Kwanini huwa tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati ardhi tumeikuta ipo bure? Why?

Yesu alishamaliza huu utata siku nyingi, aliwaambia ya Kaizari mpeni Kaizari.

Wengi hawajui Yesu alikuwa analipa kodi, kwahiyo Hakuna kiumbe yoyote wa kushindana na mfumo huu, huu siyo mfumo kristo, huu ni mfumo Babylon.
Sasa nimeweka jengo ambalo serikali hailimiliki wala haina ubia kisha inanidai kodi.

Soon wataleta air regulators watulazimishe tuzivae ili tulipie kodi ya oksijeni
 
Yesu alishindwa kuwajibu Wayahudi swali hili hili, akawaambia ya Kaizari mpeni Kaizari.

Kumbuka Yesu alikuwa analipa kodi na kuna watu wanaamini Yesu ni Mungu, Imagine.
Hilo andiko kalisome vizuri hujalielewa!
Hapa tunaongelea kwanini tunalipia kodi ya ardhi wakati ardhi ni BURE! Bali miundombinu ndiyo inalipiwa na huwa tunailipia? Tunalipia kila kitu tunakatwa kodi kila idara V.A.T
 
Sasa nimeweka jengo ambalo serikali hailimiliki wala haina ubia kisha inanidai kodi.

Soon wataleta air regulators watulazimishe tuzivae ili tulipie kodi ya oksijeni
Unajuwa kimsingi Watanzania wengi sana wana uwezo wa kumiliki magari kwa bei yanaouzwa huko Japan na ulaya, lakini wakishaingia TRA tu hapo ni nuksi tayari hata hamu ya gari inakuisha hapohapo.

Niliwahi kusikia Ghaddafi kwenye utawala wake Libya aliifuta kodi ya VAT.
 
Kumbe ardhi ni bure kisa kaumba Mungu mbona mimi sina Basi ngoja nikajikatie kipande changu pale posta na mimi niwe naye
Hujaelewa mada.
Tofautisha kati ya kodi na mauziano.
Mauziano ya ardhi huwa ni makabidhiano ya ardhi kutoka kwa mmiliki wa mwanzo aliyewahi kwenda kwa mmiliki mpya(aliyechelewa kuipata) na malipo hufanyika mara moja tu.
Lakini kodi ni tozo kwa mmiliki wa ardhi na ambayo hujirudia mara kwa mara na hii ndio hoja ya mtoa mada
 
Usisahau:
Maji tunalipia pia
Hwwa tunayovuta tunalipia
Hewa hatulipii,maji pia hatulipii bali tunacholipia pale ni huduma ya kusafishiwa na kusogezewa karibu.
Nenda kachote maji ya mtoni au kisimani kama kuna mtu atakudai pesa
 
Ili wengine wanunue V8
 
Serikali yetu huwa inafuata masharti ya WB na IMF. Haijawwhi kusikia na kupokea maoni ya raia wake.

Bahati nzuri asilimia kubwa ya watendaji ni wezi wa rasilimali na fedha za umma na wwkistaafu wanajisimika madarakani kupitia CCM.

Mabadiliko ni muhimu
 
Unaweza kunionesha hewa? Mimi naweza kukuonesha oxygen inayotozwa kodi.
Hewa ni pamoja na oksjeni katika mchanganyiko wake halisia!
Ukiichakata kiwandani unakuwa kama unaivuna!
Hivyo unapoitoa katika uhalisia maana yake umewekeza unatafta faida!
Ardhi ni udongo katika uhalisia wake ukichambua udongo ili upate kokoto ni halali kuuza na kuuziwa!
Lakini katika uhalisia wake ardhi hatutakiwi kutozwa kodi ya ardhi kabisa! Maana bila mkono wa binadam ardhi IPO tayali kama hewa!
 

Kwa ufupi,
1. Kodi lazima ilipwe kwa mfalme. Hiyo ni tanguy zama hizo.
2. Kumpa mtu umiliki kamili (absolute ownership) wa ardhi ambaye hana uwezo wa kuilinda kisheria, kiusalama, kijeshi nk. ni hatari kwa mstakabali mzima wa taifa lolote. Ukisema ardhi, maana yake ni nyumbani, maana yake ni nchi. Sasa vitus kama hivi haviwezi kuachwa vivi hivi.
3. Sheria inatambua kuwa ardhi ni Mali ya umma. Ikimaanisha mimi na wewe na yule, lakini usimamizi amepewa Rais. Hivyo haki ya kumiliki na kutumia kisheria iko sawa kwa wote, lakini kwa kufuata taratibu zilizowekwa.
 
Kwa mujibu wa Sheria, Hakuna Ardhi iliyokaa bure tu, Ardhi ni mali ya umma na msimamizi mkuu ni Rais, wewe unakuwa umepewa tu hati ya kuimiliki kwa miaka kadhaa lakini lazima uendelee kulipa kodi kwa msimamizi mkuu (Rais)
Hiyo sheria wakati wa Nyerere na Mwinyi ilikuwepo au ni mpya?
 
Hoja ya msingi hapa ni BURE! Bure kama hewa tunayovuta ambayo hulipii chochote. Kama kuipata ardhi ni kwa kununua maana yake ardhi ina thamani na inatakiwa kulipiwa kodi. Just my thinking.
 

Ardhi ni mali ya umma. Ila rais kapewa kama msimamizi.
 
Hiyo ardhi unayolipia umeipata wapi wakati ardhi yetu wote binadamu ya asili unajimilikishaje
Aliyewahi kuichukua ndio anahesabika ni mmiliki kisha yeye ataamua kummilikisha mtu mwingine kwa malipo fulani,hiyo ndio asili yake ilikoanzia.
Bila hivyo ingekuwa vurugu ingekuwa kiwanja kimoja wanajazana watu 100.
Na kumbuka si wamiliki wote wa ardhi walinunua kwa pesa,wengine waliwahi tu mapori wakajimilikisha
 
Hoja ya msingi hapa ni BURE! Bure kama hewa tunayovuta ambayo hulipii chochote. Kama kuipata ardhi ni kwa kununua maana yake ardhi ina thamani na inatakiwa kulipiwa kodi. Just my thinking.
Sio wamiliki wote wa ardhi walinunua,wewe unanunua ardhi kwa sababu umechelewa kuja kuitafuta kwa hiyo unampa fidia tu mtu aliyeiwahi na kuitunza kwa ajili yako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…