Kwanini huwa tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati ardhi tumeikuta ipo bure? Why?

Wewe ndio huelewi, tangu umezaliwa umeikuta Ardhi ni Mali ya serikali.

Usipoelewa vitu vidogo kama hivi basi repoti ya CAG ndio wala usiangaike hata kusoma.

Ukiona kitu chochote kina expire date ujuwe si chako cha milele.

Ardhi ni kama driving licence tu, mamlaka wakitaka Leseni yao wanaichukuwa.
 
Kinachokupa faida ni biashara iliyomo ndani ya jengo! Hivyo kodi inalipwa kwenye biashara husika!
Ardhi ni vazi sasa unalipiaje kodi vazi la lazima?
 
1.Kwa nini mfalme atoze kodi ya pango la ardhi wakati ardhi huyo mfalme ameikuta?
2. Mfalme ni binadamu au taasisi aliyoiunda ambayo imepewa ardhi na mungu kama ilivyo kwa wananchi wake, kwanini mfalme atoze kodi kwenye ardhi ambayo wote tumeipata bure?.
 
Ndo hapo sasa! Tumechezewa mno!
 
Kama ardhi ni Mali ya uma Kwa Nini mtu akikuuzia eneo labda Kwa milioni 5 serikali kama yenye dhamqna Inachukua 10% tu?maana yake serikali ni dalali sio mwenyewe.
 
Kama ardhi ni Mali ya uma Kwa Nini mtu akikuuzua eneo labda Kwa milioni 5 serikali kama yenye thamqna Inachukua 10% tu?maana yake serikali ni dakali sio mwenyewe.
Sijui kama somo limeeleweka!
Yaani Ardhi ni natural at existing! Swali; kwanini serikali itoze kodi kila mwaka?
 
Tanzania hakuna mtu anamiliki ardhi. Wote tumekodisha kwa serikali.
 
Sijui kama somo limeeleweka!
Yaani Ardhi ni natural at existing! Swali; kwanini serikali itoze kodi kila mwaka?
Swali limeeleweka ni kwamba serikali inalipisha udalali kwa manufaa Yao ili baadaye CAG awahoji.
 
Tanzania hakuna mtu anamiliki ardhi. Wote tumekodisha kwa serikali.
Ndio ni kwa mujibu wa hao wakusanya kodi ndio waliitunga hiyo sheria,lakini bado swali la mtoa mada litabaki palepale ni kwa nini iwe hivyo wakati ardhi yote iliumbwa na Mungu ili binadamu waitumie?
 
Reactions: Tsh
Mbona hewa hatuuziani lakini hakuna vurugu ushawahi kusikia sehemu watu 100 wanagombaniana kuvuta hewa basi Kama hewa kaumba Mungu hatugombaniani kila mtu ni yeye tu na ukubwa wa pua yake kwanini hio ardhi kuwe na kuuziana na umiliki

Hili la kununua mbona huja hoji unahoji la kodi
 
Ni kwa sababu unapotumia ardhi unamnyima mwingine fursa ya kuitumia hiyo ardhi.

Usingeweka wewe nyumba juu ya hiyo ardhi ningeweka mimi
 
Tanzania hakuna mtu anamiliki ardhi. Wote tumekodisha kwa serikali.
Kwa nini tukodishwe na Serikali wakati Ardhi tumeikuta na Kama ilivyo hewa ndio urithi wa mwanadamu?
Kama tunakiri kuwa wakoloni walitwaa ardhi zetu, wakagawa vipande na kuweka Serikali zao, zikajiendesha kwa kodi za dhulma kama hii, kwa nini Serekali yetu inaendeleza ukoloni ule ule kwa watu wake?
 
Ni kwa sababu unapotumia ardhi unamnyima mwingine fursa ya kuitumia hiyo ardhi.

Usingeweka wewe nyumba juu ya hiyo ardhi ningeweka mimi
Kwani hewa unapovuta wewe, mwingine anakosaje?

Kwanini umuwaze mtu mwingine asiyeishi hapo badala ya kuwaza hiyo ardhi pia imenufaisha wanayoitumia!

Haya unapochukua kodi ya ardhi huyo mwingine atapata ardhi ya kufidiwa?
 
Kwa nini wadhibiti matumizi ya ardhi wakati iliumbwa ili tuitumie kwa kujinafasi?Maana dunia ndio hii hii moja hatuna dunia nyingine ya kwenda
Kudhibiti nilikuwa na maana ya kusimamia kwa ajili ya manufaa ya wote.
 
... wewe sasa una-diverge; hoja hapa ni sahihi kulipa kodi ya ardhi? Kwamba kuna misuse ya kodi hiyo ni topic nyingine kabisa! Let's be focused vinginevyo mjadala huu utakuwa hauna mwelekeo unaoeleweka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…