Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

kuna watu humu ni mazuzu hawawezi kuelewa ugonjwa wao ni uleuleee! zaidi ya ebora
 
Mbona hajawahi kutamka kuchukizwa kwake na ukwapuaji wa nyumba za Serikali ambao yeye alikuwa kinara akishirikiana na fisadi Mkapa? Au huwa anachukizwa tu na maovu yanayofanywa na wengine lakini yanayomhusu yeye kama ya uporaji wa nyumba za Serikali na ununuzi wa boti lililooza kwa shilingi bilioni 8 ambalo sasa hivi liko juu ya mawe, na ufisadi mkbwa wizara ya ujenzi ambapo yeye alikuwa kama Waziri hayamchukizi? Kama nayo yanamchukiza mbona anakwepa kuyazungumzia au kuchukua hatua muafaka?

 

yaani wewe jamaa ni mweupe kabisa kichwani, sasa hapa ndo umeandika nini?
 
ukimaanisha mume ni CCM na mke ni Tanzania?maana hoja yangu ni mali zirudi serikalini,wewe mbona kila tukisemacho sisi kibaya kwako,hapa haitetewi Chadema ndugu!
Kibaya zaidi, huyu bwana Lizaboni kila wakati anabebea bango mambo yanayojadiliwa na kuyahusisha na Uchadema tu. Hapa anatuonyesha kuwa uwezo wake wa kuelewa mambo ni zero ndiyo maana anashindwa kuchanganua mambo. Kama amekaririshwa na mtu/watu kuwa yupo kwa ajili ya kushambulia Chadema, ni vema watu wakawa wanamfahamisha mada zisizohusiaña na siasa
 
Daaah, ukada umekuzidi, unakulupuka sana.
 
Mheshimiwa Raisi tunaomba wakati tunasubiri ujenzi wa uwanja mpya wa mpira utakaojengwa Dodoma na Mfalme wa Morocco,waambie CCM warudishe Wizarani viwanja vya mipira walivyokumbatia nchi nzima.
Viwanja hivi vilijengwa na pesa za watanzania na siyo vya CCm.
Viwanja vinaharibika.
Wizara ianzishe WAKALA WA VIWANJA VYA MICHEZO ili hivi viwanja vikasimamiwa na hiyo Wakala.
 
Kwa muda sasa tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, kitu kimoja hakijawekwa bayana, nalo ni viwanja vya mpira wa miguu vinavyomlikiwa na CCM. Kati ya viwanja hivi, vingi vina hali ngumu kwa maana kuchakaa na kushindwa kuhudumiwa au kuendelezwa kuwa katika hali bora.

Viwanja vingi vimechakaa mno kiasi cha kuwa vichaka, mfano kiwanja cha mpira cha CCM Musoma Manispaa. Kiwanja hiki kimejaa nyasi ndefu na ubora wake haupo kabisa. Ni kiwanja kinachotegemewa na Hamashauri karibu 8 za mkoa huu wa Mara. Tatizo kubwa la uwanja huu kuwa katika hali mbaya ni urasimu uliopo wa wamiliki wake ambao ni CCM. Uwanja unafanyiwa usafi wa kufyekwa mara moja zinapokuweko michezo ya UMISETA na UMITASHUMITA kama hali ya kubadilishana badala ya kulipia kwa fedha wao hufanya usafi.

Kama ilivyo kwa uwanja huu, ushauri wangu ni kuwa CCM imeshindwa kabisa kuendeleza viwanja inavyovimiliki, ni bora serikali ivitaifishe ili viweze kutumika kwa ajili ya kuingiza hela kwenye halmashauri husika. Pia tendo hili litasaidia kuboresha hali na ubora wa viwanja hivi na kutumika wakati wote.
 
Kama Rais wetu alivyoona mbali kwa kuirudisha serikalini shule ya CCM kule Kagera, afanye hivyohivyo kwa kuvirudisha TFF viwanja vya mpira wa miguu vyote au baadhi ambavyo viko chini ya CCM ili CCM. Hatutakuwa na cha kumpa bali tutampa zawadi ya kumpigia makofi mawilimawili na kukenua.
 
Muda mrefu sasa serikali haitaki kutaifisha viwanja vya Mpira ambavyo viliporwa na chama cha mapinduzi. Viwanja hivi vimekua sababu ya kudorola kwa michezo hapa nchini kwa sababu haviendelezwi.

Na baada ya kuvitaifisha tunaomba kuundwe wakala wa viwanja vya michezo ili kuviendeleza na kuvisimamia.

Kama alivyo taifisha ile shule ilikarabatiwa na serikali kwa fedha za maafa, tunaomba moyo huo huo utumike kuvirudisha viwanja hivi.
 
Naunga mkono hoja...na sasa bila kusita serikali ianze kufikiria kuwa na viwanja vya kisasa kwenye kanda zote za Tanzania na ikiwezekana tuombe haraka iwezekanavyo kuandaa kombe la Africa kwa mara ya kwanza , ndani ya utawala wa awamu ya tano..inawezekana tukiamua.."Hapa kazi tu"
 
kwa sababu ccm wamevihodhi lakini havitumiki. cha msingi ni kutaifisha, hapo ndipo nitaona tunakamanda ikulu
 
Unawazo zuri, lakini kitu cha ajabu ni pale mfumo wa vyama vingi ulivyoshindwa kutofautisha serikali na ccm. Kama hujaelewa ni hivi kiongozi wa chama wa ccm ananguvu kuliko mkurugenzi wa serikali.Mpaka sasa hatusongi mbele maana ccm bado haijajisimamia ila inaegemea serikali,ndiyo maana hivyo viwanja vilivyojengwa na watanzania vilitaifishwa na kupewa hati miliki ya ccm.
 
Hiyo ndio kero yako?Subiri chadema wakiingia madarakani mwaka 2090
 
kwa sababu ccm wamevihodhi lakini havitumiki. cha msingi ni kutaifisha, hapo ndipo nitaona tunakamanda ikulu
Kwanza kiukweli hivyo viwanja si vya ccm...vilijengwa na kwa nguvu za wananchi wote wa Tanzania...ni wakati mwafaka sasa vikarudi serikali vikajengwa upya
 
Kuna ukweli na mwenye macho haambiwi tizama,Hakuna investments ya CCM katika viwanja hivyo tokea kufunguliwa vyama vingi zaidi ya miaka 20.
Ni wazi CCM haiwezi kuviimarisha,au ni kwakuwa enzi ya chama kimmoja muhudumu alikuwa serikali na mmiliki alikuwa ni wananchi na serikali yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…