LATRA yatangaza ongezeko la nauli za Safari za Masafa Marefu na Mafupi kuanzia Desemba 8, 2023
Aisee yani ndani ya mwaka nauli inapanda marambili kweli na Rais yupo? Hivi kweli serikali imeshindwa kuthibiti kabisa mfumuko wa bei hasa ya mafuta? Kwanini hadi leo yale makodi ya taasisi zaidi ya kumi yapo? Kwani serikali na Rais wasilaumiwe? Hivi kweli kabisa una ruhusu kupanda kwa bei mfulululizo hivi?
Hivi ni lini nauli zilishawai kushuka? Rais hajui kuwa kupandisha nauli ni kupandisha gharama za kila kitu?

Hakika hii kali kabisa…
 
Pesa ya madafu😁

 
Watu wa Fedha hamna kitu pale wanachojua pale mkuu na kushauri wacha tuwaangalie tu...
 
Tutatumia mabango yake barabarani kulipia hizo nauli.
 
Mfano ulikuwa unakodisha gari linakuletea bidhaa kwa milion 1. Gharama za kukodi gari zimepanda na kuwa milion 1 na laki 2.
Unafikiri bidhaa utaiuza kwa bei ile ile ya mwanzo?
Mbona haihusiani na kupanda kwa nauli za mabasi?
 
Wamechelewa mno na hilo ongezeko haliendani hali ilivyo kwenye bei ya mafuta.
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza mabadiliko ya nauli katika safari za masafa marefu na masafa mafupi baada ya kupitia maoni ya wadau wa usafiri nchini.

Kwa mujibu wa LATRA nauli za safari zisizozidi kilometa 10 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 500 sasa itakuwa 600. Kwa safari za kilometa 11 hadi 15 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 550 sasa itakuwa shilingi 700.

Kwa kilometa 15 hadi 20 ambapo nauli ilikuwa shilingi 600 sasa itakuwa 800 huku kwa safari za kilometa 21 hadi 25 nauli imetoka 700 hadi shilingi 900. Safari ya kilometa 26 hadi 30 nauli ni shilingi 1100, safari ya kilometa 31 hadi 35 ni shilingi 1300 na kilometa 36 hadi 40 nauli ni 1400.

Aidha nauli za wanafunzi zitaendelea kusalia 200 kwa safari za masafa mafupi.

Nauli za mabasi zimeorodheshwa kwenye jedwali hapa chini.

View attachment 2826735View attachment 2826734View attachment 2826733View attachment 2826732
Hatuachi kwenda Mo-Mo-Mo-shi hata nauli iwe 2.5M!
 
Magufuli rip baba tunakukumbuka sana kosa ulilofanya kutuachia huyu kiumbe anatunyosha tu nauli inaongezeka 10000 nzima kwa kazi gani waliofanya hao latra, kwa maisha gani facken kabisa kesho na mimi dukani naongeza bei alfu tano tano kila mtu apige anakoweza.
Nielekeze mtaa unao ishi kesho nije na mali ya magendo mimi nitashusha bukubuku kwa kila bidhaa.
 
wangenipandishia bei za Data tu ile niache upuuzi wa Kuomba connection za kina Giggy money..

Mfano Gb 1 iwe elfu kumi.. hahhahaha
Are you serious ? Unajuwa wanapita humu na hata Mwigulu yumo humu alikuwa member kabisa.

Unaweza kuwa unaandika kwa utani na wenyewe wakaona ni sawa. Ngoja tozo iongezwe ndo utajuwa hujui. Maana wengi wameipenda hiyo post yako usikute wengi ni hao mawaziri ambao wanatumia fake id.

Kama una tatizo la kupenda connections, halafu upandishiwe kifurushi ndo uache? Umekuwa mtoto mdogo?

Siyo wote wanaotumia data kwenye ujinga hata wawe na gb kiasi gani.

Mimi ni WIFi ofisini na nyumbani unlimited data lakini sijawahi kuhangaika na huo ujinga.
 
Coaster hesabu tsh 80,000/= Eicher hesabu laki moja, posho dereva na kondakta 60,000/=

Kulikuwa hamna sababu ya kupandisha nauli,

Service ya gari kwa mwezi jumla laki sita na somethng .

Hapo wamewatengenezea ulaji wenye magari,wanapandisha hesabu
 
Back
Top Bottom