Leo ni leo asemaye kesho muongo. Polepole kuongea na Watanzania saa mbili kamili usiku! Usikose!

Leo ni leo asemaye kesho muongo. Polepole kuongea na Watanzania saa mbili kamili usiku! Usikose!

Hakika Wakati wa Mungu ni wakati sahihi

HATIMAYE Watanzania Kila Mahali wamechoshwa na Wahuni, ni kama Serikali ya Kikwete ilivyochokwa mwaka 2010-2015.

Nimepitia Online TVs Kadhaa ambazo ziko Live zikingoja Mh Polepole The Intelligent Aanze Press yake, Kuna maelfu ya Watanzania wake Kwa waume wanaendelea kutoa ya Moyon huku wakimsubiri Mzalendo !!.

Unaweza sema hivi, Maelfu ya watu walioko Live muda huu kwenye Media wakimsubiri Mh Polepole, ni Mara ya mia ya watu kwenye Hotuba yoyote ambayo Samia Huwa anazungumza.

Kataawahuni
Tanzaniakwanza
Kwani imekuaje?

Aliahidi kuwa angekuwa hewani saa 2:00Usiku, lakini nyingi ya YouTube channels zikaweka hotuba zake zilizopita na kudanganya kuwa hiyo ndiyo "live broadacasting" ya leo wakati sio...

Kama anahujumiwa, anapaswa kutumia akili zaidi kuliko wao. Mfano;
➡Mosi hakupaswa kutangaza kuwa angezungumza na Watanzania muda fulani. Yeye angezuka tu na kuanza kumwaga upupu...

➡Na pili, angekuwa anatumia utaratibu wa kurekodi hotuba zake na kuzisambaza kwenye channels ambazo hazifungamani na wahuni kama anavyofanya Askofu Gwajima..

Haikuwa sawa kutudanganya kuwa atakuwa live saa 2 usiku halafu muda ukafika, kukawa hakuna kitu chochote na yeye kunyamaza kimya tu bila taarifa yoyote wala kuomba radhi.

Asije kuwa naye ni muhuni anayetuzuga tu hapa kutupotezea focus ya NO REFORMS NO ELECTION..
 
Sound check, sound check, lighting check

UMUHIMU WA KUWASILIANA NA UMMA UNAOKANDAMIZWA

Nakala ya Los Angeles Times kutoka 1986 inatufahamisha kwa mwanamume wa Soweto wa umri miaka 30 wakati wa Utawala wa Kibaguzi South Africa aitwaye Sipho ambaye alijiita "kipaza sauti cha binadamu."

Sipho alisikiliza Radio Uhuru ikitangaza kutoka idhaa ya Radio Dar es Salaam usiku ikiongelea umuhimu wa mabadiliko na kisha, asubuhi iliyofuata, akarudia kile alichosikia, kwa sauti kubwa, kwenye treni za abiria zilizojaa kuelekea Johannesburg.

Alimwambia mwandishi wa habari wa gazeti tajwa la Los Angeles Times kwamba "Wanataka kila asubuhi kwa sauti ni waletee habari, na wanaondoka kwenye treni sio tu wakizungumza kuhusu ANC tu lakini tayari kuifanyia kazi, na kuipigania kuleta mabadiliko ."
1755812930511.jpeg
 
Na bado

Polepole jogoo wa Pasaka, kapiga mkwaara siku ya ‘Iyd, kaja shuwashuwa, asichinjwe. Mikwaara mingi mwisho kapekwa joshi, kawa kama mtwana, kaoshwa. Atoke mwengine, tumjuze hii si ya mchezo na Mama. Kule Chugastan, wanamuita Mama la Mamama. Sasa yule kinyang’unya ati katishia kuachiya shuuzi, wakati mweyewe kaharishiya. Kiko wapi e? Siye twapeta, twashusha bendera bila khofu. Mama yupo sana, Mama kaketi Ikulu, miaka kumi na tano wala hamna la kujuza. Na bado hamjaona, wallah hamjaona.
Jinsi ulivyo andika unaonekana ni mshauri wa rais.
 
Back
Top Bottom