Kwanini siku hizi wanandoa wengi hawapendi kuvaa pete za ndoa?

Uzinzi tu, pete ni kielelezo kua una mahausiano. Na si rahisi mtu kukufata kwa lengo la kukutaka kimahusiano ikiwa kaona una pete kidoleni.

Hata mwanaume kutongoza akiwa na pete kidoleni lazima mtongozwaji kama ana akili timamu atajihoji sana na ni rahisi kuchomoa.

Sasa kwakua wengi uzinzi umewatawala basi huzificha hizo pete au lah hawazivai kabisa ili watongozane kwa uhuru.

Huonagi watu wakifumaniwa au mambo kuharibika huwa wanasema alikua hajui kama ni mume/mke wa mtu, sababu ya kwanza ni kua mchepukaji havai pete kuepuka maswali.
 
Hizo mbona huwa zinavuliwa na kufichwa mifukoni au pochi.
 
Sijasoma unachouliza ila jibu ni USALITI
Hakuna usaliti wowote, Mimi zangu nauzaga kwa sonara nikiwa na pesa ya kuchezea ndio nanunuwa nyingine.

Nikikwama cha kwanza ni Pete na ndio maana nanunuwaga ya pesa ndefu, nikienda kwa sonara sikosi laki nane namaliza shida zangu bila kumnyenyekea mtu anikopeshe pesa.
 
Wewe unaishi dunia ya peke yako, waume za watu ndio wanapendwa na wadada wa kisasa kwa imani wanajuwa care na wana busara.

Na wake za watu ndio wanawindwa kwa imani kwamba hawana gharama.

Pete haina issue yoyote kwa dunia ya leo zaidi ya urembo kama kuvaa cheni na asset.
 
Lakini kuna wengine wanaoana wakiwa wembamba,utamu wa ndoa unafanya wananenepeana na vidole vinakuwa vinene kiasi kwamba pete inakuwa inabana,wanavua wanaweka kabatini.kwakuwa hakuna umuhimu kuingia gharama kuchongesha nyingine.

Jambo lingine ndoa ngumu sana,unakuta inakupiga kama ngoma hadi unajuta,sasa hamu ya kuvaa pete itatoka wapi?.
 
Mwamba huyu hapaaπŸ˜…πŸ˜…
 
Ndoa ipoo moyoni...Kama mtu msaliti ni msalitii tu..halafu hizo Pete watu hata hawaogopi now days
 
Wengine kazi wanazofanya haziwaruhusu kuingia na pete sasa ile vaa vua inakera.
Wengine ni mapenzi yameshakufa hata kuvaa pete unaiona ni nzito kama kitoto ndoo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…