Leo 16 September Mahakama inaendelea kesi ya uhaini inayomkabili Tundu Lissu dhidi ya Jamhuri

Ni kweli maana summon inasema unaitwa mahakamani siyo unaitwa na lissu.
Wasitupange waje tuu wale top 3 yetu
 
Hao majaji sijui kama wana akili, waliosema wapelekewe summons ni nani kama sio wao wanaleta mambo ujanja janja wao kwenye kesi kubwa kama hii, i knew it kama haya yatatokea wanatafuta kichaka chakukimbilia
Hakuna kukimbia wala janja janja za kiwaki, mashahidi hao wanatakiwa kuwepo mahakamani, laa hasha kanuni na sheria zifuate kadri ya matakwa yake.
 
MAJIBU YA MAHAKAMA KUHUSU MASHAIDI WA TUNDU LISSU KUFIKA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1.

MAHAKAMA IMEREJEA

Majaji na Mshtakiwa wameingia kwa pamoja.

Mawakili wa Serikali wapo tayari.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, kolamu kwa upande wa Jamhuri ipo kama ilivyokuwa awali.

Mshtakiwa yupo na sisi tupo tayari kuendelea, kama Mwenye Kesi yake yupo tayari.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, baada ya maelekezo ya Mahakama, nimeonana na Msajili wa Mahakama hii.

Amekuja kuniona kuniletea taarifa za summons za kuwaita mashahidi wa Mahakama.

Mheshimiwa Msajili amenitaarifu kwamba mashahidi wote walipelekewa summons Dodoma. Hata hivyo, haikuwezekana kuwa-save nakala za summons baada ya kusemekana wapo nje ya nchi.

Mheshimiwa Msajili anasema kati ya hao watatu, mmoja ambaye ni Kamishna wa Polisi, Afande DCI, Mkurugenzi wa Upelelezi katika Jeshi la Polisi, anatarajiwa kurudi nchini leo.

Msajili ameniahidi kuwa siku ya Ijumaa Kamishna wa Polisi atakuwepo Mahakamani kuja kutekeleza wito wa Mahakama.

Wale wengine wawili, ambao ni Generali Jacob Mkunda, ambaye ni Mkuu wa Majeshi, na IGP Camillius Wambura, haijulikani watakuja nchini lini.

Katika haki ya namna hiyo, napendekeza tuahirishe kesi hadi siku ya Ijumaa saa 8:30 mchana.

Ili session ya asubuhi nitumie kushauriana na shahidi, ikiwa ni pamoja na kuchukua maelezo yake.

Baada ya saa 8:30 nitakuwa tayari kuendelea naye.

Kuhusu waliobaki, tusubiri tumalizane na aliyepo. Then tutafanya maamuzi.

La mwisho, Waheshimiwa Majaji, nafahamu jinsi ambavyo ratiba ya shauri hili ilivyo tight, vilevile na mimi nataka sana twende kwenye final submission, ili tupate muda wa kusubiri uamuzi wenu.

Kama watatii wito wa Mahakama na kuja, imani yangu ni kwamba hatutochukua muda mrefu.

Kama mpaka tunamaliza na huyu aliyepo, tukimaliza na hawajaja, nafikiri naweza kuwa na uamuzi kama bado nawahitaji au la.

Wasipokuja kabisa, Waheshimiwa Majaji, hilo litakuwa mikononi mwenu.

Kwa sababu nyie ndiyo mlio-toa summons.

Ya kwangu ni hayo, Mheshimiwa.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA.


SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
H
Hivi shahidi asipotokea mahakamani anafanywaje? Yaani adhabu yake ni nini.
Mana wanaweza wasitokee mahakamani na wakatumikia adhabu ya kutofika mahakamani
 
Mawakili wa serikali wanetia aibu kwa hili la kutaka kumhoji tena John Heche kwa kisingizio cha kuongea na waandishi wa habari. Wamesahau kama yeye ni Makamu mwenyekiti wa chama cha siasa, na pia ana haki ya kuongea kuhusu masuala ya demokrasia na utawala bora.
 
MAJAJI WANATOA MAAGIZO YA MWISHO

Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka

Nassoro Katuga Waheshimiwa Majaji kwa masikitiko sina pingamizi la kuhairisha kesi

Waheshimiwa nakumbuka Mahakama ilisema Mwisho tarehe 18

Jaji: Tarehe 26

Nassoro Katuga: Kwa maana hiyo hatupingi kuhairisha kesi

Tunaomba Mahakama hii imsisitize Mshtakiwa Mashahidi wake wafike kwa wakati.

MAHAKA KICHEKO πŸ˜€ πŸ˜€ πŸ˜€

Jaji Ndunguru: si Mashahidi wake jamani, yeye ndo anatakiwa kuwaleta Mahakamani.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo Waheshimiwa tunaomba tusisitize Mshtakiwa aweze kuwaleta

Tutakuwa tumepoteza siku ya leo nusu na kesho tungeweza kumaliza shauri

Swala la kama Wasipo fika anaiachia mahakama , Mahakama ifanye nini.

Yeye ndiyo anatakiwa Kuiomba Mahakama iwafanye nini Mahakama

Jaji Ndunguru: unaposema anaiachia Mahakama, Mahakama ifanye nini.

Nimekumbuka ule msemo wako Mahakama siyo mama yako.

MAHAKAMA KICHEKO πŸ˜€ πŸ˜€

Nassoro Katuga: ni hayo tuh Waheshimiwa Majaji.

Jaji Ndunguru: kwa hiyo Shauri kwa leo linahairishwa hadi Ijumaa tarehe 18.

Saa 8 kamili badala ya saa 8 na nusu.

TUKUTANE IJUMAA SHAHIDI ALETWE HATA KWA MACHELA.πŸ˜€
 
Ni kweli maana summon inasema unaitwa mahakamani siyo unaitwa na lissu.
Wasitupange waje tuu wale top 3 yetu
Waje haraka sana, na hatutaki kusikia wana udhuru wowote, wanatakiwa wawepo mahakamani kutolea ushahidi juu ya case kubwa na ya mwisho kwa katiba ya TZ, Uhaini ni case ambayo anapoteza hatma ya mtu endapo kuna utaratibu utakiukwa, hivyo hatutaki kuona hilo.
 
Ni uongo,Mkunda jana nimepishana na msafara wake kimara akiwa anaelekea nyumbani kwake kule maramba.
 
Dah.. Tanganyika nchi yangu, yaani viongozi wote wakuu wa ulinzi na usalama hapa ninapoandika comment hii hawapo nchini..!

Self defence ni muhimu sana kwa kila Raia..!!
 
Sidhani kama ni kweli wapo nje yaa nchi. Hawa CCM janja janja sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…