Pre GE2025 Lema: Nikiwa na Wenje, Heche na Msigwa makamu Tundu Lisu alituhakikishia Nafasi atakayogombea Mbowe basi Yeye hatachukua fomu!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndio maana Lissu hakuitwa Ikulu na Mama aliitwa Mbowe peke yake
Akauza uzaliwa wake wa kwanza. Biashara ikaisha. Lissu anahangaika bure Uchaguzi ulishaisha kinachofwata ni ule wa kikatiba
 
CHADEMA inaendelea kunishangaza siku hadi siku. Leo hii akitokea Mwanaccm akasema maneno anayosema Lema kuwa Lissu alimwambia Mbowe, CHADEMA yote na hao kina Lema watamkosoa na kumuita CHAWA.

Itokee leo Mwigulu au waziri mmoja aseme hawezi kugombea urais anamuachia Samia kwakuwa ni mwema sana kwake amempa uwaziri, uone vile ataogeshwa kejeli na hao akina Lema.

Hii nchi kwasasa ina watu wadhaifu sana wasioweza kushindana na wanapenda kusifiwa na kupongezwa bila sababu na ndio maana uchawa umekuwa ajira rasmi.
 
😂😂😂😂😂😂 Eti kulipana fadhilaa daaa nimejikuta nimechekaa tu madam
 
Ndio maana Lissu hakuitwa Ikulu na Mama aliitwa Mbowe peke yake
Akauza uzaliwa wake wa kwanza. Biashara ikaisha. Lissu anahangaika bure Uchaguzi ulishaisha kinachofwata ni ule wa kikatiba
Ikulu wanaitwa wenye busara, sio vichaa
 
Wewe na nani?
 
Lema acha kutoa povu ,binamu yako Mzee Mbowe lazima aachie kiti cha uwenyekiti
 
Wenye busara Tanzania Ndio wezi wakubwa, Si watu wa kuaminika
Lissu aliifilisi LEAT, Lawyers Environmental Action Team, yeye na genge lake, walikodi maofisi kila mahali mpaka jengo la Nyanza kule, wakapiga hela, wakakaa kimya
 
Huyo jamaa Msukule wa Mwenyekiti kitambo kabla hata ya shambulio la risasi.

Wenye akili timamu wote wamewahi kutofautiana na Mbowe walau kwa jambo moja na wakaonesha msimamo wao hadharani ila siyo huyo jamaa.
 
kwani tatizo likowapi sasa
 
Mbowe anatosha yeyenimwamba imala mbowe atatuvusha
 
Ndio maana nilijiondoa kushabikia siasa za Tanzania
 
Mimi sijawahi kumkubali Lema ni kama kidudu Mtu. Mazungumzo ya kwenye kahawa analazimisha yawe sheria. Mbona Mbowe aliahidi atastaafu mwaka Jana? Imekuwaje Tena?.
Ndio maana naambiwa msiwe machawa wa siasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…