Kwanini huwa tunalipia kodi ya pango la ardhi wakati ardhi tumeikuta ipo bure? Why?

Watu sijui kama wanaelewa haki ya lazima na wajibu wa lazima!

Kuna vitu ukizaliwa tu tayali unahaki ya kuvitumia bure ikiwemo ardhi na hewa!
Mengine ya kuumba ni wajibu ambayo tunalipishwa kodi kwayo!
Ardhi ni bure, kwann niilipie kodi?
... hewa haina mmiliki na kuitumia wewe popote ulipo haimnyimi mwingine fursa ya kuitumia.

Kinyume chake, ardhi ukishamiliki kipande ina-exclude wengine wote fursa ya kutumia the same kipande. Hiyo ndio tofauti ya ardhi na hewa.
 
... sio kweli kwamba thamani ya ardhi ni majengo yaliyopo juu yake tu! Kile kitendo cha kui-own hata kama hujaweka chochote juu yake ni faida fulani kwako. Kama unaona haina faida iachie.
 
Hewa haionekani kwa macho ndugu,laiti hewa ingekuwa ina umbo maalumu,ina rangi na inakamatila wababe wangekuwa wanaiwahi na kuiweka ndani kwao
 
Umetafakari vyema, hata mimi pia niliwahi kuwaza hivyo hivyo kwann tulipie kodi ya ardhi? Nadhani hata kama serikali inawajibu wa kukusanya kodi katika kila nyanja basi kodi ya ardhi ingeondolewa kwa wale wanaoitumia kwa ajili ya makazi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hewa haionekani kwa macho ndugu,laiti hewa ingekuwa ina umbo maalumu,ina rangi na inakamatila wababe wangekuwa wanaiwahi na kuiweka ndani kwao
Na kwasababu hio pia usiweke hewa na ardhi kwenye kundi moja kisa zimeumbwa na Mungu ni asili Kama ulivyokuwa unasema..... Ardhi ni kitu Tangible kina shikika, inakalika, inaonekana, ina milikika na kutathminika lazima iwe tofauti na kitu Kama hewa hivyo usisashangae kukunulika na kulipiwa kodi
 
NA kwanini tunainunua wakati tumeikuta bure?
Wakati vitu vingi thamani ina-depreciate, ardhi always inaongezeka thamani. Ukijua maana ya kauli hiyo ambayo ni sahihi huwezi kutumia neno BURE kwa ardhi.
 
Wakati vitu vingi thamani ina-depreciate, ardhi always inaongezeka thamani. Ukijua maana ya kauli hiyo ambayo ni sahihi huwezi kutumia neno BURE kwa ardhi.
concept ni Nani ana mamlaka ya kuiuza ardhi tuliyoikuta, anayeuza aliitengeneza? Kama unaweza kununua kitu kilichoumbwa bure basi kilipie na kodi
 
concept ni Nani ana mamlaka ya kuiuza ardhi tuliyoikuta, anayeuza aliitengeneza? Kama unaweza kununua kitu kilichoumbwa bure basi kilipie na kodi
... kama concept ndio hiyo basi everywhere pawe free for everybody which is not the case kama baadhi wanavyojaribu kuilinganisha ardhi na hewa.

Kitu kikishakuwa na ownership ambayo inamnyima fursa mwingine kuki-own; lazima kilipiwe kodi.
 
Haya wataitoa kodi ya pango, makodi mengine je!!!! Hii ni dhulma ya wazi kabisa, aise ni wachache sana wataingia peponi

Duh kama ardhi ingekuwa haina kodi, saivi tusingerithi chochote , manake kila mtu angekuwa ameshajikatia zake kilomita za mraba 10,000 akajimilikisha , yaani kusingekuwa na ardhi yoyote iko tupu.
 
Duh kama ardhi ingekuwa haina kodi, saivi tusingerithi chochote , manake kila mtu angekuwa ameshajikatia zake kilomita za mraba 10,000 akajimilikisha , yaani kusingekuwa na ardhi yoyote iko tupu.
Point! Kodi inasaidia pia kupunguza walafi wa ardhi.
 
Kwa hiyo uelewa wako ni kwamba ardhi haina thamani hivyo ni ya buree!?
 
Ushuru wa magari n.k

Kodi za kipumbafu zisizo na maana mpaka stand za mabasi tunalipishwa watembea kwa miguu, magari n.k

Kodi za mapango, viwanda na manyumba dah watatumaliza aise
 
Duh kama ardhi ingekuwa haina kodi, saivi tusingerithi chochote , manake kila mtu angekuwa ameshajikatia zake kilomita za mraba 10,000 akajimilikisha , yaani kusingekuwa na ardhi yoyote iko tupu.

Uko sahihi kabisa mkuu. Kenya na Zimbabwe ni mifano halisi. Mfano Kenya, akina Kenyatta na wazungu wanamiliki wilaya kadhaa.
 
Ngoja tusubiri ufafanuzi kutoka kwa wasomi
Ardhi ni Mali ya umma, na Rais ndo amekabidhiwa kama msimamizi thus wote tumekodishiwa kutumia tena kwa muda maalum. Ndo mana kuna hati za miaka 33, 99 ndo mana tunalipa kodi. Ukipata muda pitia sheria ya, Ardhi ya mwaka 1999 na maboresho yake.
 
... wewe sasa una-diverge; hoja hapa ni sahihi kulipa kodi ya ardhi? Kwamba kuna misuse ya kodi hiyo ni topic nyingine kabisa! Let's be focused vinginevyo mjadala huu utakuwa hauna mwelekeo unaoeleweka.
Ana changanya! Hakuna anaepinga kodi! Tatizo unachukua kodi kwenye nini!
Mfano kodi ya mifugo, kodi ya ardhi, kodi ya jengo zote hizi hazina tija kabisa ni wizi!

Already existing on its nature! Kwanini uombe kodi!
Zamani kulikuwa na kodi ya kichwa! Vyote hivi ilikuwa ni unyama wa hali ya juuu! VIFUTWE VYOTE
 
Mfumo wa dunia wa Kiutawala, wanachuma mpk kwenye kazi ya Uumbaji wa Mungu.
Sheria za kidunia, Ardhi ni mali ya Serikali pamoja na vyote vilivyopo chini na juu yake isipokuwa bhangi
Quid plantue solo solo cediit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…