Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

Lini Viwanja vinavyomilikiwa na CCM vitakuwa chini ya umiliki wa Serikali Kuu au Halmashauri husika?

wewe unachekesha kweli. Ccm ni ya wananchi na si kama ilivyo kwa mtei na cdm. Kama unataka mali kwani ccm imekunyima kuwa mwanachama umekimbia mwenyewe, ccm itabaki kuwa ya wananchi maishani, nenda kaulize zile mia mia mlikuwa mnachangia mboye aruke na chopa mkisema mnajenga chama, ccm milele itabakia kuwa ya wananchi. Utakufa utaiacha, wananchi wataendelea kuikuza, ccm daima chama cha wananchi.

Lazima ujaribu kuvuruga hoja kwa buku 7,kama chama cha wananchi mbona kuna chama kinaitwa chama cha wananchi wagaieni nao,hulka ya ccm ni wizi na dhuluma,kumbuka epa,meremeta,rada mabilioni ya uswisi,mmewadhulumu wazee wa jumuia ya afrika mashariki hadi wanakufa pale relwe,hamna hata huruma kweli ccm janga la kitaifa
 
Hilo la CCM kubaki na mali zilizojengwa na wananchi ni jambo linaloniuma sana.kuna jamaa alifungua kesi ya hili jambo lakini mahakama iliamua hovyo kwa sababu baada ya jamaa kufungua kesi aliikacha na kupotea, sasa kwa utaratibu wa kisheria mdai akikimbia kesi yake inabidi ifutwe, sasa mahakama sijui kuifurahisha CCM ikaendesha kesi bila mdai na kuipa ushindi CCM. Lakini nina matumaini ipo siku hii hukumu itatenguliwa tu kwa vile ilikosewa kisheria. Kenya jengo la Nyayo lilirudishwa serikalini baada KANU kuangukia pua.
 
Akili za kuambiwa hizi ni shida. Na huko bavicha/chadema ziko nyingi kweli, kwanini hamtumii hata akili kidogo tu
nyie wachaga??? MALI ZAKO si unazo mwenyewe au?? Au unatangaza biashara kistaili flani???
Acha ukabila ww haujengi?
 
Nimejaribu kufikiri jinsi ccm ilivyo zulumu kibabe mali zetu zikiwemo viwanja vya mpira kama ccm kirumba mali hizi tulichangishana enzi zile za chama kimoja,na sasa ni wengi tu si wafuasi tena wa vyama vya siasa na ccm kwa kutenda haki nashauri rudisheni serekalini mali zote.

Mke mdogo akiolewa na kukuta mke mkubwa na wanawe wamechuma mali hizo mali atazidai kuwa ni zake?
Miaka 22 hamjachuma zenu? Hata ofc tu hamna. mnaishi katika majengo ya viongozi.
 
Mke mdogo akiolewa na kukuta mke mkubwa na wanawe wamechuma mali hizo mali atazidai kuwa ni zake?
Miaka 22 hamjachuma zenu? Hata ofc tu hamna. mnaishi katika majengo ya viongozi.

Uwezo finyu wa fikira kijana ongeza nyama kwenye bongo
 
quote_icon.png
By Uhuru Odinga
Wana siku 723 zimebakia mali za umma watarudisha tu
Siku tatu alizopewa rais ili afute kauli yake hazijaisha? hizi 723 zitafika kweli?
 
Nadhani wote ni waelewa kuhusu mfumo wa chama kimoja ambao ulikua unakipa mamlaka makubwa sana chama tawala na moja ya kosa kubwa tulilolifanya kipindi tunaingia katika mfumo wa vyama vingi ni kuruhusu mali zilizokuwa chini ya serekali kupitia CCM kubaki mikononi mwa chama cha CCM nadhani sasa huu ni muda muda muwafaka kwa serekali kurudisha viwanja vya michezo mikononi mwa wanannchi kupitia shirikisho la mpira Tanzania (TFF ), Baadhi ya viwanja hivyo ni ccm kilumba, ccm mkwakwani, majimaji songea, sokoine mbeya na vinginenyo ambavyo havijatajwa . Tunaomba busara itumike kwa viongozi wa ccm kuvirudisha viwanja hivyo ili kuinua mpira wetu Tanzania
 
Ngoja waje, jiandae kurushiwa mawe.

Tiba
 
Hili walishamaliza walisema ukimchangua mtu kuoa mke ni wake peke yake, viwanja vingepewa majina ya halmashauri vingekuwa vya umma. Kwa hili tuwasameheni tu wachukue
 
Napata tabu kidogo binafsi naomba kueleweshwa juu ya nadhalia ambayo wanaccm wamejijengea ya kujimilikisha Mali za umma.
Mfano mzuri eti viwanja vyote vya michezo kasoro vile vya Uhuru na taifa ni vya ccm. Viwanja kama mkwakwani, kirumba, jamhuri, Shekh amri abeid na vingine vyote Tanzania. Ina maana ccm ilitoa pesa yake kujenga viwanja hivi ama kuna siri gani nyuma ya pazia?
Tukosoane Kwa staha.
 
Ccm Wamepora Mali Za Wanainchi, Huo Ni Ukweli Usiopngka
 
Hata haijawahi na kuwa na afisi zake zote wamepora CCM ni washamba kama mtu mmoja kutoka Kigoma wizi wizi tu mpaka siku ya kiama chao.
 
Back
Top Bottom