Lema: Bodaboda imekuwa ni ajira ya Laana

Yaani imekuwa wimbo hoja muhimu ya Lema haitajwi lakini minor issue ya bodaboda ndiyo inawasumbua. Chukueni tukio zima la kuondoka kwake na kisha kurudi sababu ni zipi tujadili.
Bodaboda hawakumkimbiza au kumrudisha lema! This is very minor, hence, it needs no discussion men!
 
 
Ndivyo mnavyodanganyana na vipro pagan da uchwara. Tuambie ni sera gani za CCM ambazo ni bora kuliko hao Unapodai hawana sera.
Mimi sio mpenzi wa CCM kwanza wewe jibu tu hoja CHADEMA Wana sera zipi juu ya Hili Taifa waaminiwe na wananchi?
 
Lema ni mjumbe wa kamati kuu, anachokisema kwenye mikutano yake ya hadhara hatupaswi kuyapuuza, kamati kuu ya chama chetu cha Chadema ndio chombo chenye kutengeneza mipango yote ikiwemo mikakati ya chama kushinda uchaguzi, kwahiyo anapongea mjumbe wa kamati kuu kama Lema, Msigwa nk tunapaswa kumsikiliza kwa makini.

Lema amewananga bodaboda akisema sio kazi, ni kazi ya laana, amefika mbali akidai kazi hiyo imesababisha vijana wengi kuwa vilema.

Jamaa kweli ni mwehu sana ingawa namshabikia sana, hivi Lema hajui kuwa ajali za magari zimesababisha vifo na vilema wengi kama lilivo jina lake? Mbona kuna watu wana mwaka wa 20 huu wanaendesha bodaboda na hawajahi kupata ajali?

Ajali ni mipango ya mungu, hivi wanasiasa wa chadema mnaokwenda kwenye majimboni kuongea na wananchi wenu mtajibu nini mkiulizwa hoja ya Lema, mjumbe wa kamati kuu kuwa bodaboda sio kazi.

Chadema itoke hadharani na kueleza kuhusu hoja hiyo vinginevyo lema rudi Canada aliko mke ukainjoy conjugal rights
 
Nikajua umeambatanisha na press release ya CDM toka kwa katibu kua kama CDM huo ndio msimamo wao!! Kumbe hakuna ni muendelezo wa thread za kitoto toka kwa wachunga ng'ombe wazee wa legacy!!!
 
Hebu acheni upumbavu.
Unapoongelea bodaboda unaongelea value chain ya motorcycle industry yoote kwa ujumla.
Kuna viwanda vinavyotengeneza bike kuna makampuni na mawakala wanaonunua hizo bike kutoka viwandani, pia kuna wauzaji na wakopeshaji wanaouza bike kwa rejareja.

Kuna mabosi wanaonunua bike na kuwapa vijana ambao ndio wanafanya biashara ya bodaboda pia kuna wauzaji spares na mafundi wa bike.

Hivyo unaposema bodaboda ni kazi laana unakua umehusisha watu wote waliokwenye mnyororo wa thamani wa industry ya bodaboda.
 
Hoja zao mbofu mbofu kweli!
Yaani wanatembelea na ile Doctrine ya kiinjili. Gospel!

A Gods intervention
 
A must read

The Transactional Context of Psychological Normality.

Jeremiah 26:2-7

The Industrial Revolution: The conflict between English and Irish Workers etc etc

Lema na CHADEMA ni vibaraka wa mabeberu.

Hawana sera za kuuza, wanahubiri injili...."The angry white man" mentality!
 
Mkuu, usiifanye hii kuwa ajenda kuu. By the way kabla Adam na Hawa hawajalaaniwa, walikuwa hawafanyi kazi yoyote.
Mungu aliwapa assignments ndogo ndogo kama vile ya kutunga majina ya wanyama na ndege.
Siku walipolaaniwa, Adam akaambiwa kwa jasho utakula.
Kwa hiyo unaweza kuona kuwa kufanya kazi ni laana. Ni matokeo ya binadamu kulaaniwa na Muumba wake.
Wastaafu wenye pensheni ambao kwa sasa hawali kwa jasho ndio baadhi ya binadamu ambao wamevuka 'mstari wa laana' kwa vile hawali tena kwa jasho...
 
Hii ni muda mchache uliopita. Sasa mnadhani vijana wangapi nchi nzima wanakumbana na haya madhila siku ya leo?
 
Hii ni muda mchache uliopita. Sasa mnadhani vijana wangapi nchi nzima wanakumbana na haya madhila siku ya leo?View attachment 2536796
halafu mapoyoyo ya ccm yakiambiwa bodaboda ni kaz ya laana yanapayuka payuka haya wafuas wa lumumba nenden kwa huyo kijana aliyegongwa mumuulize kama kaz ya bodaboda anaifurahia na kama haifurahii bas ni kaz ya laana
 
yani chadema iwe vibaraka wa mabeberu huku mamayenu wa ccm anaenda kukopa kwa mabeberu kila siku had deni limefika trillion 76, kama hujui mamayenu ccm na mamayenu ndio mawakala ya mabeberu ndio maana mnakimbilia kukopa huko kila siku wapuuz kabisa.
 
Mimi sio mpenzi wa CCM kwanza wewe jibu tu hoja CHADEMA Wana sera zipi juu ya Hili Taifa waaminiwe na wananchi?
Hata mimi siyo mapenzi wa Chadema. Pia ushasema Chadema hawana sera. Sasa kwa nini unaniuliza tena kuhusu sera zao.
 
Wasubiri ajira ama
Marekani kila mwaka inapeleka maelfu ya wahitimu wake wa vyuo vikuu katika nchi za ulimwengu wa 3 kwa ajili ya kujitolea kwa mkataba miaka isiyopungua miwili, huku wakilipwa posho ya kujikimu.

Baada ya hiyo miaka miwili, wanarudidi nchini mwao kwa ajili ya kuajiriwa. Sisi nchini mwetu kuna sekta kibao za serikali zina upungufu wa watenda kazi! Lakini serikali inashindwa kutoa ajira za kujitolea kwa wahitimu wake.

Badala yake, wako tayari kufanya matumizi yasiyo na ulazima wowote ule, na mwisho wa siku wahitimu wa vyuo vikuu baadhi yao wanaishia kuwa bodaboda.
 
Nimekaa karibu dakika mbili tatu nikitafuta maneno ya kuandika juu ya maneno haya uliyoweka hapa katika hii mistari michache niliyonyanyua kwenye bandiko lako.

Ninakubaliana na wewe bila ya kupinga chochote hapo.
Ila, huenda tofauti inayoweza kuwepo kati yako na mimi juu ya swala hili ni kwamba ni uamini wangu kuwa niko tayari kuunga mkono chama kingine chochote kinachoonekana kuwa na uwezo wa kuwaondoa CCM madarakani kwa sasa, bila kujali chama hicho kimejitangaza kufanya mambo gani kikiwa na madaraka.
Kwa hiyo, kwa upande wangu, kukitokea kupiga kura leo, nitawapa CHADEMA kura yangu ili wawaondoe CCM madarakani. Wakishafanya hivyo, tunaanza mwanzo mpya wa kuwaza ni chama kipi kinachosimamia zaidi maslahi ya waTanzania.

Hii ndiyo 'bottomline' niliyoifikia katika kutafuta uhuru wa nchi yetu toka kwa mkoloni mpya CCM.

Sera za CHADEMA hazinipi matumaini hata kidogo kuhusu hatma ya Tanzania na wananchi wake. Wakiweza kutufanyia hiyo kazi ya kuwaondoa CCM, tutawashukuru; lakini baada ya hapo, kama hawana msimamo mwingine kuhusu sera zao, tunaachana nao njia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…