Kwanini Wakristo hawavui viatu wakiingia Kanisani? Mbona Musa aliambiwa avue viatu?

Kwanini Wakristo hawavui viatu wakiingia Kanisani? Mbona Musa aliambiwa avue viatu?

Ila mjadala unavyoelekea, msingi wake ni hiyo "mada nyingine".

Ukiangalia, hakuna anayeanzisha uzi wa kufundisha ila kutuhumu upande mwingine, ni kana kwamba mna-assume wote ni maulamaa, hivyo mko kujadili shortcomings za pande zote!

Ni sawa, lakini si muanze na jambo moja, ligongeni, kubalianeni hata kama mtakubaliana kutokukubaliana, kisha muhamie jambo la pili?

Leo mnazungumzia "wakristo kutovua viatu kanisani", mimi nimeshapata mambo kadhaa hapa lakini sijapata muafaka wake bado;
  • Hakuna sehemu inadhibitisha kwa mujibu wa dini, mila na desturi za kiyahudi, kuwa walikuwa wanavua viatu.
  • Mungu, hakumtokea Musa mara moja tu, ila ni mara moja tu ndio Musa aliambiwa avue viatu.
  • Sinagogi, Msikiti, Hekalu na Kanisa, ni majina kwa mujibu wa jamii, sio imani!
  • Kuna hoja kuwa kumbe sio kosa kuingia na viatu msikitini, kwamba hata Mfalme/prince wa Arabuni amewahi onekana akiswali na viatu msikitini.
  • Kwamba, kusujudu ni lazima wakati wa kuswali kwa imani ya kiislamu.
  • Nimeona tafsiri ya najisi, na jinsi gani inakinzana baina ya uelewa wa watu.
  • Nimeona hapa, kuwa Muhammad ndio muislamu wa kwanza kisha nimeona waliomtangulia wakisemwa kuwa waislamu.
  • Lakini imefika mbali hata kuzungumzwa kuhusu mabikra 72 hapa
  • Nimeona pia imetajwa suala la watu kupakatwa kwa mujibu wa biblia.
  • Nimeona hapa kuwa Adam na Yesu wote waliumbwa kwa udongo kwa mujibu wa Quran
  • Nimeona suala la kuwa Yesu pekee ndio atakayerudi siku ya kiama kupambana na Dajjal(sijui ni nani) kisha ikajibiwa kuwa wote tutarudi, akikusudia kuwa Muhammad naye atarudi ili kuja kuhukumiwa.

Mengi yamejumuishwa kwenye hii mada, na kama haitajikita kwa topic moja moja, mtaruka ruka huku na kule bila kufika muafaka na sisi wanafunzi tutabaki watupu!
Kwa upande wangu Musa alivua viatu ila wakiristo hawapaswi kuvua viatu kwakuwa Musa hakuwa mkiristo mengine ni maelezo kama kuna sehemu hujaelewa uliza nitakufahamisha
 
Mbona wengine wanaoga kabla ya kuingia kwenye majengo yao ya kuabudu lakini tumboni wamejaa mbolea?. Vipi wanapokuwa ndani wanakuwa bado wasafi?.
 
Naona ni jinsi gan Waislam hamuelewi hiki nitakachosema chini!.

Misingi ya Dini ni Miongozo ya namna ya kuishi , kusali na taratibu zake ambavyo zipo kwenye Vitabu.
Kitabu chenu ni Quran.

Kimeshushiwa kwa Mohamed akiwa na miaka 40.
Kabla ya hapo hakukuwa na Uislam kwaababu hakukuwa na Miongozo kama nilivyosema hapo juu.

Mohamed alikuwa mpagani.
Na Baba yake alikuwa Mpagani.
Na kabla yake hakukuwa na Uslam.

Hebu soma hii
Quran 42:52 -
Na namna hivi tumekufunulia Qur'ani kwa amri yetu. Ulikuwa hujui Kitabu ni nini, wala Imani. Lakini tumekifanya kuwa ni Nuru ambayo kwayo tunammwongoa tumtakaye katika waja wetu. Na hakika wewe unaongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka.
Uislam ulikuwepo ila watu/ummah wa Muhamad walikuwa hawaufuati walikuwa wanaabudu masanam na miungu watu Muhammad ni mjumbe wa Mungu alietumwa kwa umma wake kuwaambia waache hizo mila na kumuabudu Mungu mmoja kama alivyoambiwa, Daudi, Musa na Isa(Yesu) vile vile walikuwepo manabii wengine waliotumwa na Mungu katika kaum/umma/watu wao kama Yusuf, Yakuub/Yakobo na wengine wengi
 
Swali lako linaonyesha kana kwamba hujaelewa mantiki ya kwa nini jina la Musa limetajwa katika mada hii.

Sijamtaja Musa kwa sababu tunamfuata au tunataka kuiga kila alichofanya. La hasha. Nimemtaja Musa kwa sababu kuna watu wanaojaribu kuhalalisha utaratibu wa kuvua viatu kanisani kwa kutumia mfano wa Musa. Kwa maneno mengine, wao wanasema: “Mbona Musa alivua viatu aliposimama kwenye ardhi takatifu? Basi hata sisi tuvue.”

Kwa hiyo, nimetoa mfano wa Musa kwa lengo la kubatilisha hoja hiyo, si kwa lengo la kumfanya Musa kuwa kielelezo cha Ukristo. Musa hakuwa Mkristo, na hakuna mahali katika Agano Jipya ambapo Wakristo waliagizwa kuvua viatu kama utaratibu wa ibada. Yesu hakufundisha hilo. Mitume pia hawakulisisitiza hilo. Hivyo basi: kama sababu pekee ya kuvua viatu ni kwamba “Musa alivua,” basi sababu hiyo haina mashiko. Umenipata?
Nafikiri kuvua viatu wakati wa kuongea na mungu ni mfano bora wa kuigwa, watu walikuwa wanavaa mpaka magunia wanaposali,

Tunaposali tunapaswa kuonesha heshima na unyenyekevu zaidi mbele za mungu, tusisali tukiwa tume piga nne, au mikono mfukoni, na ikukubidi kwa hiari yako vua viatu, vua nguo za thamani vaa nguo za gharama ndogo kubwa kama wazee wazamani hili ni jambo la busara sio la kujadili.

Usisimame mbele za aliye mkuu na viatu au na vitu vyovyote vyenye thamani lakini fanya haya kwa hiari yako mwenyewe ukiwa na nia ya kujishusha mbele zake atakubariki zaidi na zaidi.

Nje ya hapo kama utaamua kusali na viatu ni wewe kama utaamua kusali umepiga nne ni wewe inategemea na moyo wako lakini kwasababu mungu ni mwelevu sana na atatenda apendavyo.
 
Mtume kabla ya kushushiwa wahyi alikuwa muislam by nature lakini asie na elimu wala uwelewa wa dini na mafundisho yake kama wewe tu wakati unazaliwa hukujua lolote kuhusu dini

Yesu alikuwa Myahudi ila wanafunzi wake wawe wakiristo? Wakati huo Uyahudi ni Dini na Ukiristo ni dini au hiyo ya Uyahudi sio Dini sahihi ni ukafiri ndio maana akawaambia wanafunzi wake wawe wakiristo? Nawaza tu

Tumia tu Logic ya kawaida.

Hakukuwa na Uislam kabla ya Quran.
Wote wanaoifuata Quran ndio Waislam.
Wote wanamfuata Mohamed ndio Waislam.

Sasa ukisema alikuwa Muislam by nature ina maana Hata Mchina anayezaliwa huko Maccau ni Muslam?.

Nini maana ya Kusilimu?.
Kwanini Mohamed amesema yeye ndio wa Kwanza Kusilimu?.

Kwanini watu wanasema Shahada ?
Bila shahada unaweza kuwa Muislam?.
Bila shaka ni Hapana.
Sasa manabii hao waliopita walisema Shahada?.
Bila shaka hapana.
Inakuwaje sasa wawe Waislam?

LOGIC tu ndogo inakuambia kuwa hawakuwa Waislam
 
Yesu alikuwa Myahudi ila wanafunzi wake wawe wakiristo?
Mkuu, mwalimu wako aliyekufundisha shule ya msingi, alikuwa na kusudi la wewe uwe mwalimu pia? Au ni lazima uwe mwalimu?

Najaribu kufikiri, Yesu alizaliwa na kukuwa kwenye misingi na imani ya walezi wake, alionesha uwezo mkubwa sana wa yale yaliyokuwa yakifundishwa na walimu wa dini(ile aliyokuzwa nayo). Hii si ni kawaida?
  • Waislamu wangapi wameuchagua uislamu tangu utotoni?
  • Madrasa si zipo na sisi tumekuwa tukiona jinsi bakora zikitumika kuwashikisha watoto imani!

Wakristo kadhalika, wengi wakua wakiishika imani toka kwa walezi wao.

Tofauti ni kuwa, utakapokuja kubadili au kutoka kwenye uislamu, uislamu unaamuru uuawe tofauti na ukristo.

Sasa, Yesu, alinolewa kwenye makuzi ya kijamii na kiimani iliyomzunguka, ya walezi wake.
  • Yesu akaendeleza yaliyo bora
  • Yesu akawafunza wasiyoyajua
  • Yesu akawaahidi eternal life
  • Yesu akawahakikishia kuwa, wakifuata mafunzo yake na kuzishika amri zake, basi watakuwa naye kwa baba baada ya muda wao kuisha hapa ulimwenguni.
  • Yesu akawajuza kuwa, yeye atakuwepo kuume kwa baba yake huko mbinguni
  • Yesu akawaambia, yeye na baba yake ni wamoja, na bila kupitia yeye, hakuna atakayefika kwa baba yake.
  • Akisema, yeye ndiye njia, kweli na uzima.
  • Akawafundisha jinsi mpya ya kubatiza, akisema watumie jina la baba, la mwana na la roho mtakatifu.
  • Aliwaelekeza yatakayotukia akiwa hai duniani, akiwa kuzimu na akishatoka kuzimu.
  • Akawaeleza atapoenda yeye na anayoweza kufanya akiwa huko kwaajili yao.

Mkuu, huyu mtu, hata kama ungekuwa wewe, utaacha kumfuata?
  • Utafuata maneno matupu?
  • Utafuata hadithi?
  • Utafuata mtu anayekiri hajui anaupeleka wapi umma wake?
  • Utamfuata mtu ambaye anakiri kuna mambo hayajui hata kama ameshushiwa yeye ili awaambie na kuwaelimisha umma wake?

Sasa, kama yeye hakuja na dini, ila alisema watu wafuate mafunzo yake, zaidi akasema yeye ndiye njia, huoni kuwa yeye ndiye dini kwa hao wanaomfuata?
  • Hakuna anayesema wala kulazimisha kuwa Musa alikuwa mkristo.
  • Hakuna anayesema kuwa Daudi, Adamu, Ibrahimu, Yakobo, Isaka n.k kuwa ni wakristo.

Ila wakristo ni wanaomfuata Kristo(Masihi), wangependa, wangeweza pia kujiita Wa-masihi.

Waislamu wanamfuata Muhammad,na kabla hakuna anayemfuata Muhammad na wahyi yake aliyoshushiwa yeye!

Hakuna ujanja ujanja hapo mkuu!
 
Tumia tu Logic ya kawaida.

Hakukuwa na Uislam kabla ya Quran.
Wote wanaoifuata Quran ndio Waislam.
Wote wanamfuata Mohamed ndio Waislam.

Sasa ukisema alikuwa Muislam by nature ina maana Hata Mchina anayezaliwa huko Maccau ni Muslam?.

Nini maana ya Kusilimu?.
Kwanini Mohamed amesema yeye ndio wa Kwanza Kusilimu?.

Kwanini watu wanasema Shahada ?
Bila shahada unaweza kuwa Muislam?.
Bila shaka ni Hapana.
Sasa manabii hao waliopita walisema Shahada?.
Bila shaka hapana.
Inakuwaje sasa wawe Waislam?

LOGIC tu ndogo inakuambia kuwa hawakuwa Waislam
Ni kweli kila mtu anaezaliwa duniniani ni muislam (amejisalimisha kwa Mungu) ndio maana muislam alizaliwa hahitaji shahada anakuwa automatic ni Muislam tofauti na mkiristo hata azaliwe na mkiristo lazima abatizwe
 
Kwanza jua kutofautisha taaluma na dini ni vitu viwili tofauti kabisa
 
Ni kweli kila mtu anaezaliwa duniniani ni muislam (amejisalimisha kwa Mungu) ndio maana muislam alizaliwa hahitaji shahada anakuwa automatic ni Muislam tofauti na mkiristo hata azaliwe na mkiristo lazima abatizwe
Hakuna uthibitisho wowote kuwa mtu akizaliwa tayari ni muislam, falsafa hii imekaa kinadharia isiyo na ushahidi vipi utajuaje kama umedanganywa ?
 
Jibu hoja yangu ya pili
Nadhan nilishajibu.
Kabla ya Yesu. Hakukuwa na Ukristo.

Ulikuwepo Uyahudi kama Dini.

Ila Yesu alikuja kuitengemaa torati.
Na ni Yeye ndio aliamuru Watu wafundishwe kwa kufuata yeye.

Kama alivyosema Ndalilo .
Kristo nina maana masihi.

Tumekuwa wakristo sababu tunafuata yale Masihi aliyoamuru kama maagizo.
 
kunatofauti kubwa kati ya kabila na imani
Huyo unae zungumza nae anachukulia dini na kablla na imani ni vitu tofauti lakini hata hivyo hajachunguza na kuvijua ni nini yeye yupo yupo tu na kile kidogo alicho ingiza kisha sasa anakuja kutafuta watu abishane nao. inasikitisha sana.
 
Tumia tu Logic ya kawaida.

Hakukuwa na Uislam kabla ya Quran.
Wote wanaoifuata Quran ndio Waislam.
Wote wanamfuata Mohamed ndio Waislam.

Sasa ukisema alikuwa Muislam by nature ina maana Hata Mchina anayezaliwa huko Maccau ni Muslam?.

Nini maana ya Kusilimu?.
Kwanini Mohamed amesema yeye ndio wa Kwanza Kusilimu?.

Kwanini watu wanasema Shahada ?
Bila shahada unaweza kuwa Muislam?.
Bila shaka ni Hapana.
Sasa manabii hao waliopita walisema Shahada?.
Bila shaka hapana.
Inakuwaje sasa wawe Waislam?

LOGIC tu ndogo inakuambia kuwa hawakuwa Waislam
Jibu hoja yangu ya pili hapo juu ili tuendelee
 
Nadhan nilishajibu.
Kabla ya Yesu. Hakukuwa na Ukristo.

Ulikuwepo Uyahudi kama Dini.

Ila Yesu alikuja kuitengemaa torati.
Na ni Yeye ndio aliamuru Watu wafundishwe kwa kufuata yeye.

Kama alivyosema Ndalilo .
Kristo nina maana masihi.

Tumekuwa wakristo sababu tunafuata yale Masihi aliyoamuru kama maagizo.
Nani kakwambia uyahudi ni dini ? kabla ya ujio wa ukristo ? kama utaki elimu kwanza ndio ujue utakuwa mbumbumbu, huwezi kujua kitu bila kukielewa ni nini.
 
Ni kweli kila mtu anaezaliwa duniniani ni muislam (amejisalimisha kwa Mungu) ndio maana muislam alizaliwa hahitaji shahada anakuwa automatic ni Muislam tofauti na mkiristo hata azaliwe na mkiristo lazima abatizwe

Kubatizwa ndio maagizo Yesu alisema.
Tunayafuata.

Muislam lazima aseme Shahada hata kama amezaliwa katika uislam.

Si ni moja ya nguzo zile tano.

Sasa mtu ambaye hajawah sema Shahada anakuwaje Muislam?.

Tutumie tu Logic hata kama tunayo logic kidogooo. Hiyo hiyo tutumie kujua hilo.
 
Back
Top Bottom