Hata kama angeikuta misikiti Yesu angeingia na kujumuika na waumini kwa lengo la kuwahubiria injiri:
Huko Sinagogini siku ya kwanza kuingia na kuhubiri walimfukuza na nusu wamjeruhi:
Luka 4:14
Yesu akarudi kwa nguvu za Roho, akenda Galilaya; habari zake zikaenea katika nchi zote za kandokando.
15 Naye alikuwa akifundisha katika masinagogi yao, akitukuzwa na watu wote.
16 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome.
17 Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa,
18 Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa,
19 Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa.
20 Akakifunga chuo, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.
21 Akaanza kuwaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu.
22 Wakamshuhudia wote, wakiyastaajabia maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake, wakasema, Huyu siye mwana wa Yusufu?
28 Wakajaa ghadhabu wote waliokuwa katika sinagogi walipoyasikia hayo.
29 Wakaondoka wakamtoa nje ya mji, wakampeleka mpaka ukingo wa kilima ambacho mji wao umejengwa juu yake, wapate kumtupa chini;
30 lakini yeye alipita katikati yao, akaenda zake.