Leo ni leo asemaye kesho muongo. Polepole kuongea na Watanzania saa mbili kamili usiku! Usikose!

Kwani imekuaje?

Aliahidi kuwa angekuwa hewani saa 2:00Usiku, lakini nyingi ya YouTube channels zikaweka hotuba zake zilizopita na kudanganya kuwa hiyo ndiyo "live broadacasting" ya leo wakati sio...

Kama anahujumiwa, anapaswa kutumia akili zaidi kuliko wao. Mfano;
➡Mosi hakupaswa kutangaza kuwa angezungumza na Watanzania muda fulani. Yeye angezuka tu na kuanza kumwaga upupu...

➡Na pili, angekuwa anatumia utaratibu wa kurekodi hotuba zake na kuzisambaza kwenye channels ambazo hazifungamani na wahuni kama anavyofanya Askofu Gwajima..

Haikuwa sawa kutudanganya kuwa atakuwa live saa 2 usiku halafu muda ukafika, kukawa hakuna kitu chochote na yeye kunyamaza kimya tu bila taarifa yoyote wala kuomba radhi.

Asije kuwa naye ni muhuni anayetuzuga tu hapa kutupotezea focus ya NO REFORMS NO ELECTION..
 
Sound check, sound check, lighting check

UMUHIMU WA KUWASILIANA NA UMMA UNAOKANDAMIZWA

Nakala ya Los Angeles Times kutoka 1986 inatufahamisha kwa mwanamume wa Soweto wa umri miaka 30 wakati wa Utawala wa Kibaguzi South Africa aitwaye Sipho ambaye alijiita "kipaza sauti cha binadamu."

Sipho alisikiliza Radio Uhuru ikitangaza kutoka idhaa ya Radio Dar es Salaam usiku ikiongelea umuhimu wa mabadiliko na kisha, asubuhi iliyofuata, akarudia kile alichosikia, kwa sauti kubwa, kwenye treni za abiria zilizojaa kuelekea Johannesburg.

Alimwambia mwandishi wa habari wa gazeti tajwa la Los Angeles Times kwamba "Wanataka kila asubuhi kwa sauti ni waletee habari, na wanaondoka kwenye treni sio tu wakizungumza kuhusu ANC tu lakini tayari kuifanyia kazi, na kuipigania kuleta mabadiliko ."
 
Jinsi ulivyo andika unaonekana ni mshauri wa rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…