Siyo siri, Tanzania taasisi za kidini takriban zote, kwenye mikoa na wilaya zote zinahodhi maeneo makubwa ya ardhi ambayo hayatumiki kabisa au utakuta kwenye maeneo yao makubwa wanayohodhi kinejengwa kijumba kimoja au viwili vya kuzuga tu.
Wakati huohuo tunasikia mara kwa mara migogoro ya majeshi yetu na raia kuhusu ardhi.
Kwanini serikali isizirudishe hizo ardhi na kuwapa raia?
. Maeneo ya mashambani wapewe wenye kuhitaji kulima japo eka mbili mbili. Wawekewe miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji.
Maeneo ya maporini wapewe wafugaji waanze kufundishwa kupanda majani bora ya mifugo kama alfalfa na mengineyo, nao wawekewe miundombinu ya kilimo cha umwaguliaji. (irrigation). Wakafuge huko badala ya kuwa wahamahamaji, kurandaranda Tanzania nzima wskitafuta majani ya mifugo yao.
Maeneo ys kuishi watu wapewe raia wajenge.
Hii utaendana vizuri na mpango wa mama Samia wa BBT.
Nawakilisha.
Faizafoxy, nilikuwa sijui kama una akili ndogo namna hii. hapo unazuga tu. mimi sio mkatoliki, ila nikusaidie tu kufunguka, nia yako ni kusema kwanini wakatoliki wanahodhi maeneo makubwa namna hii?
jibu ni kwamba, Wakatoliki sio watu wa uswahilini wanaojenga nyumba za ibada katikati ya waswahili. wao huchagua maeneo ya pembezoni kabisa ya mji, mapadre na mabruda/mabrother na watawa wote hupendelea kujenga mission sehemu za pembezoni kusiko na watu, pawe pametuliaaa ili wapate muda mzuri kusoma Neno la Mungu na kutafakari. wakishajenga mission, hujenga pia huduma za kijamii ambazo dini zote hutumia. shida inakuja pale watu huwa wanawafuata, wananchi ndio siku zote huwafuata hawa jamaa kwenye maeneo yao. hapo kosa lao ni nini? maeneo kweli wanayo makubwa ila ukiuliza utasikia waliyapata miaka 30 au 40 iliyopita wakati dingi yako faiza alikuwa anacheza kigodoro huko hana hata mpango kutafuta ardhi.
lengo kubwa wao huwa ni kuwa na eneo kubwa la kujenga shule, hospitali na vyuo. ni huduma 100% kwasababu wao hawahodhi mali, hawana familia ya kutunza, hawana watoto mke wale mume, chochote wanachofanya hufanya kwa faida ya kanisa. hivyo ukikuta wana maeneo makubwa wapongeze kwasababu wamekuwa nayo miaka yote hiyo wakiyatunza.
pia, Tanzania hii ina maeneo makubwa mno yapo bure tu, wakatoliki wataenda huko na miaka ijayo watoto wenu watakuja kulalamika kwamba kwanini wakatoliki wana maeneo makubwa namna hii. nasema umelenga wakatoliki kwasababu hakuna dhehebu lingine lolote lenye maeneo kama hili. walokole hawanaga maeneo, walutheran na waanglican au nisema waprotestants wote hawanaga desturi ya maeneo. tukija upande wenu nyie kina faizafoxy ndio sio utamaduni wenu kabisa, iwe wa kumiliki maeneo, kujenga shule, hospital au vyuo. mnasubiri kupewa kama chuo cha morogoro.