Kwa mtaji wa Shilingi laki moja hadi laki tisa (100,000 - 900,000) unaweza kufanya biashara gani?

Kazi ya UDOBI mkuu....tengeneza MEZA YA MBAO..
PASI YA MKAA....MASHUKA MATATU...MKAA debe MOJA.... SABUNI YA MBUNI MICHE 3... Sabuni YA UNGA... TOSS ndoo.1 NA NDOO 3 TUPU ZA PLASTIC kwa ajili ya kufulia....PESA kama 120000 utatoa kodi ya baraza..kwa mwezi 10000""unalipa mwaka mzima....na 5000 utalipia BANGO LA KIBAO CHA MATANGAZO. utakiandika kama ifuatavyo.....MTAALAM WA KUFUA NA KUPIGA PASI...YUPO HAPA...suruali ISIPOSIMAMA YENYWE BILA KUSHIKWA baada ya KUPIGWA PASI......unarudishiwa pesa zako... Mkuu lazima UTOKE TU....maisha hayo mkuu....
 
Hellow,wana jf nina mtaji wa laki moja..nilitaka kujua naweza anzisha biashara gani??
 
Bila kujali jinsia yako, unaweza kufanya bishara ya mboga mboga na matunda kwa kutembeza majumbani, waweza kuwa na beseni ama chochote ya kubebea, unaweza anzia hapo, kama upo Dar nakuhakikishia hutojuta
 
Pamoja na biashara ya mboga mboga, unaweza tengeneza ubuyu, karanga, tambi na crips na kuziuza kwa jumla kwa faida ndogo, Kwa laki 1 mtaji na vifaa inatosha kwa kuanzia
 
Hapana unaweza kama upo dar,..angalia bidhaa online kupitia alibaba na wengine (fanya research kwanza)agiva Vitu vidogo vinavoweza kuuzika haraka apa tz,..chukua vya bei ya chini lakin vipo in high demand,..then see urself grow as fast as rocket jet
 
Hapana unaweza kama upo dar,..angalia bidhaa online kupitia alibaba na wengine (fanya research kwanza)agiva Vitu vidogo vinavoweza kuuzika haraka apa tz,..chukua vya bei ya chini lakin vipo in high demand,..then see itself grow as fast as rocket jet
like what mkuu eg.
 
Je unaweza kunipa changamoto kubwa inayowakuta ukiwa unafanya mradi huu.
Bila kusahau kila kazi ina vikwazo.

Hapa katika mradi huu utakutana na vitu vikuu vifuatavyo.
1.magonjwa
2.soko

Ukiweza kuwa mwangalifu kuwakinga na kutibu magonjwa ndo unaelekea kwenye uvunaji mzuri wa mazao ya huu mradi.

Pia unatakiwa utoke utafute soko katika maeneo mbalimbali(maofisini na taasisi bila kusahau watu wenye shughuli za harusi).

Ukiweza watengeneze vizuri na kuwapaki kwa kilo moja(1kg) then tafuta frame(duka la vitoweo/nyama ya kuku).

Kwa haraka haraka vikwazo ndo hivyo na njia za kutatua ndo hizo nilizojaribu kueleza hapo, na zingine unaweza angalia mazingira yanayokuzunguka.
 
Acha kumpoteza mwenzio.
Hyo kazi ya kijungu jiko.
 
Asante hebu nifuatilie hii
 
Habari Wakuu
.
.
Nimehitimu kidato cha sita wiki iliyopita na sasa nasubiria matokeo ya mtihani huo lakini.
kwa bahati nzuri nilijiwekea Akiba ya Pesa kiasi cha Elfu hamsini ambayo nahitaji kuitumia kuanzisha biashara ambayo naweza kuifanya kwa wakati huu badala ya kukaa nyumbani bila kazi na kusubiria ugali au kucheki movie na kupoteza mda bila sababu.
.
.
Changamoto yangu ni kuwa cjui nijishughulishe na biashara gani ambayo inaweza kuanzia na kiasi hicho cha fedha.
.
Tafadhalini wakuu naombeni mawazo na ushauri wenu
.
Nifanye nini?
 
Mmmh,hiyo pesa ndogo sana labda ufanye biashara ya karanga na vocha,biscuits,pipi,sigara nk.
 
Kwanza Pole kwa changamoto za kubezwa nabaadhi ya wadau humu Sijui nao huwa

Hawaombi ushauri Binadamu nikama ibilisi wa binadamu mwenzie anapenda anavyo vifanya yeye viwe sahihi kulilko la mwingine

Is not fear

Naenda kuku shauri mkuu kama unaweza wekeza katika mifugo hasa ya kuku wa nyama utaingiza zaidi ya pesa hiyo ukitaka ushaur zaidi pm

Nautatengeneza ajira pia kwa wengine
 
Kama unania kweli ya biashara kanunue u- fresh ni maji yaliyowekwa ladha na rangi box(ice cream za wanafunzi) ni 4000tsh na zinakaa 100 na zinauzwa kila moja 100tsh.
100*100=10000
Hapo faida ni 6000

Haya kwa hy 50000
Nunua box 8 kwa 32000
Itabaki 18000
Kama unaweza kukomaa nauli kutoka tegeta kiwandani popote kwa dar haizidi 10000
Hiyo 8000 ongeza umeme nyumbani ili uzigandishe tayari kwa biashara

Box 8 * idadi ya pc 100=800
800*100=80000
80000-50000=30000
Faida ni 25000-30000

Aya kijana kazi kwako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…