Kwanini tukarabati kivuko kwa Tsh. bil 7.5 wakati kipya ni bil 8.5?

Ndani ya nchi zipo kampuni zingefanikisha ukarabati kwa bei ya kawaida.

Huu ni upigaji tu.

View attachment 2519624
Wakati wa Nyerere nchi hii ilikuwa ya wakulima na wafanyakazi. Wakati wa Mwinyi, Mkapa na Kikwete ikawa ya wafanyavyo na wafanyakazi. Wakati wa Magufuli na sasa Samia Suluhu nchi imekuwa ya viongozi. Wao ndio wanaopanga na kuamua kufanya kila kitu. Wananchi tumebakiwa na mamlaka ya kwenye maandishi tu, ukweli viongozi wanafanya kila kitu wananchi wamebaki kushiriki kutekeleza maamuzi yao tu bila kuhoji: kama kulipa kodi na tozo, kuhamishwa kwenye maeneo yao ya asili, nk.
 
Sijui ni ukarabati gani huo, hata kama ni kubadilisha engine zote mbili na kuweka mpya haitakiwi izidi billion moja!
 
Huyu Moderator alieunganisha thread yangu na hii atakuwa mgonjwa kabisa! Na hana sifa za kuwa hapo kama anaona Content zinafanana.
Wanakosea Sana,
Uzi wako na huu Zina maudhui tofauti KABISA, ule wa kwako ulichambua kwa kina
 
KUNA barabara za mtaani kila siku zinapitishwa greda wakati zinaweza kujengwa lami vizuri tuuu unadhani kwa nini??? URASIMUUU... yani yote ni upigajiiiiii
 
Daah hata wangepeleka SA wanunue Engine zote na vitu vingine kwenye kampuni ya Atlas Marine isingefika bei hiyo maana gharama kubwa ni ile dry Dock pia sijajua sasa hivi wanachaji bei gani kwa siku...ila tunaibiwa sana aisee daah...na hawana huruma kabisa..
 
Weka quotations za kipya from various sources, uko sahihi kabisa. Weka ushahidi...
 
Halafu anajidai kutisha watu wasiquery hizo tenda kina januari na wenzake wanatoa eti kazi itachelewa. Bora kuchelewa kuliko wajanja kula mabilioni ya umma. Anaweka watu hawaaminiki na wananchi halafu anafikiri wananchi wataamini matumizi ya serikali?
 
Binadamu ni mtu mmoja mjinga sana, hawajui hizo hera wanazowaibiya wanaichi wao wataenda kuulizwa kwa Mwenyezi Mungu,pili siku ya kufa hawatazikwa na chochote kile,wataenda kama walivyozaliwa,ukilijua hilo utamuogopa Mungu wako
 
Waulizwe Wizara ya Ujenzi na kama ujuavyo Temesa ni wezi na wapigahi balaa, gharama ya matengenezo ya gari ya serikali Huwa kubwa mara mbili ya gereji za mtaani.

Swali kama Hilo Wabunge wakambane Mbarawa
Kina babu tale bungeni hawana msaada wowote ule, wanajiita madoctar
 
L
Mwisho wa siku mpinga rushwa si mmemuita muuaji?

Mpinga rushwa ndie leo amekuwa mwizi!

Mtamkumbuka sana,wacha vijana wa Mama wale urefu wa kamba zao!
Lakini si ndiyo huyo aliyeliharibu bunge,ingalau leo hii wabunge wa upinzani wangepinga bungeni
 
Achana n mambo hayo fanya yako,hakuna jipya TZ
Kuna kiongozi mmoja mwasisi wa taifa hili aliwahi nukuliwa akisema kama hamtaki kujihusisha kwenye siasa za nchi hii, kama hamtaki kujihusisha na maendeleo ya nchi hii basi huko mbele mambo yakiharibika msijekulaumu kwa sababu hakuna mtu atakayewafanyia hayo bali ni nyie wenyewe. Sasa mwenzako ameleta masikitiko yake kwa jambo la msingi kabisa wewe kwa ujinga au kutofahamu unaona jambo hilo halina maana, ila cha ajabu ikitokea kukawa hakuna kivuko hapo Kigamboni ndiyo utakuwa wa kwanza kulialia.
 
Ndani ya nchi zipo kampuni zingefanikisha ukarabati kwa bei ya kawaida.

Huu ni upigaji tu.

View attachment 2519624
Kwako waziri Makame. Ukifanya upigaji mkubwa Kama huu, fanya bila kutangaza, maana ukitangaza wengi wetu tunajaa nyongo isiyo ya lazima.
Hivi ndugu mawaziri kwa upigaji wa kufuru mnaofanya, mnategemea mtaishi miaka mingapi. Kumbukeni hata hapa Dar watoto wetu hawana madawati na wanakaa Mia mbili kwenye chumba Cha darasa. Najua hakuna mbunge au waziri anayelijua hili.
Wachaga wanasema, ukitafuna nyama usifungue mdomo.
 
Nikumbushe tu kwamba 2020 tulipokwa haki yetu ya kuchagua viongozi tunaowapenda. Sio upinzani tu hata ndani ya CCM majina ya watu wenye akili yalikatwa. Mfano mzuri Ni Korogwe vijijini. Mahindi wa kwanza na wa pili walikatwa majini. Kachukuliwa mbumbumbu hata huko bungeni haendi.
 
Umeongea vema kabisa na mimi nayakumbuka hayo yote uliyosema. Hoja yangu ni kwamba hatupaswi kuchoka kuyasemea na kuyapigania mambo haya pamoja na ukweli kwamba kuna vipingamizi na changamoto nyingi sana kama hizo ulizosema. Kuna siku moja kule bungeni kwenye mijadala ya kwenye kamati wakabaki Lissu na Mnyika ndiyo wakawa wanakomaa ili muswaada ulioko mezani urekebishwe kwa maslahi mapana ya walio wengi, wabunge wengine naona wakawa wame give-up maana bunge lilikuwa limeenda mpaka usiku siku hiyo. Lissu akawa anamwambia Mnyika ndugu yangu Mnyika pamoja na kuwa tumeachiwa sisi wawili tuendelee usikate tamaa, tuendelee kupambana mpaka kieleweke hahaaaaa yaani mpaka Spika Anna Makinda akacheka. So ninachosema tusichoke tuendelee maana tukiacha kusema ndiyo kabisaaa bucha limeachiwa kwa.......hahaaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…