Kwa mara ya kwanza Vacation na familia yangu

Ng’ombe wapokee wengine kiko nilete mimiπŸ˜‚
Kwani una zizi umeandaa? Kwa ule mzigo niliouona Jana selfika, nakuletea fuso mbili kama za Mobetto 🀭
 
Niliposema mpunga hauliki bila mchuzi nilimaanisha kua,kuna vitu vya ziada nje ya kuamini kua hela ndio kila kitu,

Anyway nakuombea upate hela uzitakazo,uzizowee na kuona ni kitu cha kawaida tu,hapo ndio tunaweza kujadili na kuelewana.
 
Ricardo Kaka. Huyu mwamba hapa. Alimuoa binti mrembo sana. Walibahatika kupata watoto watatu. Familia yao ilikuwa bora sana. Waliishi kwa upendo na furaha.

Mwamba alijitahidi asimkwaze kwa chochote mke wake. Bahati Kaka alilelewa ktk malezi mema bora ya kikristo. Hivyo hakuwahi kuchepuka,hakuwa anakunywa pombe. Hakujihusisha na kamali kama ilivyo kawaida kwa vijana huko Brazil. Hakujihusisha na makundi kama ilivyo kawaida huko.

Bahati nzuri Kaka alikuwa na mkwanja mrefu. Hivyo mke wake alipata chochote alichohitaji ktk maisha yake. Yaani chochote. Mke alisafiri popote alipotaka.

Lakini pamoja na maisha yote hayo mwanamke bado aliomba takaka.

Alivyoulizwa kwa nini anaamua waachane katika familia bora ya Kaka?. Mwanamke alijibu wewe Kaka ni MKAMILIFU MNO. Hakuomba talaka ili wagawane Mali au kama ilivyo kawaida ya wanawake wengi tamaa ya mali.

Mwamba hakuwa na namna,japo kwa ukristo hakuruhusiwa kumuacha mke waliefunga nae ndoa. Lakini akaamua kumuacha mkewe aende kama alivyotaka.

PESA SIO KILA KITU
 

Attachments

  • Screenshot_2026-06-08-14-49-02-149_com.google.android.googlequicksearchbox.jpg
    214 KB · Views: 5
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…