LATRA yatangaza ongezeko la nauli za Safari za Masafa Marefu na Mafupi kuanzia Desemba 8, 2023
Inategemea unapita wapi, tatizo lako unalazimisha iwe Kondoa.

Nimesema kutoka Dodoma kupita Babati kwenda moshi hakuna Kms 1090 bali ni kms 502. Mbuzi wee
 
Nimesema kutoka Dodoma kupita Babati kwenda moshi hakuna Kms 1090 bali ni kms 502. Mbuzi wee
Tena mbuzi wa maziwa kabisa
 
Nimesema kutoka Dodoma kupita Babati kwenda moshi hakuna Kms 1090 bali ni kms 502. Mbuzi wee
🤣🤣love you peno man.
 
Distance between Dodoma and Geita is 540 kilometers (336 miles)

Huku Latra wanasema ni kms 1,659😳
 
Tena mbuzi wa maziwa kabisa
Mbuzi meeee!
tapatalk_1570278204264.jpg
 
Latra wawajibike kwa kudanganya wananchi na kutangaza nauli za uongo unaotokana na umbali.

Na waombe radhi watanzania haraka, kwani wameleta hali ya taharuki nchi nzima.
 
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza mabadiliko ya nauli katika safari za masafa marefu na masafa mafupi baada ya kupitia maoni ya wadau wa usafiri nchini.

Kwa mujibu wa LATRA nauli za safari zisizozidi kilometa 10 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 500 sasa itakuwa 600. Kwa safari za kilometa 11 hadi 15 ambayo nauli yake ilikuwa shilingi 550 sasa itakuwa shilingi 700.

Kwa kilometa 15 hadi 20 ambapo nauli ilikuwa shilingi 600 sasa itakuwa 800 huku kwa safari za kilometa 21 hadi 25 nauli imetoka 700 hadi shilingi 900. Safari ya kilometa 26 hadi 30 nauli ni shilingi 1100, safari ya kilometa 31 hadi 35 ni shilingi 1300 na kilometa 36 hadi 40 nauli ni 1400.

Aidha nauli za wanafunzi zitaendelea kusalia 200 kwa safari za masafa mafupi.

Nauli za mabasi zimeorodheshwa kwenye jedwali hapa chini.

View attachment 2826735View attachment 2826734View attachment 2826733View attachment 2826732
NINGEKUWA NINA MAMLAKA...VIONGOZI WOTE NINGEWANYANG'ANYA MAGARI YA SERIKALI NA MAFUTA WAJILIPIE WENYEWE...ILI WAFEEL KILE WANACHOPITIA WANAOWAPANGIA YALE WANAYOPANGA.
 
Angalia kituko cha Nauli kutoka Dodoma kwenda Iringa halafu Dodoma kwenda Mbeya yaani ni vituko tupu!
 
Mbona ongezeko n kubwa sana kuna ruti ya magar ya mkoan ongezeko n 7000+[emoji357][emoji3482][emoji3482]
 
Nilikuwa sifahamu km kutoka Dodoma kwenda Geita kuna umbali mkubwa kiasi hicho!...
Yaani umbali uliopo ni sawa na kutoka Dar hadi Kigoma?. Ama kweliii
 
Katika miaka hii miwili LATRA imekuwa ikifanya kazi nzuri sana kuboresha huduma za usafiri wa umma hasa mabasi. Tumeshuhudia safari za usiku zikiruhusiwa na kufanya kazi vizuri chini ya usimamizi wa LATRA

Hata hivyo taarifa iliyotolewa jana ya nauli mpya za usafiri mabasi ya ruti ndefu inaweza kuchafua kabisa taswira yao nzuri waliyojijingea na kuharibu maboresho yote waliyokuwa wamekusudia katika sekta ikiwemo mabasi kuhakikisha mzigo yote ya wasafiri inakuwa na lebo yenye taarifa kamili za abiria na abiria kupaswa kuonyesha tiketi yake kabla hajachukua mzigo.

Taarifa ya mabadiliko ya nauli iliyotoka jana ina makosa mengi mno na bila shaka inaonyesha uzembe na ukosefu mkubwa wa umakini wa muandaaji taarifa na aliyeisambaza au kitengo cha mawasiliano cha LATRA kwa ujumla.

Mamlaka husika msameheni Mkurugenzi wa LATRA, amekuwa akifanya kazi nzuri kabla ya mauzauza haya haya, kitengo cha mawasiliano kushughulikiwe kwa kutojoridhisha na usahihi wa taarifa kabla ya kuitoa kwa umma.

Mfano wa makosa ni kama jedwali kuonyesha nauli ya Dar es Salaam hadi Dodoma kuwa sh.5000/= !
 
Nauli ilishapandishwa na wenye mabasi kitambo sana !
Tangu bei za dizeli zianze kupanda tumekuwa tukilipishwa nauli ya shs 65,000/- kwenda Mwanza kwa mabasi ya daraja la kawaida !
Wasitudanganye !
 
Back
Top Bottom