Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

habar za midaa hii wana jamvi?
Nimeona nyuzi nyingi zikiwa na maswali mengi yakiusiana na BIASHARA GANI ZA KUFANYA KWA MTAJI MDOGO..
Bhaaaasi kwa wale wabishi,wavumilivu na wasiokata tamaa,msio ogopa biashara za kudharaulika angalau tunaeza peana mwanga jinsi ya pa kuanzia.

Kwa kifupi mimi ni kijana wa miaka 29 nimezaliwa kwenye maisha ya kishuani huko Arusha ila nilifukuzwaga nyumbani toka 2006.Hapo ndo nilipopata changamoto za kufanya biashara za mitaji midogo.
Katika biashara nilizowai kufanya zote nilifanikiwa.

AINA ZA BIASHARA
1:KULENGA NGUO ZA KIKE KUUZA VYUONI
2:KUUZA PIPI,MAJI YA KANDOROO NA SIGARA(Nyakati maalum)
3:MATOFALI YA KUCHOMA
4:KUUZA DAGAA LA KUOSHA
5:BANDA LA CHIPSI
6😛LAYSTATION(KUCHEZESHA MAGEMU)

Nyingine nashindwa kuziorodhesha kutokana na kupitwa na wakati.
Sitaweza kuchambua zote ila nitaanza kuchambua moja kwa sasa.

JE WEWE UNAWEZA KUUZA PIPI,MAJI YA KUFUNGA(Kandoroo enzi zile) NA SIGARA KIPINDI CHA SABA SABA AU NANE NANE?(SIKU 7/8 ZA MAFANIKIO)
Nilipewa wazo toka kwa house boy aliyefukuzwa hom miaka mingi.lilikua wazo gumu kwangu tokana na maisha niliyokulia ila nilijikaza nikafanya.

NILIANZA NA MTAJI WA ELFU 70(MOROGORO)
niliazima meza mbili kwa ajili ya kuwekea pipi,nilikodisha ice box mbili kwa ajili ya barafu,nilinunua ndo 8 za maji,nililipa kitambulisho cha mfanya biashara ili kupunguza gharama za kulipa kila nikiingia langoni mwa uwanja wa nane nane.

Nilinunua vifuko vya kufungia maji vya kutosha.nilinunua chujio kubwa. katika hii biashara maji ndo yalinipa pesa nyingi
Ndoo ya maji sh 100

Sikumbuki mahesabu yote kwa uhakika ila siku ya kwanza niliuza maji elfu 9 ikiwa kandoro moja ni tsh 50 wakati biashara ya pipi na sigara ikisua sua,siku ya pili niliuza maji ya elfu 12 biashara ilienda vizuri lakini ugumu maji yaliisha sikua na uwezo wa kufunga huku nikiuza biashara ya pipi.jion yake nikamualika mshikaj(house boy)usiku tukafunga maji mengi sana.siku ya tatu tuliuza elfu 24.

JION YA SIKU YA 3
Nilipata moyo sana nikaanza kuona faida ya biashara niliyokua naidharau.
Basi tukapata wazo la kuwaajiri vijana wanne kutoka kitaa usiku tunafunga maji.asubuh mpaka jion tunafanya biashara ya kuuza tu.pamoja na kufunga maji mengi sana.biashara ya pipi na sigara nayo ikachanganya sana.

Hakika mpaka inafika tarehe 5 tulikua tunauza mpaka maji laki mwaka huo Mungu alijalia jua lilikua la maana.maajabu ni tarehe sita saa 6 mchana maji yote yameisha na watu wanataka tuwauzie hata kwa glasi. Hapo ndo tulipopiga pesa wadau. Zile cooler box zilikua na kitu kama kabomba. Tukazijaza maji na barafu tukanunua na vikombe 10.

Sisi kazi yetu ilikua ni kujaza barafu na maji tu.kila glas ya maji sh 100. Uongo dhambi kama kuibiana lazima siku hiyo niliibiwa sana ila sikujali. Usiku wa tarehe nane tulilewa sana na vijana wangu.asubuh ya tarehe 9. Ndio nikapiga mahesabu nimebaki na laki 8.

Nikagawa laki 2 nikabaki na sita. Pipi zilizobaki nikaziuza kwa bei ya jumla kwa muuza duka elfu 50 tukasambaratika tarehe 10.

Nia ni kutaka kukutia moyo kama kweli unania. Pia changamoto zilikua ni nyingi sana. Mfano sehemu ya kupanga meza zilikuwa zinapangishwa kwa zaidi ya mtu mmoja. Mwenye nguvu ndiye anafanya biashara.
Nawasilisha
 
nimependa sana kujituma kwako...vipi kuhusu hii biashara ya playstation mkuu,inatoa kweli?
 
nimevutiwa sana na hii thread sema ni.ya mda.sijui kama.bado kutakuwa nafasi kwa group la whasap
 
Mkuu naomba uzoefu wa biashara ya Kupoint nguo..nataka kuianza
 
Kwaiyo saiv wewe tajiri
 
Sina mishemishe na nimemaliza chuo nursing ila mambo ya ajira siyaelewi ila ninakakimtaji kama laki 3 iv je nifanye biashara gani wadau life la kitaa gum eti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…