Kwanini tukarabati kivuko kwa Tsh. bil 7.5 wakati kipya ni bil 8.5?

Labda Songoro hawana utaalamu wa kukarabati MV Magogoni ndio maana amepewa Mkandarasi wa Nje ya Nchi
 
Kwani songiro yeye nani .
Mbna makampuni saiv kibao tu kila deal yeye na sisi tutatusua vipi.
Kwa dau Hilo inasikitisha kweli ila mmamshabikia sana huyu songiro utazani yeye ndo anazitengezaga fresh.
Sio lazima Songoro angepewa Kampuni yoyote ya kitanzania yenye uwezo
 
Rais alisharuhusu mtu kupewa tenda bila kufuata mchakato hakuna tatizo hapo.

Tatizo lipo kwako usiye na kumbukumbu.
 
Tupate jibu hili kwanza,ni kwanini kipindi cha awamu ya tano tenda zote za kutengeneza/kukarabati vivuko na meli zilikuwa hasitangazwi na zote alikuwa akizifanya SONGORO MARINE tu?!!tukipata jibu hili kwanza ,itakuwa rahisi kujua huwa ni nini kinatokea.
 
Hapo ni sahihi kujiuliza na ni muhimu sana lakini kumbuka kosa halirekebishwi kwa kosa na ukumbuke hii nchi ya Watanzania na wala sio ya Jiwe.... hizo ni fedha tunazolipa kodi mimi na wewe
 
Hivi gari ulilolinunua 2011 kwa 20M ukiamua kulifufua kwa service nzito garage ya kishua haivuki 20M kwa usawa huu wa 2023?

Wakala wa majengo TBA,SUMA JKT wajiandae.

Mpaka miradi ya REA zabuni zitachukuliwa na Maltauro ya Nairobi.
 
Hii mirangi ya Kijani nayo daah
 
We jamaa uko timamu kweli? Kivuko kile hakiwezi kuchukua watu 2000 at per??
We weka hapa thamani ya kivuko kipya chenye capacity kama ya Magogoni.

Watanzania mnapenda kulaumu na kuonekana nyie ndio wenye uelewa kuliko wataalam wenyewe.
Watu elfu 2 inabebea wap shekhe?
 
Wametoa sababu hii hapa na naona ni logical

 
Hapa hamna kutengeneza Kwa kiasi hicho, kinacho fanyika ni pitio la kuchukulia pesa,na hili nahis ni Dili la wakubwa kabisa maana Kwa kelele hizi lingekuwa Dili la wahuni tu wakubwa wangekuwa wameisha Toka na kuungana na wananchi kukemea pia.Wanajuana hao labda wanatafuta pesa za uchaguzi.
 
Hapo ni sahihi kujiuliza na ni muhimu sana lakini kumbuka kosa halirekebishwi kwa kosa na ukumbuke hii nchi ya Watanzania na wala sio ya Jiwe.... hizo ni fedha tunazolipa kodi mimi na wewe
Ni sawa,lakini haya mambo kama mna katiba nzuri ambayo inalifanya bunge kuweza kuisimamia serikali ipasavyo yasingekuwepo.Shida inaanzia pale jitu zima tena lisomi linasema KATIBA HAIWEZI KUKULETEA CHAKULA MEZANI!!!Kuna mambo yanafanyika Afrika hadi mtu unajiuliza hivi hiki kiumbe (Mwafrika mweusi)kilitoka wapi?!!
 
Unalia mapema mno, lakini ni haki yako.

WaTanzania tutalia sana chini ya huyu mwanamke. Bado sana, na mambo ndiyo yanaanza hivyo.

Lakini tusiwe wanyonge kuliko kiasi. Akheri wewe umeona hilo na kuliweka kwenye kumbukumbu, hii ni kazi tunayoweza kuifanya pamoja na unyonge wetu. Hakuna anayeweza kuzuia tusiweke kumbukumbu kwenye haya mauchafu yote yanayoinajisi nchi yetu.

Historia itawahukumu.
 
Rais alisharuhusu mtu kupewa tenda bila kufuata mchakato hakuna tatizo hapo.

Tatizo lipo kwako usiye na kumbukumbu.
"...hakuna tatizo", kwa "mtu kupewa tenda bila kufuata mchakato", kwa vile tu "Rais alisharuhusu".

Hili unaliweka hivi, pamoja na kwamba linakuumiza, lakini najuwa katika wakati uliopita maneno hayo hayo ungeyasema bila ya maumivu yoyote.

Mimi "kumbukumbu" ya huyo aliyeruhusu ninayo, na ninalaani siku moja uhujumu huu uwakwame kooni hao wanaoufanya.
 
CCM sio chama cha wakulima na wafanyakazi, ni chama cha mafisadi, wezi na majambazi wa Uchumi wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…