Leo nimegundua kitu kimoja, kuvuka barabara si kitu kidogo!

Leo nimeacha chombo changu sehemu fulani, nikatembea kwa miguu kwa muda mrefu. Kwa kweli nilichokutana nacho njiani kimenifanya nitafakari sana kuhusu usalama wa watembea kwa miguu.

Nilipofika sehemu ya kuvuka barabara, nilihisi wasiwasi mkubwa. Pikipiki zinakuja kwa kasi, magari nayo yanapita kwa kasi, na wakati mwingine unalazimika kuvuka haraka huku ukitazama kulia na kushoto kwa hofu.

Cha kushangaza ni kwamba kwa muda mrefu nimekuwa nikisafiri kwa chombo, hivyo sikuwahi kuzingatia sana changamoto ambazo mtu anayesafiri kwa miguu anakutana nazo kila siku.

🦷Swali langu kwa wanaJF ni hili:🦷
👉 Kwa wale mnaotembea kwa miguu mara kwa mara, ni hatari gani kubwa mnazokutana nazo barabarani?
👉 Kuna maeneo ambayo mnaona ni hatari sana kuvuka?
👉 Tatizo kubwa ni kasi ya magari/pikipiki, kutokuwepo kwa pedestrian crossing, barabara mbovu, au madereva kutowajali watembea kwa miguu?
👉 Na wewe umewahi kukutana na tukio ambalo lilikufanya uogope kuvuka barabara?
Ni balaa, Kuna siku nilikuwa navuka barabara pale njia panda ya kunduchi ilikuwa usiku Sasa baada ya kuangalia kulia na kishoto nasikia mngurumo wa pikipiki Lakini siioni Ile navuka pikipiki hii hapa ipo Kasi sana kumbe haikuwasha taa.
 
Nasikia sikuhizi wachawi hawasafiri na ungo wanasema eti umepitwa na wakati eti wanatumia ufagio😁😁😁
 
Good move ya nini mie ,kuliko kijifanya mjuaji kuna siku niliomba traffic anisaidie kuvuka Road
Sahihi kabisa, kuna siku natoka dom nikaomba shabiby lnishushe karibu na Flomi pale… Uwiii kucheki hivi magari kibao barabarani na taa za magari zinamulika balaa mbona nilisimama hapo karibu dakika 10 nzima nikajuta bora ningeenda stand nirudi hata na boda maana sio mbali.

Nilisimama hadi boda wa upande wa pili wakagundua nimekwama ikabidi boda mmoja akavuka kwa mguu akanivusha, na hivi nilikuwa na begi isingewezekana kabisa.
 
Shida ni boda na bajaji, daladala huwa wako rough ila somehow wanaheshimu sheria. Kwenye taa wanasimama, kwenye zebra wanasimama maana pia wanajijua ni mtaji wa polisi.

Ila boda na bajaji vishandu ndo kipengele, hawana zebra crossing wala taa za barabarani. Hawana njia ya kupanda wala ya kushuka wao njia ya kupanda wanashuka na ya kushuka wanapanda, ukijifanya eti hii si ni one way acha niangalie kulia/kushoto pekee, aloo kitakuramba.

Kila barabara unaangalia kushoto na kulia then kushoto tena ndo uvuke.
 
Safi ujuaji mwingi useme wananiona ety navuka ndo mwisho wa habari huwa sipendi kukandiria jambo mimi
 
Hakuna barabara rahisi kuvuka kama hii....😋
20260628_142220.jpg
 
Shida ni boda na bajaji, daladala huwa wako rough ila somehow wanaheshimu sheria. Kwenye taa wanasimama, kwenye zebra wanasimama maana pia wanajijua ni mtaji wa polisi.

Ila boda na bajaji vishandu ndo kipengele, hawana zebra crossing wala taa za barabarani. Hawana njia ya kupanda wala ya kushuka wao njia ya kupanda wanashuka na ya kushuka wanapanda, ukijifanya eti hii si ni one way acha niangalie kulia/kushoto pekee, aloo kitakuramba.

Kila barabara unaangalia kushoto na kulia then kushoto tena ndo uvuke.
Hakuna kukadiria jambo always
 
So watembea kwa miguu inabidi tuwe makini mno kwenye zebra au wakati wa kuvuka ndo solutions
Umakini kwenye kuvuka barabara unahitajika sana ,madereva wengi wanapiga viroba ,wengi wanavuta mihadarati so wakiwa brbrn wanakuwa washawaka na hawapo makini ,sasa pata picha mvuka barabara asiye makini akakutana na dereva naye hayupo makini hapo lazima BUYU litokee.
 
Dua mingi
 
Siku zote kosa akili zote lakini ya kuvukia barabara isikukose. Hapa hata cjacheka vizur ndugu yangu. Yalinikuta cku moja hadi sikumaliza nilichokianza. Acheni tu akili nyingi mbaki na moja tu nawaambia
 
Ni balaa, Kuna siku nilikuwa navuka barabara pale njia panda ya kunduchi ilikuwa usiku Sasa baada ya kuangalia kulia na kishoto nasikia mngurumo wa pikipiki Lakini siioni Ile navuka pikipiki hii hapa ipo Kasi sana kumbe haikuwasha taa.
Mkuu ulitoka salama
 
Back
Top Bottom