CCM wananyang'anya watu maeneo yao kupitia mgongo wa serikali kujitaftia kura 2020,Wengine kesi ziko mahakamani lakini wao hawajali, wanalipa visasi kutuliza makovu yao ya kisiasa.
Sasa nao warudishe viwanja vyote wanaomiliki ambayo kiasili na kiuhalali ni Mali za uuma. Vipo viwanja vingi vya mpira wa miguu wanamiliki ccm vinajiotea nyasi havijaendelezwa.
CCM wanasahau kua hata Ofisi yao ya Lumumba wanayomiliki ilikua Ofisi ya TANU ambayo ilijengwa kwa jasho la watanzania wote, kiuhalali sio ofisi yao lakini wanajimilikisha kwa mambavu.
Ukifuatilia Yale maeneo yote upanga ya umoja wa vijana yanayojengwa maghorofa chanzo cha umiliki ni miikono ya umma na sio Mali ya chama.
Tuseme kua iko siku haya wanayoyafanya yatawaliza, ni suala la muda tu.