Kwangu mimi hawa ndio wachezaji bora wa muda wote kwa timu za Yanga na Simba na Taifa Stars miaka ya 90s, wewe je?

Kwangu mimi hawa ndio wachezaji bora wa muda wote kwa timu za Yanga na Simba na Taifa Stars miaka ya 90s, wewe je?

Simba tu (3-4-3)
1.Juma kaseja
2.Shomary kapombe
3.Pawasa
4.Yondani
5.Wawa
6.Matola
7.Okwi
8.Boban
9.Ema Gabriel
10.Chama
11.Mogela.


Yanga 4-4-2

Mapunda
Nsajigwa
Maftah
Canavaro
Ken mkapa
Fredy Mbuna
Abdi kasimu
Ngasa
Tabwe
Makambo
Said maulid


Nb,sijasoma umeandika vibaya
Yanga bila Lunyamila haijakamilika, halafu huyo Makambo toa weka Mohamed Hussein "Mmachinga"
 
Kumbe Musa Hassan Mgosi alikua wa kawaida eee?

Alafu kumbe Makambo amefanya makubwa Jangwani kumshinda Jerryson Tegete?
Mgosi huwezi kumlinganisha na ema Gabriel ama Zamoyoni Mongela.

Makambo kwangu Mimi ni bora zaidi hata ya mayele
 
Swadakta kabisa mkuu.
Yanga
1. Hamis Kinye
2. Yusuph Ismail Bana
3 Ahmed Amasha
4. Shomari
5.Isihaka Hassan
6 Juma Mkambi
7. Omar
8. Mkwassa
9. Homa ya Jiji
10 Abeid
11 Hanzuruni " mchawi'

Simba
1 Mahadhi/ Mambo sasa
2. Kiwhelo Mussa
3 Mohamed Kajole
4.
5 Mohamed Bakar Tall
6 Nicodemus Njohole
7
8 Ngulungu
9 Malota
10. Zamoyoni
11 Thuwen Ally
Thuwen Ally alicheza miaka ya 70 huko
 
Fred felix Minziro..
Juma Pondamali.
Salum kabunda.
Godwin Aswile Scania.
Saidi Zimbwe.
Michael Paul.
Hamis Gaga.
Gebo peter.
Twaha Hamidu.
Alphonce Modest.
Madaraka Selemani.
Idd Selemani.
Julio aka Mtwa...aka Mwana..
Hussein Masha.
Iddi Mkuki.
Nico Bambaga.
Mustafa Hoza.
Iddi Pazi.
Mohamedi mwameja
Lunyamira.
Edo boy, Edo chumira..
Malota soma
Juma Amir
Issa Athumani Mgaya.
Kasongo Athumani
Ramadhani Lenny.
Dua Bin Said.
Samora Said.
Nteze John.
George Masatu...


Soka ilipigwa acha mchezo, sio hawa wanyoa viduku....watu walikuwa physic acha kabisa...
 
1.Juma K Juma
2.Amri said
3.Ramadhani Waso
4.Bonifas Pawasa
5. Serg Pascal Wawa
6. Seleman Matola
7.cloutas chota Chama
8 Madaraka Selemani
9 Athuman Machupa
10 Emanuel Okwi
11.Luis Miqussone
Kikosi chochote cha Simba cha miaka ya 1985-90s kama hakuna Mohamed Mwameja(TZ one), Hussein Amani Masha, George Magere Masatu na Hamis Thobias "Gagarino"hicho ni feki. Kikosi cha Yanga kwa miaka hiyo, Kenneth Pius Mkapa, Issa Athuman Mgaya, Peter Tino (nguguye Gebo Peter) na Athuman Abdallah China pia hicho ni feki. Kikosi cha SC Villa, Paul Hasule, George Ssemogerere, Majid Musisi pia hicho feki.
 
1.Juma K Juma
2.Amri said
3.Ramadhani Waso
4.Bonifas Pawasa
5. Serg Pascal Wawa
6. Seleman Matola
7.cloutas chota Chama
8 Madaraka Selemani
9 Athuman Machupa
10 Emanuel Okwi
11.Luis Miqussone
Okwi vipi?
 
Habari zenu wana JF wenzangu. Ama baada ya salam, sasa ningependa nijielekeze kwenye mada husika. Ndugu wana JF kabla ya kuandika list ya wachezaji bora wa muda wote wa timu za Yanga na Simba, ningependa kwanza nijitambulishe kuwa mimi ni mshabiki mkubwa sana wa timu ya Yanga. Nimeanza kuipenda Yanga toka nilipoanza kupata akili na mpaka leo sijawahi kubadilisha msimamo wangu huo, pamoja na changamoto zote tunazozipitia na tulizozipitia huko nyuma. Nakumbuka miaka ya 90s kila time ilikuwa na tawi lake mtaani. Kwahiyo ilikuwa ni kawaida timu ya Yanga inapoifunga Simba, basi wana Yanga wote tunatoka katika maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es salaam, na kukimbilia Jangwani kuwapokea wachezaji wetu, huku tukiimba nyimbo mbali mbali za kuwasifu wachezaji wetu na timu yetu. Hivyo hivyo kwa upande wa Simba, walipopata ushindi wao dhidi ya Yanga, wana Simba nao walitoka katika maeneo mbali mbali ya jiji na kuelekea Msimbazi kuilaki timu yao. Kwahiyo naweza kusema kwangu mimi hakuna kipindi kilichokuwa kitamu kwa furaha ya michezo kama kipindi hicho. Hapa chini naweka kikosi kazi cha wachezaji wa Yanga ambao walikuwa tishio sana miaka hiyo. 1) Goli kipa- Steven Nemes, huyu hakuna mtu wa miaka hiyo, asiejua kazi kubwa aliyoifanya kwa timu ya Yanga pamoja na timu yetu ya Taifa (jamaa utahisi alikuwa na simaku mikononi kwa jinsi alivyoivuta mipira mikononi mwake). 2) Difenda- Mwanamtwa Kihwelo, huyu kumpita ilikuwa ni kazi ngumu sana kwa vile alikuwa na akili ya kile anachokifanya uwanjani (kwake yeye ilikuwa ni bora mpira upite ila mchezaji abaki, au mchezaji akipita basi mpira utabaki) 3) Keneth Mkapa, mkongwe halisi na moto wa kuotea mbali ambae hajawahi kutoa boko au kuharibu mpira hata siku moja (mkapa hata timu za nje zilikuwa zinamhofia sana, kutokana na umahiri mkubwa wa uchezaji wake). 4) Midfielders- Sanifu Lazaro, ukipenda mwite Mwiba (sifa zake hazina shaka kiuchezaji). 5) Thomas Kipese, winga machachari ya kushoto (ilikuwa ukimpa pasi anatembea na mpira mdogo mdogo, maana wachezaji wa timu pinzani walikuwa wanaogopa kumfuata asiwadhalilishe kwa kanzu au tobo. 6) Salvatory Edward, mzee wa pasi to pasi. 7) Nico Bambaga, kichoteo (yani alikuwa akishika mpira anauchota tu mpaka kwa mfungaji, sasa hapo inabaki kazi ya mfungaji, afunge au atoe nje) 8) Forwards- Salumu Kabunda, tingatinga (jamaa alikuwa kajaa kama mzee wa "GYM" afu misuli iliyokakamaa kiasi kwamba ukipigana nae bambi lazima utoke nje ukapokee matibabu) 9) Shaban Nonda (Mkongo), huyu nae hakuwa nyuma katika kufanya kile kilichompeleka uwanjani. 10) Saidi Mwamba Kizote, mzee wa kunyakuwa (alikuwa na uwezo wa kunyakua mpira juu ya kichwa cha mtu kupitia miguu yake mirefu tena bila kumgusa aliechukuliwa mpira) kwa ufungaji pia alikuwa tishio, George Weah hatosahau siku aliyopigwa tobo na baadae kanzu na mzee huyu wa kiminyio. wengi tulimfananisha na Rivaldo wa Brazil. 11) Edibilly Jonas Lunyamila, huyu hata ukienda Rwanda, Congo, Burundi, Zambia, Kaburu na kwengineko wanamfahamu fika kwa umahiri wake wa kutambaa na mpira hasa pembezoni mwa chaki, (mabeki walikuwa wanasakiziana kumfuata) na yeye alitumia mwanya huo kufanya yake, kwa kufunga magoli mengi. Nikija upande wa Simba naweza kusema wachezaji wao wengi nimewasahau ila kuna baadhi nawakumbuka kama vile 1) Goli kipa- Mohammed Mwameja, Tanzania one (huyu aliisaidia sana Simba na Taifa Stars, mpaka kuna watu walihisi labda jamaa ana mikono mingine pemben ya akiba) 2) Difender- Alphonsi Modest. 3) Husein Marsha. 4) Forwards kuna- Dua Saidi. 5) Madaraka Selemani, "mzee wa kiminyio" , yani alikuwa anatisha kama anaenda mbele afu anauminya mpira, beki anajikuta kapitiliza mzima mzima afu yeye anamua atoe pasi au aendelee na mpira akafunge. Hao ni baadhi ya wachezaji hodari na mahiri wa timu hizo wa muda wote. Ila kama kuna mdau mungine aliekuwa anafatilia timu hizi, na michezo kwa ujumla anaweza akaongeza wengine tuliowasahau kutoka hata timu zingine kongwe za miaka hiyo. Karibuni. Mods ndugu zangu, tafadhalini naomba uzi huu muuache ujitegemee ili kuweka kumbukumbu nzuri.
Mimi nilikuwa Simba damu. Ndugu yetu alikuwa ni mmoja wa viongozi wa Simba, kwa jina aliitwa Ismail Kaminambeo, kwa sasa ni marehemu.
 
Mwameja
Kapombe
Twaha hamidu
Costa nampoka
Masatu
Mkude
Mashine abduli
Masha husein
Leny ramadhan
Chama
Kagere
 
Huna hata unalolijua.
Binti,nafuatilia mpira tangu 88,nimeona wachezaji wengi,wengi wanaocheza Leo ligi kuu,miaka ya 90 wasingekua ligi kuu(ikiitwa ligi daraja la kwanza) Wala ligi daraja la pili,mgosi nimemuona Sana Simba pale,goli alikua mshambuliaji Bora kuliko mgosi,mgosi kupiga mpaka ajiandae!
 
Mwameja
Kapombe
Twaha hamidu
Costa nampoka
Masatu
Mkude
Mashine abduli
Masha husein
Leny ramadhan
Chama
Kagere
Yaani chumila hayupo!!?..dua bin said,kimti...1990s wamepita wachezaji mjomba,inasikitisha kuona Simba na yanga leo wanaocheza akina sakho,mugalu,yikpe,molinga
 
Salum Kabunda Ninja alikuwa beki sio forward, list yako haitakamilika usipowataja Constantine Kimanda na marehemu Method Mogela
Asante mkuu kwa ukumbusho wako. Dah umenikumbusha mbali sana, mpaka nahisi machozi kunitoka. Constantine Kimanda nilijua nimemuweka kwenye list kumbe nimemsahau, sasa hivi ashakuwa marehemu. Method Mogela nilimtaja kwa comment fulan ya chini.
 
Hizi ni enzi nimeshakata shauri kufuatilua mpira, nilikua shabiki wa Yanga kupitiliza Hadi walipofungwa Kwa penalties Zanzibar usiku. David Mwakalebela alikosa penalty akaipa Simba ushindi.

Bila kujali timu walizichezea, Hawa jamaa walivuma enzi hizo.

Sanifu Lazaro ( Tingisha)
Said Swed hii ilijulikana kama scud
Makumbu Juma
Hamiss Thobias Gagarino
Said Mwamba Kizota
Thomas Kipese (Uncle Tom)
Mkuu wewe ni kama mimi. Mara ya mwisho kufuatilia mambo ya mpira ilikuwa 2001. Na hii sio kwa club zetu tu, bali hata kwa club za ulaya pia niliachana nazo maana mwaka huo ndio ule uhondo wa mpira wa dunia ulipoishia. Kwa upande wa nje mimi nilikuwa shabiki mkubwa wa Man United, huku Tanzania mimi na familia yetu yote kuanzia wazazi mpaka ndugu wa kuzaliwa tukiwa Yanga.
 
Binti,nafuatilia mpira tangu 88,nimeona wachezaji wengi,wengi wanaocheza Leo ligi kuu,miaka ya 90 wasingekua ligi kuu(ikiitwa ligi daraja la kwanza) Wala ligi daraja la pili,mgosi nimemuona Sana Simba pale,goli alikua mshambuliaji Bora kuliko mgosi,mgosi kupiga mpaka ajiandae!
Nimeamini kuwa wewe ni mwana michezo wa kweli, maana sikutegemea kama ungeweza kumfahamu mpaka Edward Chumila hapo chini. Dah kweli enzi zetu tulifaidi sana mkuu.
 
Yaani chumila hayupo!!?..dua bin said,kimti...1990s wamepita wachezaji mjomba,inasikitisha kuona Simba na yanga leo wanaocheza akina sakho,mugalu,yikpe,molinga
Wengi hapa wamewasahau Makumbi Juma na Hamis Gagalino "mwamba".
 
Back
Top Bottom