LATRA yatangaza ongezeko la nauli za Safari za Masafa Marefu na Mafupi kuanzia Desemba 8, 2023
Vichekesho hivi
Dom kwenda Dar nauli sh ngapi?
Na umbali wa Singida Dom ni ngapi?
🤣🤣🤣🤣
 
Magufuli rip baba tunakukumbuka sana kosa ulilofanya kutuachia huyu kiumbe anatunyosha tu nauli inaongezeka 10000 nzima kwa kazi gani waliofanya hao latra, kwa maisha gani facken kabisa kesho na mimi dukani naongeza bei alfu tano tano kila mtu apige anakoweza.
 
Yaani hajawahi kutokea Ndani ya miaka miwili nauli KUPANDA mara mbili

Samia is the worst president ever in our country's history

Nitamshangaa Sana akigombea Tena 2025. Sioni sababu ya msingi ya yeye kugombea. Labda Kama anapenda kuwa Rais kwa manufaa yake na familia yake. Lakini Kama ni nchi ameshindwa kazi tayari.
 
Mama yenu hafai kwa urais, amevuruga uchumi wa nchi na kuongeza ugumu wa maisha kwa raia wasio wezi

Tangu siku ile amekiri kwamba ilibidi wakope ili kulipa mshahara, niliacha kumfuatilia kabisa. Ninamuomba 2025 asigombee Kama kweli anatupenda watanzania. Lakini Kama hatupendi basi agombee na hiyo Time yake ya NEC wampe urais azidi kuharibu.
 
Hakika bado tuna safari ndefu. Aliyekaa na kutoa taarifa hii mpaka muda huu hapaswi kuwepo ofisini Hivi kutoka Dodoma hadi Dar ni umbali wa Kilometa 80? Dodoma hadi Morogoro kilometa 1,140!!? Pole sana watanzania na mimi nikiwemo. Chart tu ya Dodoma kwenda maeneo mengine imejaa madudu ya namna hii, vipi kuhusu maeneo mengine na yale ambayo hayako wazi kwa wananchi?

Sijui walikuwa wanaharaka ya kwenda wapi.
 
Wao badala ya kupunguza kiwango kikubwa cha kodi ambayo mafuta yana 26% kwa jumla yote wapo busy kuongeza bei ya nauli maana kwa kodi hizo bei zitaendelea kupanda tuu...
 
Back
Top Bottom