Pre GE2025 Lema: Nikiwa na Wenje, Heche na Msigwa makamu Tundu Lisu alituhakikishia Nafasi atakayogombea Mbowe basi Yeye hatachukua fomu!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Lissu anahakikisha amekibomoa hicho 'kikundi' kabla ya kuhamia chama chake kipya.
 
Sintofahamu ukiendelea baina ya viongozi wa Chadema Kwa pande mbili za Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho juu ya nani anastahiki kuwania Urais 2025,baadhi ya wapambe wa viongozi hao nao wameongia na kuanza kutishana

Mmoja wa viongozi hao ni Godbles Lema ambaye amemtaka Lissu akumbuke juu ya wema wa Mbowe wa kumshikia chupa ya Damu wakati aliposhambuliwa Kwa risasi

Katika andiko lake lema amelitaja andiko na Uchambuzi wa mwanasiasa Bob Wangwe kuwa ni Sehemu ya maandiko ya watu wanaotumwa na CCM kuwachonganisha viongozi hao

Lema amendika "Tulipokuwa Mimi Lissu Heche,Msigwa na viongozi wengine Lissu alikumbushia kuwa hatochukua fomu yoyote kushindana na Mbowe Kwa kuwa alishika chupa ya Damu pale alipokuwa ameshambuliwa

Andiko Hilo la Lema linamtahadharisha Lissu kuwa Mbowe alimuokoa na kuruhusu kushindana nae ni sawa na kusaliti wema aliomfanyia alipokuwa akiumwa
 
Kwa hiyo mbowe kubeba chupa mpaka Nairobi ndio ilikuwa malipo yake asigombee?kwa nini mnavunja katiba yenu wenyewe kwa ujinga ! Kwa nini msiruhusu demokrasia iongee? Chadema ni wajinga sana
 
Godbless Lema ameandika ukurasani X

Halafu wakitoka hapo wanasema CCM inatoa Fomu Moja

Siasa za Tanzania pasua kichwa sana aiseee
We naye Acha kupotosha weka statement yote. Alichoandika lema mwishoni anadai lissu anasema "wapambe wasitugombanishe" na hiyo ndio ilikua quotation ilipoishia. Cha ajabu umechukua maneno ya kwanza ukayakatiza katikati. Hivi Jamii check kazi yake ni nini hasa kama fake news hazifutwagi?
 
Lissu atagombea urais na Mbowe uwenyekiti hawa wanajuana watagawana majukumu
 
Bottom line ni statement nzima kwamba "wapambe wasitugombanishe". Chadema hakuna crisis yoyote kama ni kugombea urais, mbona Lissu aligombea 2020 licha ya Mbowe kuchukuliwa fomu ya urais na wapambe?

Issue kubwa ya hiyo statement ni kwamba Lissu hataki wapambe wawakosanishe wakati personally anamheshimu Mbowe and vice versa kwa kurejea issue ya Mbowe kusimama kwenye ndege akishikilia chupa za kumuongezea damu hadi Nairobi.
 
Hiyo ni endapo Lissu ndiye angekuwa ameitoa hiyo statement.
Lema kusema hivyo tafsiri ni tofauti.
 
Kwa hatua iliyofikia inabidi Lissu akubaliane na hali au ahame chama. Iko wazi kuwa Mbowe kamtumia Lema kufikisha ujumbe kwa Lissu. Na Lema kafanya vizuri sana kutamka kuwa kulikuwa na mashahidi. Godbless Lema kaandika hivi mitandaoni
Mgogoro upi? Mbona message ipo clear kuwa Lissu hayupo ku compete na yeyote ila issue ni wapambe kuwakosanisha? Na hili ndio la muhimu zaidi.

Kama hayo aliyosema Lema ni ujumbe wa Mbowe, mbona 2020 Lissu alichukua fomu ya kugombea Urais licha ya Mbowe "kuchukukuliwa" fomu ya kugombea Urais?
 
Chama chako hakuna haja ya kupangiwa cha kufanya
 
It's too late. Chawa hamwezi kuokoa jahazi lililozamishwa na Lema. Statement ya Lema iko wazi kumwambia Lissu akumbuke fadhila. Na hapo Lema kamwambia kistaarabu sana kwasababu Lema alishawahi kumshurutisha kiongozi mwenzake Msigwa afute post yake kwa neno moja tu FUTA.
 
Mimi ninachokiona ni kushamiri kwa Demokrasia ndani ya Chadema.
 
Lissu mroho wa madaraka
 
Mimi kwa maoni yangu Freeman Mbowe bado chadema imamhitaji kama Mwenyekiti

Katika kosa kubwa chadema watafanya ni kumpindua Mbowe ndani ya uongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…