Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 69,329
- 164,730
Ukweli ni kwamba barabara za Arusha mjini asilimia kubwa sana zina lami, hakuna barabara yanye kilomita mbili isiyo na lami, ni mitaa michache sana sana haina lami.We acha tu, leo mtu anakuja kudhiaki eti barabara ya lami nyembamba, kwani huko arusha kuna foleni gani? Watu wanataka hata barabara za changarawe wanaishia kuziona kwenye tv.
Hapa naongelea mjini kati...Makao mapya, kaloleni, stand ndogo na kubwa hadi clock tower kote huko lami.
Tatizo kubwa sasa ni masoko mfano kilombero ni soko kubwa sana lakini miundombinu mibovu, stand kubwa na ndogo hazifai tena.
Kumekuwa na mvutano miaka mingi sana kuhusu kujenga stand kubwa ya mabasi.
Eneo limetengwa nje ya jiji mbali sana lakini utekrlezaji hakuna.
Arusha ni ngumu sana, imetekwa na matajiri wakubwa kila kitu kinafanywa kwa maslahi yao.
Ni mji mgumu sana kuuongozo.
Wazee wa Kilimanjaro wana nguvu kubwa sana katika jiji hili.
Kuna wakati nawateyea wachaga sana lakini ni watu hatari sana linapokuja suala la maslahi yao