Kwanini tukarabati kivuko kwa Tsh. bil 7.5 wakati kipya ni bil 8.5?

Magufuri unayemzungumzia ndio huyu huyu alienunua ndege na vivuko cash??

akanunua na kivuko kile ambacho hakitembei watu walivyo hoji akawapatia JWTZ ili watu waache kuulizia?

au unamzungumzia Magufuri yupi? Period
Kabisa. He was not patriotic leader, wasn't he?
 
Kama kivuko kilikuwa Beyond Economic Repair kingekatwa katwa kisha kingeuzwa kama chuma chakavu (siso) tu
 
Na mimi niliposikia 7.5B nikajua tumepigwa tena. Sitaki wazo la viongozi wakuu katika sakata hili kuwa hawana uchungu na mali za Wabara liingie kichwani mwangu. Hivi Songoro Marine hana uwezo ku kukarabati hiyo feri kweli. Kama kweli ilijengwa kwa 8 B leo tena unatoa kiasi kama hicho kukarabati TEMESA na wote mliotia sahihi mna la kujibu kwa Mungu. Upinzani msikae kimya na kwa hili, maana ni kama hampo hapa Tanzania. Zito, Lisu, nk mko wapi?
 
Waulizwe Wizara ya Ujenzi na kama ujuavyo Temesa ni wezi na wapigahi balaa, gharama ya matengenezo ya gari ya serikali Huwa kubwa mara mbili ya gereji za mtaani.

Swali kama Hilo Wabunge wakambane Mbarawa
 
Bahati mbaya sana, Unakuta Hizi Pesa, watu wa TAKUKURU wanafungu lao, Usalama Wana lao, Vyombo vyetu vya Ulinzi ma Usalama nao wa lao, Viongozi wa Dini Wana lao, Wapinzani njaaz Wana lao , Kiongozi Mkuu naye ana lake '.
Usisahau Mstaafu asiyestaafu naye yupo kutoa uzoefu
 
Tukisema nchi haina Raisi. mnakunja sura acha watu wajipigie bila huruma
 
Bunge limekua kijiwe Cha kudiskas uganga na uchawi na ushirikina.
Hakika Mwigulu alisema kweli kwamba kwenye ule mjengo waongelee uganga wa kienyeji tu.
Vitu Kama hivi kina Babu Tale hawawezi kuvihoji. These issues are too abstract for the likes of kibajaji.
 
Wasalaam member wote wa JF!

Kwanza nianzw kuwapa pole wote mliopata na mshangao wa gharama za ukarabati wa ferry yetu wa Mv Magogoni kuwa ni Tsh Billion 7.5 huku gharama za ujenzi wa ferry ile ikiwa mpya mwaka 2009 ulikuwa ni Tsh Billion 8.

Niende kwenye hoja yangu juu ya harufu ya rushwa ninayoiona kwenye issue iliyoteka mirandao ya jamii katika siku ya leo juu ya gharama za ukarabati wa Mv Magogoni.

Gazeti la The Citizens November 09,2022 liliandika habari juu ya PPRA kubatilisha tender iliyokampa ushindi kampuni ya African Marine and General Engineering Company Ltd. Huku mlalamikaji akiwa Kampuni ya Songoro Marine ambaye alifungua shauri hilo PPRA kwa kuilalamikia TEMESA kwa kuto mtendea haki katika ushindani na PPRA alikubaliana na Songoro Marine na hatimae kubatilisha ushindi wa kampuni ya African Marine and General Engineering Company Ltd. Na kuagiza mchakato uanze tena upya.

Ajabu mda uliotolewa maamuzi na PPRA mpaka kufikia leo ni kweli Temesa ilishatangaza tender tena na kupata mshindi yuleyule African Marine and General Engineering Company Ltd. Na kwa gharama zilezile ambazo walishindwa mwanzo?


Ni kweli Songoro Marine ambae alijenga hiki kivuko kwa Gharama ya Tsh Bilion 8 leo hana sifa ya kukifanyia ukarabati?

PPAA nullifies Sh7.5 billion Mv Magogoni ferry tender
 
Ngoja wahuni waje,
Watasingizia inflation[emoji1787]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…