MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 14,588
- 32,361
Mama ndo afisa mtendaji mkuu wa kila siku kwenye nyumba. Asipokuwa imara familia itayumba. Ndugu wa mume huwa kiukweli hatuwezi vumilia mapungufu ya mke wa ndugu yetu. Pia kwa sababu hatuna uoga wowote kwa ndugu yetu hali inakuwa mbaya kwa mama mwenye nyumba. Mke lazima apaniki kwasababu hata akisema akatae upuuzi wa baadhi ya ndugu lazima lawama zimrudie kwamba hapendi ndugu wa mume.
Kwanini ndugu wa mke wanadumu? Kwanza wanatambua wapo pale kwa hisani ya mke kwahiyo kumheshimu ni lazima. Pili lazima wawe na tahadhari kubwa sana na mume vinginevyo wanaweza sababisha matatizo kwa ndugu yao ambaye ni mama mwenye nyumba. Kwahiyo kwa hizo hali wanajikuta hata kwa mume wa ndugu yao wanakubalika.
Mimi nadhani wanaume tuwasaidie ndugu zetu wakiwa makwao sio kuja kuishi nao. Mke ni lifetime partner kwahiyo usijaribu avurugwe na chochote kile. Kwa ustawi wa familia yako lazima Mke wako kwanza ndugu baadae. Yeyote atakayeshindwa kuelewana na mkeo aondoshwe tu maana hakuna namna.