Kwanini baadhi ya "wanajeshi" wetu wana vitambi?

Kwanini baadhi ya "wanajeshi" wetu wana vitambi?

Walengwa hapa ni JWTZ, POLISI, JKT, Magereza na Zimamoto!

Wengi wa askari wenye vitambi ni "mabosi'

Vitambi kwa askari wa vyeo vya juu vina manufaa gani kwao na kwa Taifa?

Wanajua kuwa hivyo vitambi vinatusababisha "sisi" tusio na uzoefu wa masuala ya Kijeshi tuwaone kuwa ni wazembe? Mbona wenzao wa China, North Korea , na Rwanda hawana vitambi?

Wanajua kuwa wao ni mfano wa askari wa chini? Kwa kuwa wanasema "like the son, like the father", watajisikiaje siku moja wakigundua kuwa askari wote wanaowaongoza nao wan vitambi kama wao?

Hivi kukitokea dharura itakayowalazimu kukimbia kwa masaa matatu mfululizo si wanaweza wakahisi ulimi unataka kutoka?

Kwa nini "wanajeshi" wetu, japo siyo wote, wana vitambi?
Uzi huu bila picha ni umbea.
 
Matokeo ya ulaji mbovu na kubweteka.
iu

😌
 
Hawana kazi za kufanya, mishahara minono, muda mwingi wamekaa tu

Si wangekuwa wanatumika kwenye miradi ya ujenzi wa hospitali, barabara, vyuo au shule za serikali?
Wakati RC wa Dar alivyowataka wakasafishe barabara, wengi walihemuka humu.

Wacha wajinenepeeee
 
Sasa Trafik kuvaa nguo nyeupe na kusimama katikati ya barabara kuanza kukusanya rushwa ya buk 5 ni mpaka mazoezi hata wewe hapo siunaweza tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna chuma kimoja niliwahi kukiona kilikuwa mazingira ya (mlio wa kengele) kwa sasa kimestaafu alikuwa S/Sgt ana hicho kitambi kweli ila ni balaa combination za K/combat zimetubu.
Hivyo vikwazo vinavyorukwa acha tu, kwahiyo wapo wengine wana maumbile hayo ila wepesi.
 
Drill Sargent [emoji23]
Ndio Mkuu.
au ni makelele tu juu ya wenye vitambi.

Ki uhalisia, wanajeshi, polisi n.k wanapaswa kuwa fit kabisa, kama alivyoelezea mleta mada. Lakini haimanishi majeshi yote au wanajeshi wote wanafanya kazi za kukimbizana na kubingirika.
 
Back
Top Bottom