My love...Kwa ruhusa yko naomba nichangie kidogo
Ndoa yenye afya ni Ile yenye utulivu na upendo,na ukiacha mambo yote utulivu ndio kila kitu.
Sasa mwanamke mtiifu kwa mumewe huleta Sana utulivu na upendo katika ndoa
Na
Utiifu uonekane katika namna unavyoongea na mumeo, utiifu katika kutekeleza maagizo yake, na utiifu hata katika kutoa ushauri pia.
Hakikisha unatimiza majukumu yako kama mke pale nyumbani kwako, mume anapenda kufanyiwa mambo mbali mbali na mkewe, mfano kupikiwa chakula,usafi WA nguo zake. Hata Kama mke nae anaenda kazini basi walau siku moja moja apatapo nafasi aingie jikoni na mume atajisikia burudani kabisa.
Mwanamke siku zote ainamishe bawa lake Chini, ajishushe hata kama ana mashahara mkubwa kuliko mumewe au cheo, atambue pale nyumbani atabakia kuwa mke Tu,na akifanikiwa katika Hilo atauteka Sana moyo WA mumewe .
Aepuke haya yafuatayo:
Kumpandishia mwanaume sauti juu katika mikwaruzo, yaani akifanya hivyo ujue amechokoza nyuki
Asionyeshe dharau yoyote Ile kwa mumewe
Na hata kama kuna jambo ambalo halipendi kwa mumewe basi amfikishie ujumbe katika namna ambayo haita vunja hadhi na utu WA mwanaume.
Shukrani.