Kwanini siku hizi wanandoa wengi hawapendi kuvaa pete za ndoa?

daah kazi tunayo
 
Sijawahi kuvaa, za nini kwanza?
Kuna siku nilikuwa nimepiga kinoma, nikaiuza ilikuwa ya gold. Nimerudi homa naulizwa pete iko wapi, nikamuambia nimeuza.. paliwaka.. kwakua na miw mzima wa akili, kawakaa sanaaa.. nikaona hizi fujo, nikabeba begi nikasepa nikaenda kulala hotel, asubuhi nakuta na missed call zaidi ya 50 🤣🤣🤣🤣 hakurudia tena kuniuliza mambo ya pete
 
Misijawahi kuivua pete ya ndoa, na ninaamini kuvaa pete kwangu ni agano kati ya mimi na mke wangu mpenzi.
Pia kuvaa pete ya ndoa ni utambulisho kwa jamii inayo kuzunguka, ingawa pete haimzuii mwenye roho ya usaliti kufanya yake.
 
Gazeti loote hujaelewa pointi yangu. Kuna wengine wanaishi kindoa kabisa bila wenzi wao kufahamu wana ndoa halali eneo jingine. Unakuta binti anaishi na mwanaume ana kuja kufahamu ana ndoa pale jamaa anapofariki au linapotokea fumanizi
 
Hahaha, binafsi sioni umuhimu wake. Sikuwahi kuzivaa.
 
Sasa mtu km ana saliti na kutoka nje ya mkewe au mumewe kwann anavaa Pete? Si ni ubatilii tyuuh.

Bora hata wasivae tyuuh.
 
Hahaha, binafsi sioni umuhimu wake. Sikuwahi kuzivaa.
Kiroho ( inafaida ) yanakuja mambo ya imani tena. ila sio lazima.. na hadi pia muwe mumevalishana kiimani sasa sie tunavaa kifasheni.. Yangu niliinywa safi na sina mpango wa kuja kuvaa tenaa.. hata wife sijuagi nae kama anavaaa 😅😅
 
Sababu mbalimbali ni zipi!?

Kwanza me sikuwahi ona wazee wangu hata mababu zangu na majirani wakiwa wamevaa pete za ndoa. Hiyo siku hizi reference yako ni lini!?

Me naona siku hizi ndo watu wanazivaa na huwa nashangaa wanawezaje kuzivaa...
 
Huu mtihani kwanza haujawahi kutungwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…