamshutumu Irani anayefwata sunna ya Mtume Muhammad(S.A.W) na maisha aliyoisha swahaba immamu Ali bin twalibu au manataka muendeleza wa maisha ya makafiri wa Makka kina Muwaiya kabla hawajakubali kusilimu kinguvu
Mbona unabadilisha swali?Kwani katika ulimwengu huu ni wote wanafanya mabaya?
Mimi ninaposema "wenzake" namaanisha wale ambao hawatendi mabaya
Kwa hiyo huwezi kumtetea eti hana kosa kwa kuwa ameletwa kwenye ulimwengu wenye mabaya na wakati kuna wenzie hawatendi hayo mabaya katika ulimwengu huohuo.
Kwa mfano hapa nakujibu mwenye kosa ni huyo anayefanya mabaya kwa sababu ameamua mwenyewe kuchagua mabaya wakati wenzie wakichagua mazuriKati ya aliyeumba ulimwengu ambao mabaya yanaweza kufanyika, na wanaofanya mabaya kwa sababu tu wapo katika ukimwengu ambao mabaya yanaweza kufanyika, nani ana kosa kubwa zaidi?
Sunni sio dhehebuUliyoyataja, ni vi-sub-part vya dhehebu la Sunni.
Endelea kuchimba zaidi.
Uliyoyataja hapo ni vi-sub-part (shule za sheria) vya dhehebu la Sunni.Uislamu ni dini ya kumtii au kumnyenyekea Allah kwa kufuata maamrisho na makatazo yake
Madhehebu yake ni Hanaf,Malik,Shafi na Hanbal
Mungu angeumba ulimwengu ambao mabaya hayapo, hayajulikani, hayawezekani kufanyika, huyo aliyefanya mabaya angeweza kufanya mabaya?Kwa mfano hapa nakujibu mwenye kosa ni huyo anayefanya mabaya kwa sababu ameamua mwenyewe kuchagua mabaya wakati wenzie wakichagua mazuri
Majibu yako hayana mantiki.Sijajibu au hujafurahishwa na majibu yangu?
We endelea kutetea tu uovu lakini hilo ni kosa la mtu binafsi kwa kuchagua uovu badala ya uzuriMungu angeumba ulimwengu ambao mabaya hayapo, hayajulikani, hayawezekani kufanyika, huyo aliyefanya mabaya angeweza kufanya mabaya?
Mfano, Mungu angeumba ulimwengu ambao mauaji hayawezi kufanyika, watu wangeweza kuua?
Hata wewe maswali yako hayana mantikiMajibu yako hayana mantiki.
Mungu mjuzi wa yote anatujaribu ili iweje wakati yeye anajua yote na ndiye anatupa uwezo wa kufanya mema na mabaya na mipaka yake?
Sasa anatujaribu ili iweje wakati anajua kila kitu na yeye ndiye anayetupa uwezo?
Kwanza kabisa, hili si suala la mimi kutetea uovu, ni suala la kuhoji logical consistency, but I suspect you do not understand that.We endelea kutetea tu uovu lakini hilo ni kosa la mtu binafsi kwa kuchagua uovu badala ya uzuri
Bila shaka unatumia Google au AIUliyoyataja hapo ni vi-sub-part (shule za sheria) vya dhehebu la Sunni.
Endelea kuchimba zaidi ili ujue madhehebu makubwa ya Islam ni yapi.
Kisha uje utuambie kama Shia ni Islam au sio Islam.
Hata wewe maswali yako hayana mantiki
Nimekwambia amekuleta duniani ili hata akikuhukumu uwe na yakini kuwa kweli nastahili adhabu kwa niliyoyatenda
Kuhusu kuwepo kwa ulimwengu usio na maovu hajataka uwepo na ukimlazimisha kuwa angefanya hivyo huyo anakuwa sio Mungu tena ila ni babu yako