Lema: Bodaboda imekuwa ni ajira ya Laana

Lema: Bodaboda imekuwa ni ajira ya Laana

Bodaboda na Bajaji na Machinga wakiwekewa utaratibu mzuri na miundombinu na wawe operational maeneo Fulani Fulani ni kazi ya kuingiza kipato..

Huko Vijijini ni usafiri muhimu sana,kwanza sijajua inakuaje laana.
Elimu aliyonayo Lema haina uwezo wa kuyafikiri yote haya kwa umakini wake.
Yeye alijua tu akisema ni "laana' atashangiliwa.

At least, angejitahidi kidogo kueleza alichokusudia kusema hilo neno, halafu na kutoa mbadala wa laana hiyo, au kuifanyia marekebisho, hapo ingemfanya aonekane kuwa na maana kidogo.

Kwa ujumla, sijawahi kuona umahiri wowote wa kisiasa toka kwa Lema, mbali ya matukio tu yahusuyo misuguano ya CHADEMA na CCM.

Na siyo Lema pekee, katika viongozi wengi wa chama hicho. Wengi wanazosifa za vijimambo mambo tu. Katika hao nawaondoa Heche, Mnyika pamoja na Lissu.
 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kutetea Rasilimali za Taifa ya WARAMI, Philip Mwakibinga amekubaliana na Lema!
Hello!

Naona Lema ameanza kwa gia ya matusi kwa wanaojiita bodaboda. Lema amesema bodaboda sio kazi ila ni laana.

Hivi hizi si ni dharau kwa vijana wa bodaboda? Yaani watu wanaendesha familia kwa kazi hiyo halafu anakuja mtu anawadharau na kutukana eti wamelaaniwa?

Nyie wafuasi wa CHADEMA mnaposhabikia watu muwe mnajitambua. Hawa kina Lema wamekuwa wabunge hapo Arusha miaka 10, waliwafanyia nini cha maana?

Ujinga kama huu wa CHADEMA ndio kina Ruto walikuwa wanawadanganya Kenya badala yake hakuna cha maana anafanya; ameongeza tax, ameondoa ruzuku kwenye mafuta maisha yako juu, anakopa na alisema hatokopa, anaomba misaada ya chakula hadi Ukraine, mfumuko wa bei ndio usiseme nk.

Ujinga kama huu wa upinzani ulifanyika hata Malawi, kawaulize Wamalawi kama kuna nafuu wamepata, the likes ya Zambia.

Ukiwasikiliza CHADEMA huwa wanaota ila hawana strategy ya kile wanachoota, uje uwaulize watawatoa vipi Watanzania kwenye umaskini kama wanavyodai wakati hawana hata sera inayoeleweka.

Toka nimeanza kuwasikiliza CHADEMA zaidi ya Katiba Mpya na mambo ya Majimbo hakuna jipya, maana hizo political tools sio nyenzo za kuondoa watu kwenye umaskini.

Mwisho, ukiwasikiza ACT Wazalendo unaona content ila ukiwasikiza CHADEMA unaona ulalamishi na kuorodhesha matatizo ya Watanzania bila suluhisho.

Watanzania stukeni mnafanyiwa ngazi za kutengenezea watu maisha.

 
Mkurugenzi wa Taasisi ya Kutetea Rasilimali za Taifa ya WARAMI, Philip Mwakibinga amekubaliana na Lema!
Baada ya kukubaliana ametoa njia mbadala? Ni mpuuzi tuu Kwa sababu ana pa kushika ndio maana ana jeuri.

Mtakumbushwa 2025
 
Elimu aliyonayo Lema haina uwezo wa kuyafikiri yote haya kwa umakini wake.
Yeye alijua tu akisema ni "laana' atashangiliwa.

At least, angejitahidi kidogo kueleza alichokusudia kusema hilo neno, halafu na kutoa mbadala wa laana hiyo, au kuifanyia marekebisho, hapo ingemfanya aonekane kuwa na maana kidogo.

Kwa ujumla, sijawahi kuona umahiri wowote wa kisiasa toka kwa Lema, mbali ya matukio tu yahusuyo misuguano ya CHADEMA na CCM.

Na siyo Lema pekee, katika viongozi wengi wa chama hicho. Wengi wanazosifa za vijimambo mambo tu. Katika hao nawaondoa Heche, Mnyika pamoja na Lissu.
Lema anawaharibia sana cdm ,imagine swala la vikoba na maswala ya microfinance na duniani kote haya mambo yapo.Nakubaliana na wewe kabisa kuwa huyu jamaa elimu yake ni ndogo mnoo kiasi kwamba hawezi tambua kuwa vikoba ni microfinance
 
Ingekuwa bodaboda tunapanda sie mafukara tu basi ningesema wewe hujawahi kupanda bodaboda kwa sababu ni wa kishua.
Sasa hutaki?

Sijawahi kupanda bodaboda maishani.

Yani nilikaa Tanzania kabla bodaboda hazijaanza nikajua huko mbele kutakuja bodaboda, nikaondoka nchini.
 
Uvccm buana [emoji28]
FB_IMG_16762806455838775.jpg


Sent from my DRA-LX5 using JamiiForums mobile app
 
Sasa hutaki?

Sijawahi kupanda bodaboda maishani.

Yani nilikaa Tanzania kabla bodaboda hazijaanza nikajua huko mbele kutakuja bodaboda, nikaondoka nchini.
Kawaida tu hata mie sio mpandaji sana wa bodaboda mpaka pale napolazimika.
 
Muwe naelewa Alichomaanisha, msikimbilie kukashifiwa tu, Hakuna mtu anaependa kuuza. Madawa uku akijua adhabu zake, lakini Inabidi tu afanye ili maisha yasonge
Ifanye akili yako iwe msaada wa maisha kwako acha kujifungia
 
Muwe naelewa Alichomaanisha, msikimbilie kukashifiwa tu, Hakuna mtu anaependa kuuza. Madawa uku akijua adhabu zake, lakini Inabidi tu afanye ili maisha yasonge
Ifanye akili yako iwe msaada wa maisha kwako acha kujifungia
Mkuu lakini bodaboda ni kazi halali hata kama mtu anafanyia shida, ina maana badala ya kuuza hayo madawa ya kulevya au ujambazi ameamua kufanya bodaboda ili kupata riziki yake kihalali hata kama ni kiduchu, sasa kuita kuwa ni laana lazima usieleweke. Mfano kazi ya umalaya huwa inalaaniwa kila siku na ni kawaida kwa sababu inafahamika si kazi halali kweli ni laana ila kuita bodaboda kuwa ni laana unakuwa hujaitukana serikali ya ccm tu kama hata huyo Lema anavyodhani bali unawatukana hao waendesha bodaboda wenyewe. Hakuna namna unaweza kueleweka mkuu, kulikuwa na namna ya kuelezea pasina kuita ni laana.
 
Ukitaka kuamini Tanzania ni nchi inayoongozwa na wapumbavu na wapuuz na ndio reflection ya hata raia wake wengi walivyo , pale Kagera au Kilimanjaro na Arusha watu wanalima kahawa huko vijijini wakitaka kupeleka kuvukisha border kwenda kuuza hapo Uganda au Kenya Tu ambapo bei ni zaidi ya mara mbili ya hapa Tanzania na malipo ni cash wala hakuna kukopwa na kutapeliwa kama kwenye vyama vya ushirika hapa Tanzania ,imagine serikali inawawinda wakulima wanaotaka kwenda kuuza huko kama nini sijui ,hivi ni akili za wapi ?

Na hapo nimeongelea sekta moja tu ya kilimo na ufugaji , sekta ya kilimo tu kama ingefanyika na kusimamiwa kikamilifu kwa tija leo hii kusingekuwa na upuuz wa vijana kukimbilia mjini kuwa mamachinga wa bidhaa feki za kichina na kuwa maboda boda na kufanya kazi nyingine za ovyo zisizo na future ,hiyo ya kufanya hizo kazi ni watu kukosa options za kuendesha maisha yao kutokana na umasikini uliopindukia
 
Kama tunataka hii nchi kuchomoka kwenye umasikini kwa muda mfupi ,option iliyopo ni kuwekeza kwenye kilimo cha tija , settler economy , watu raia wapewe mitaji ,mitambo na kutengenezewa nyenzo au minundombinu wezeshi kama usafiri wa reli na barabara kumove hicho kinachozalishwa huko pori , watu wawe trained kwenye modern agricultural techniques bure na wawe encouraged kumove country side huko porini na kufanya mass agricultural plantation economy kama huko Australia na hata canada na Marekani hizo nchi ziliendelea kwa kupitia hii settler economy concept , mass agricultural production kuuza nje kwa tija ndio solution hapo kuna mamilioni ya ajira zinatengenezwa na at the same uchumi wa nchi unainuka na umasikini wa kaya na mtu mmoja mmoja kupungua kwa kasi , Brazil wamefanya angalia walipo sasa hivi .
Why sisi ? Jibu ni ccm, hii ndio laana na kizuizi kikubwa nchi hii .

Ni aibu nchi kubwa hivi land iko empty na haijawa utilized ipasavyo halafu tunazalisha millions of unemployed youths wanaoishia kuwa maboda boda ,mamachinga na kazi za ajabu kama hizo
Mabaresho makubwa yafanyike katika sekta nyingine mfano madini , kufaidisha raia wa kawaida wa nchi hii
 
Mfano mdogo wenzetu wana ufugaji wa samaki kwa scale kubwa ,cafe fish farming na hii inafanyika kwenye maziwa na bahari , ni moja wapo ya kitu inwezafanyika na tunazalisha samaki wengi tu kama export product huko nje ya nchi ,samaki bado ni kitoweo ambacho kinapendwa na demand yake bado ni kubwa , tukifanya mass production ya mifugo na kilimo hata sekta ya viwanda itachochewa maana tutafanya processing hapa then tunauza nje ya nchi refined products si tunakuwa tumeua ndege wawili kwa jiwe moja.

Just imagine wachina wameshaiona idea na wameanza kuwekeza ziwa Victoria kwa Mwanza kuna sehemu za ziwa nimeona wameshangaa hizo projects ,sasa kama watu wanatoka china wanakuja kuwekeza kwenye hizo ideas ,why serikali ya kipumbavu ya ccm isiwekeze ,kuwatrain na kuwawezesha raia wake kucapture hizo opportunities ?
 
Kuna jamaa alinitania kuwa Wachaga hawajui kuongea ila ni upigaji tu wa pesa. Sasa muone Lema, hapo kasema nini?
 
Hakuna neno dogo Kama samahani na lenye thamani kubwa sana maana wakubwa wanasema "unapokosea kuchutama siyo dhambi.

Hakika nimefadhaika sana juu ya huyu mwanasiasa mkimbizi godbless lema kutamka maneno yasiyofaa mbele ya kamera na waandishi wa habari wakimtazama nakumchekea maana ya kwamba kazungumza vitu vya msingi sana.

Bodaboda ni kazi iliyo watoa vijana kutoka kwenye ukabaji, matumizi ya madawa ya kulevya mpaka kwenda kufanya kazi ya bodaboda nakuhudumia familia zao Hadi kujenga nyumba kujilipia chakula, Kodi na mavazi.

Leo hiii anakuja mpuuzi mmoja kutoka mafichoni nakuleta dharau nakuanza kusema bodaboda ni kazi iliyo laaniwa, kiukweli nimechafukwa sana.

Na siyo Mimi tu tuna vijana wengi hawana elimu hawakubahatika kujiendeleza na elimu wapo huko kwenye bodaboda wakiendesha maisha yao.

Godbless lema hii haipo sawa, tunajua umekuja huku kusikilizia upepo Kama unaweza kupata madaraka yoyote katika hiii nchi na utakapoona hakuna madaraka utarejea Tena huko ulipotoka na ndiyo maana umekuja peke yako familia umeiacha huko mafichoni.

Tengua kauli yako haraka iwezekanavyo bodaboda siyo Kazi ya laana na Kama ni laana basi kailaani Bibi yako.

Nasimama na bodaboda kupinga huu upuuzi uliozungumzwa na Mwanaharakati feki.
 
Macho yako kwenye katiba mpya ndugu kwenye reli hatoki mtu
 
Yule pale kasema vizuri Ila wao tu, kasema ili serikali wajiongeze kwa kufikilia fursa za vijana, Kama kazi nzuri mtoto wa kikwete , lowasa, sumaye,au makamba, waendeshe bodaboda.
 
Godbless lema-- Ubodaboda ni kazi ya laana. Mpwayungu village-- Uwalimu ni kazi ya laana. [emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom