Leo nimeacha chombo changu sehemu fulani, nikatembea kwa miguu kwa muda mrefu. Kwa kweli nilichokutana nacho njiani kimenifanya nitafakari sana kuhusu usalama wa watembea kwa miguu.
Nilipofika sehemu ya kuvuka barabara, nilihisi wasiwasi mkubwa. Pikipiki zinakuja kwa kasi, magari nayo yanapita kwa kasi, na wakati mwingine unalazimika kuvuka haraka huku ukitazama kulia na kushoto kwa hofu.
Cha kushangaza ni kwamba kwa muda mrefu nimekuwa nikisafiri kwa chombo, hivyo sikuwahi kuzingatia sana changamoto ambazo mtu anayesafiri kwa miguu anakutana nazo kila siku.
🦷Swali langu kwa wanaJF ni hili:🦷
👉 Kwa wale mnaotembea kwa miguu mara kwa mara, ni hatari gani kubwa mnazokutana nazo barabarani?
👉 Kuna maeneo ambayo mnaona ni hatari sana kuvuka?
👉 Tatizo kubwa ni kasi ya magari/pikipiki, kutokuwepo kwa pedestrian crossing, barabara mbovu, au madereva kutowajali watembea kwa miguu?
👉 Na wewe umewahi kukutana na tukio ambalo lilikufanya uogope kuvuka barabara?