mzamifu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2010
- 6,400
- 3,853
Yaani imekuwa wimbo hoja muhimu ya Lema haitajwi lakini minor issue ya bodaboda ndiyo inawasumbua. Chukueni tukio zima la kuondoka kwake na kisha kurudi sababu ni zipi tujadili.Godbless Lema wa Chadema....
View attachment 2534970
Kwamba bodaboda ni kazi ya laana! Sawa tumekusikia! Ebu tuambie kama umeona hao ni laana! Ina maana kwamba hata abiria wao nao ni laana kubwa zaidi. Maana wao ndio wanaowawezesha hao bodaboda kuweza kujiendesha kutokana na malipo wanayowalipa. Na ikumbukwe kwamba wananchi wengi wa kipato cha kati na cha chini ndio wanaonufaika na huduma hii ya bodaboda nchini Tanzania. Na pia ikumbukwe kwamba kwa hapa nchini Tanzania, hilo tabaka pia ndio ambalo linashiriki siasa katika kiwango cha upigaji kura kwenye chaguzi mbalimbali.
Je, Lema unamaanisha hata wapiga kura wa nchi hii nao wamelaaniwa? Pia tuambie... kama bodaboda ni laana nchi hii. Inakuwaje mnaowatumia kwenye shughuli zenu zote za kisiasa nchini? Je, mnaitumia laana ili kupata political mileage toka kwao?
#Lema na #Chadema njooni hapa mtutajie nchi ya Afrika ambako hakuna bodaboda! Na mnapowaita bodaboda laana, ni kazi ipi mmewaandalia ambayo ni mbadala wa hiyo laana! Msiishie kuchonganisha wananchi huku mkiwa hamna lolote la mbadala vichwani. Mfano mzuri ni hapo #Kenya kwa Rutto, aliwaahidi Paradiso kwa kujiita "Hustler"... Nenda leo Kenya au angalia media zao na uone kinachojiri huko...
Bodaboda hawakumkimbiza au kumrudisha lema! This is very minor, hence, it needs no discussion men!