Kwa muda mfupi sana kiongozi wa Tanzania alipata maadui wengi sana

Kwa muda mfupi sana kiongozi wa Tanzania alipata maadui wengi sana

Hivi wewe hata siku moja hukui ukabadilika kidogo?

Sasa unaniuliza swali la kipuuzi namna hiyo, unataka nikwambie kitu gani. Unataka unifundishe nikikwambia kuwa sijui?

Kama naijua historia hiyo, unataka niiandike yote humu JF?

Una mambo ya kitoto sana wewe.

Mabandiko yako yote ni ya kipuuzi puuzi tu!

Tumia ukumbi huu ukusaidie kupanua mawazo na ujadiliane na wengine kwa utulivu.
Kama mabandiko ni ya kipuuzi mbona umewashwa kuchangia? Unajifanya mjuaji. Nimekuuliza unajua Mao Zhedong aliifanyia nini China kama kiongozi aliyekuwa ana ushawishi binafsi unabaki unaharisha.
 
Kama mabandiko ni ya kipuuzi mbona umewashwa makalio kuchangia? Huna akili zaidi ya kujifanya mjuaji. Nimekuuliza unajua Mao Zhedong aliifanyia nini China kama kiongozi aliyekuwa ana ushawishi binafsi unabaki unaharisha.
Nimekwishakueleza, na umeelewa. Hilo ndilo muhimu.
 
Marehemu alichofanikiwa ni propaganda za hadaa kwa wajinga. Na aliwaokota wengi.

Utawala wa awamu ya 5, kwa vigezo vyote vya maendeleo, alifeli kabisa.

Ukuaji wa uwekezaji aliuangusha toka 28% mpaka 4%, wajinga hawajui.

Ukuaji wa mapato ya utalii, aliyaangusha kutoka 15% mpaka 3.6%, wajinga hawajui.

Thamani ya mauzo ya mazao ya kilimo aliyaangusha kwa 50%, wajinga hawajui.

Kwenye uzalishaji dhahabu, aliiangusha Tanzania toka kuwa mzalishaji wa 3/4 (kuna wakati tulikuwa tunakuwa wa 3, na wakati
mwingine wa 4) barani Afrika mpaka kuwa mzalishaji wa 6.

Aliyaharibu mazingira ya uwekezaji katika sekta ya madini, toka nchi ya 74 bora mpaka kuwa nchi ya mwisho.
Jk alikuwa hakusanyi Kodi kutoka kwa hao wawekezaji ndiomaana waliitana wengi kuja kuwekeza maana walikuwa wakipiga hela bila kusumbuliwa, JPM aliamua tu kufuata sheria kuhakikisha wanalipa Kodi stahiki ndio maana wawekezaji uchwara walianza kukimbia
 
sijui una umri gani kiongozi,ila wewe ni kati ya watu wazima wajinga sana.

nyinyi wazembe wachache ndio matokeo ya tz hii ilipo zaidi ya miaka 50 ya uhuru.
Sasa hao wazembe wachache madhara yao yanafunika vipi jitihada za wachapakazi wengi?
 
Kwanza kabisa ni wanachama wenzake ambao walishazoea kupiga madili makubwa. Hawa walishazoea kukwapua mabil ya shilingi na wao huona kama wamekwapua shilingi elfu moja. Hawa walishamchukia sana kwa kuziba mianya yao ya upigaji.

Pili ni wanasiasa wa upinzani ambao baada ya kusambaratisha vyama vyao nao wakawa hoi kisiasa. Na vyama vyao vikwa vimeyumba kisiasa na kiuchumi.

Tatu ni wananchi ambao wengi walimuona kama kiongozi ambae ni dikteta hawa wengi walidai kupoteza jamaa zao au ndugu zao kwa kile kilichodaiwa ni watu wasiojulikana.

Nne ni wafanyabiashara ambao walizoea kuhujumu uchumi kwa kutengeneza bidhaa bandia, kukwepa kodi, wengi walikamatwa na kukwepa kodi na walikuwa magerezani kwa kuhujumu uchumi

Tano ni matapeli na wapigaji hawa walishazoea kulipwa mabilioni ya senti kwa kuwa na kampuni za mfukoni na walikuwa wakilipwa hata kama hwajafanya kazi.

Kwa ujumla kiongozi alikuwa na maadui wengii sana kwa muda mfupi.

Hivi ndivyo Africa ilivyo.
Kwa mara ya kwanza nakupongeza
 
Wachina walikwenda hivi kwa miaka isiyopungua 20 na leo tunawaona wako hapa ila sie miaka 5 tu ndg yetu washamuwaisha ahera, haitatokea tukajitegemea watanzania na daima tutaendelea kutawaliwa na kuonewa. Tumechukua upande wa wakataa pema sasa pabaya pametuita rasmi
Pole kifo cha mama mdogo wako
 
Muda utasema tu kiongozi tatizo la watanzania wengi hawana uzalendo na wanapenda kuishi kiujanja ujanja na kifisadi bila kufanya kazi.
Shida wengi wenu mnadhani kuwa masikini ndio uzalendo mmekaririshwa ujinga na nyie bila kujielewa mnadhani ni sifa. Aliyejifanya mtetezi na myonge mwenzenu kumbe yeye anapiga za kutosha halafu anawadanganya nyie mazumbukuku kuwa ni masikini mwenzenu
 
Wachina walikwenda hivi kwa miaka isiyopungua 20 na leo tunawaona wako hapa ila sie miaka 5 tu ndg yetu washamuwaisha ahera, haitatokea tukajitegemea watanzania na daima tutaendelea kutawaliwa na kuonewa. Tumechukua upande wa wakataa pema sasa pabaya pametuita rasmi
Wakati wa mapinduzi ya Kijani,China ilitumia jeshi kuhakikisha wananchi wanafanya kazi.
Rushwa ,upendeleo,ukabila,havikukubarika,
Wananchi walipitia Hari ngumu lakini waliona matokeo,
Sasa huwezi kulinganisha juhudi za Mao se tung,na Jiwe,Jiwe alizuia wengine wasiibe Ili aibe yeye na maswaiba zake,Mfano mdogo tu Makonda aliingiza mzigo wa magari akidai ni viti vya shule Ili asilipe kodi,Hakutumbuliwa.
Jiwe alichukua tender ya uwanja wa Chato akampa shemeji yake,bila kufata taratibu za tender,hii china unapigwa risasi.
Jiwe alikuwa muhongo sana,miradi ya flyover za Dar ilibuniwa kipindi Cha Kikwete na inajengwa kwa pesa za UN na Ulaya.
Siku hizi mapato yote yanakusanywa na TRA,halmashauri zimezuiwa kukusanya,hakuna kilichoongezeka.
Jiwe halikuwa haambiriki,Mkabila,much know nyingi,hafati Sheria.Bora limeenda.
 
Hawa watakataa unayoyasema.

1. Wale waliopotea na waliopotelewa na ndugu zao katika mazingira tata
2. Wale waliochukuliwa mali zao kidhalimu na ma-task force
3. Wale walipelekwa magerazani kwa miezi na miaka kwa kesi za kubumba
4. Walipoteza maisha katika chaguzi kama Akwilina
5. Waliopoteza biashara kama Kwanza TV na Mbowe
6. Walionyang'anywa passports kama Eyakuze
7. Waliochafuliwa wanafanya biashara za madawa na kipendwa chake bashite
8. Waliopoteza kazi zao kwa mkono na niaovu kama Fatma Karume
9. Wakulima Ambao hawakupewa pesa zao za korosho
10. Waliobomolewa nyumba zao Kimara
Orodha ni ndefu sana ya mambo ya namna hii
 
Unasema huvyo kwa sababu hukuwahi kuguswa wakati wa utawala wa yule shetani. Mimi ni mhanga niligombea nafasi Fulani ndani ya chama Fulani tena ni chama cha wafanyakazi tu. Kilichotokea ni maajabu. Kwa kuwa walihisi nipo upande wa pili, nilitekwa nikalazimishwa kujiunga na upande wa kijani. Niliyoyaona huko sithubutu hata kumuomba dua yule kayafa. Mungu amlaze mahali panapostahili.
Wewe usiwafanye watu wajinga Chama cha wafanyakazi kinauhusiano gani na siasa acha uujinga peleka huko kwa wenzio hukumu ndani sio size yako, unatengeneza maneno huenda hata elimu huna nenda kalime na upambane na maisha yako.
 
Zamani vilikuwa ni matawi ya CCM, sasa mwendazake alikuwa anataka kuturudisha huko, si unaona bunge limekuwa la chama kimoja kama zamani, hakuna cha ajabu hapo.
 
Wachina walikwenda hivi kwa miaka isiyopungua 20 na leo tunawaona wako hapa ila sie miaka 5 tu ndg yetu washamuwaisha ahera, haitatokea tukajitegemea watanzania na daima tutaendelea kutawaliwa na kuonewa. Tumechukua upande wa wakataa pema sasa pabaya pametuita rasmi
Hatuwezi kurudi kule kwenye enzi za ujima eti kisa ndivyo wachina walivyoendelea.
Toa na mifano ya mataifa mengine makubwa basi, au huyaoni? USA, Ujerumani, Ufaransa, UK, Hispania nk.
Ukatili, uonevu ,kuua wenzako kwa kisingizio cha maendeleo haikubaliki.
Isitoshe alikuwa mpigaji kama wapigaji wengine.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Wachina walikwenda hivi kwa miaka isiyopungua 20 na leo tunawaona wako hapa ila sie miaka 5 tu ndg yetu washamuwaisha ahera, haitatokea tukajitegemea watanzania na daima tutaendelea kutawaliwa na kuonewa. Tumechukua upande wa wakataa pema sasa pabaya pametuita rasmi
Eti wachina 🤣🤣🤣🤣
 
Motion ya huyo hayati wenu haikua na uelekeo wa kutupeleka uchina,ngoma ilikuwa inaelekea ZIMBABWE acheni kufananisha uharo na futari.
NIPO WAZI KABISA SIKUMPENDA JAMAA YENU HAKUWA KIONGOZI RAFIKI WA WATANZANIA.
Ficha chuki za kijinga, hakuwa rafiki yako wewe na Mzee wa MIGA labda.

Watanzania walimpenda sana kwa uzalendowake na kazinzuri alizo wafanyia nandio maana walimlilia kwa mamilioni.
 
Kwanza kabisa ni wanachama wenzake ambao walishazoea kupiga madili makubwa. Hawa walishazoea kukwapua mabil ya shilingi na wao huona kama wamekwapua shilingi elfu moja. Hawa walishamchukia sana kwa kuziba mianya yao ya upigaji.

Pili ni wanasiasa wa upinzani ambao baada ya kusambaratisha vyama vyao nao wakawa hoi kisiasa. Na vyama vyao vikwa vimeyumba kisiasa na kiuchumi.

Tatu ni wananchi ambao wengi walimuona kama kiongozi ambae ni dikteta hawa wengi walidai kupoteza jamaa zao au ndugu zao kwa kile kilichodaiwa ni watu wasiojulikana.

Nne ni wafanyabiashara ambao walizoea kuhujumu uchumi kwa kutengeneza bidhaa bandia, kukwepa kodi, wengi walikamatwa na kukwepa kodi na walikuwa magerezani kwa kuhujumu uchumi

Tano ni matapeli na wapigaji hawa walishazoea kulipwa mabilioni ya senti kwa kuwa na kampuni za mfukoni na walikuwa wakilipwa hata kama hawajafanya kazi.

Kwa ujumla kiongozi alikuwa na maadui wengii sana kwa muda mfupi.

Hivi ndivyo Africa ilivyo.
Hakuheshimu katiba
Alizuia nyongeza ya mishahara ambayo ipo kikatiba.
Alionea sana watu
Wasiojulikana walishamiri
Kikokotoo cha uonevu
Ubinafsi(Airport kijijini kwake)
Kushamiri kwa kesi za uhujumu uchumi ili kuwasotesha watu jela.
Kutumia task force kuharibu biashara za watu.
Kukumbatia viongozi waovu.

Kunyang'anya UHURU wetu (halafu eti kila j.pili kanisani kutoa vijembe)

Kwani ilishindikana nini kufanya maendeleo bila kuyanfanya yote hayo hapo juu?

HE WAS WRONG.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom