Leo ni leo asemaye kesho muongo. Polepole kuongea na Watanzania saa mbili kamili usiku! Usikose!

Niwe mkweli, kuingia mitini kwa Polepole Leo bila taarifa yoyote kazingua Sana. Alitakiwa atoe taarifa ya kuhairisha Mkutano wake. Leo watu wengi wamefurika kumsuburia Polepole halafu hajatokezea.

Kazingua big time hata kama ni kwa bahati mbaya.
Ni kweli kakuzingua mno mmbea mwandamizi.
 
Jamaa amenyooka sana leo🙌🏿🙌🏿🙌🏿
Polepole🙌🏿
Anasema vyama vingine ni project ya CCM.
Mpinzani halisi yupo gerezani.
 
Amka utakojoa ndotoni
 
Paschali
Pascal Mayalla ndiye Carlos The Jackal?
 
Hivi kuna jipya lililosemwa na Polepole, ambalo lilikuwa halifahamiki; au kwa vile limesemwa na Polepole?

Ubovu wa chama cha Mapinduzi haujaanza na Samia; ila Samia kaufanya uonekane waziwazi zaidi kwa udhaifu mkubwa zaidi wa uongozi alio nao.

CCM chini ya Kikwete ilikuwa ni mbovu vilevile; alipoingia Magufuli kafunika madonda yasionekane waziwazi, na chini ya Samia kila kitu kikawa nje nje.

Sasa mtu yeyote anayedai yeye ni mwana CCM, kama anavyodai Polepole, jambo la kumuuliza ni CCM ipi hasa ambayo yeye bado ni mwanachama wake mtiifu.
CCM halisi ilikwisha ondoka siku nyingi, enzi za Kikwete. Ina maana siku zote hizo hawa wana CCM walikuwa hawalijui hilo?
 
CCM kwa hili MCHUTAME...Uchaguzi usogezwe mbele..iteni Meza ya Mazungumzo ya dhati , mtupatie Katiba Mpya iliyo BORA na Tume huru kwelikweli ya Uchaguzi....

Jaji Mwambogele Wa Mahakama ya Rufaa na Mwenyekiti NEC "Huru" kulinda hadhi ya nchi, hadhi ya Mahakama na hadhi yako mwenyewe JIUZULU
 
Mkuu umenikumbusha kauli ya Nappe ilopelekea akatumbuliwa juzi kuhusu matokeo ya uchaguzi.

Je alikuwa mbele ya wakati?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…