Sijafanya research ya kuweza kuhalalisha majibu yangu.
Ila nitatoa mfano.
Kesho unatakiwa kuukata mti.
Unajihimu Alfajiri na vitendea kazi, unafika pale na kuanza kukata mti. Unajitoa kweli kweli, unatumia msumeno, unatumia shoka na unatumia panga.
Lakini muda wote huo ulikua hauahangaiki kukata shina, ulikua unakata mizizi na matawi.
Kufika jioni mti haujakatika.
Kesho unarudi tena, na kwenda na routine ile ile.
Kwa maoni yangu WaTz wengi wanaoonekana wanafanya kazi angalia kama kazi yao inashughulikia tatizo. Utakuta ni inalizunguka tatizo.
Angalia wanasiasa, timu za mpira, hata maofisini n.k. ni wachache wanaaddress tatizo.
Ninaamini ndiyo sababu tunaonekana tunafanya kazi ila mafanikio hayaji au yanakuja kiduchu