LIssu: Bandari zote bara, DP World kauziwa

LIssu: Bandari zote bara, DP World kauziwa

Mkuu tunayasikia lkn mimi hili la kuuzwa silioni huenda kwasababu, kama inavyodaiwa, mimi ni Mzenji na Mzenji kwa mtazamo wa wanajamii forum wengi ni Mwarabu, kwaivyo nikisema nitaambiwa nawatetea Waarabu!

..utambulisho wa Uzanzibari unafifisha Utanzania wenu.

..wakati Watanganyika wakijitambulisha kama Watanzania ndugu zao wa Zanzibar wamedumisha utambulisho wao wa kabla ya muungano.

..kuhusu Uarabu kuna suala la ukoloni na biashara ya utumwa. Sasa tatizo ni kwamba Waarabu walizaliana na Waafrika na uzao huo umeendelea kuwepo nchi.

..Mazingira hayo ndio yamesababisha hisia za " uarabu " vs Uafrika / Utanzania. Wazungu wangezaliana na Waafrika kungekuwa na hisia za " uzungu."

..Wazanzibari kuwatetea Waarabu ni jambo la kawaida kibinadamu. Wanawatetea kwasababu ya kuwa na vinasaba nao. Ni sawasawa na sisi Watanganyika tunapotetea Waafrika wenzetu kila wanaposhambuliwa au kunyanyaswa.
 
Kwamba rais ni mzanzibari hiyo siyo hoja ya Lissu labda kama unataka kutulazimisha tu ndugu.

Hoja ni kuwa bandari zimeuzwa na aliyeziuza anautambulisho wake kutokea Zanzibar kama Butiama, Lupaso, Msoga au Chato.

Hoja haikimbiwi. Hoja hujibiwa kwa hoja. Watu Gani nyie mliopanga kukimbia hoja Ili kulazimisha humo zenu?
Rejea kauli ya Mbowe na hii ya Lissu then kumbuka Uzanzibar si sawa Lupaso Uzanzibari ni utaifa
 
Mh [emoji848] ngoja manguli wa mikataba waje akina.. Lord denning Faizafoxy covax GUSSIE choiceVariable HIMARS tuone wanadadavua vp kisheria!!
Mbona unawadhihaki watu. Yaani Faiza, Gussie, HIMARS, ChoiceVariable, Covax, wawe manguli wa sheria!! Maana ya nguli itakuwa imebadilika.
 
Nami cjaelewa kwann hawaja show up ili kuleta hoja za kisheria kuhusu suala la DP world ili wakina LISSU tuwaone ni wababaifu!!!
Ni kazi sana kutetea uovu kutumia sheria. Ndiyo maana wanabakia kupiga kelele tu, mara oh DP ni kampuni kubwa, mara oh DP wamewekeza nchi nyingi. So what?

Ngoja Lisu aendelee kutoa elimu ili maandamano yakianza, watu wajue kwa nini wanaandamana.
 
Rejea kauli ya Mbowe na hii ya Lissu then kumbuka Uzanzibar si sawa Lupaso Uzanzibari ni utaifa

Uzanzibari uliopo hapa ni sawa na Lupaso, Msoga, Butiama au Chato.

Ndiyo maana walipovunjiwa nyumba kibamba lakini si Mwanza Kwa sababu alizozitoa bwana yule wengi tuli hamaki!

Jibuni hoja siyo kuzikimbia hoja.
 
HIMARS kala ban baada ya jana kuzidiwa kwa hoja na kuanza kurusha lugha zisizofaa hapa jukwaani.DPW imemfanya awe kama kichaa kwa kuitetea huku akitukana matusi hovyo,pengine akirudi atakuwa kajifunza jinsi ya kupangua hoja za wadau wanaopinga mkataba.
HIMARS hana uwezo wa kupangua hoja.
 
Ni kazi sana kutetea uovu kutumia sheria. Ndiyo maana wanabakia kupiga kelele tu, mara oh DP ni kampuni kubwa, mara oh DP wamewekeza nchi nyingi. So what?

Ngoja Lisu aendelee kutoa elimu ili maandamano yakianza, watu wajue kwa nini wanaandamana.
Hakika ✔️
 
Mbona unawadhihaki watu. Yaani Faiza, Gussie, HIMARS, ChoiceVariable, Covax, wawe manguli wa sheria!! Maana ya nguli itakuwa imebadilika.
Mkuu nadhan unawaelewa humu wao ndio husimama na kuwatetea DP world kila cku!! Maybe wao ndio manguli wa mikataba.
 
Mbona nyepesi ni hoja zako? Za Lissu ziko wazi:

1. Je, rais Hana mamlaka makubwa mno kwa mujibu wa Katiba?
2. Je, bandari zote za bara kakabidhiwa DP World Kwa mujibu wa makubaliano yaliyopo?
3. Je, kuna bandari yoyote ya Zanzibar kwenye makubaliano haya?
4. Je, rais ni mzaliwa wa Zanzibar?
5. Je, maslahi tokea DP World hayawahusu wazanzibari?

Ungejikita kwenye hoja zake hoja kwa hoja hudhani kuwa ungejitendea haki zaidi?

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
1-Hata Mwalimu Nyerere alishawahi kusema kwamba madaraka aliyopewa raisi na katiba yetu hii ni makubwa kama akipatikana raisi kichaa ataharibu nchi, lakini na yeye ndiyo alikuwa nayo.
2-Huwenda kukawa na mapendekezo hayo ya DP World kupewa kuendesha bandari zote za bara kwani ndizo zenye manufaa na faida kwa muwekezaji, bandari za Zanzibar hazina faida kwa uwekezaji kwani ukiwa na bandari za bara unaweza ukahudumia mpaka nchi za jirani, ndiyo maana hata njia za train zimetengenezwa zitakazo unganisha Tanzania bara na nchi za jirani.
3-Kwenye uwekezaji wa faida bandari za Zanzibar hazina faida sana ukilinganisha na za Bara hasa Dar.
4-Raisi ni mtanzania aliyezaliwa Zanzibar.
5-Maslahi kutoka DPW yatahusu Tanzania kwa ujumla ikiwa TZ Bara ni mnufaika mkubwa.
 
Uzanzibari uliopo hapa ni sawa na Lupaso, Msoga, Butiama au Chato.

Ndiyo maana walipovunjiwa nyumba kibamba lakini si Mwanza Kwa sababu alizozitoa bwana yule wengi tuli hamaki!

Jibuni hoja siyo k

1-Hata Mwalimu Nyerere alishawahi kusema kwamba madaraka aliyopewa raisi na katiba yetu hii ni makubwa kama akipatikana raisi kichaa ataharibu nchi, lakini na yeye ndiyo alikuwa nayo.
2-Huwenda kukawa na mapendekezo hayo ya DP World kupewa kuendesha bandari zote za bara kwani ndizo zenye manufaa na faida kwa muwekezaji, bandari za Zanzibar hazina faida kwa uwekezaji kwani ukiwa na bandari za bara unaweza ukahudumia mpaka nchi za jirani, ndiyo maana hata njia za train zimetengenezwa zitakazo unganisha Tanzania bara na nchi za jirani.
3-Kwenye uwekezaji wa faida bandari za Zanzibar hazina faida sana ukilinganisha na za Bara hasa Dar.
4-Raisi ni mtanzania aliyezaliwa Zanzibar.
5-Maslahi kutoka DPW yatahusu Tanzania kwa ujumla ikiwa TZ Bara ni mnufaika mkubwa.
Sio kwamba bandari za Zanzibar hazina faida ila Rais Samia anaongoza nchi ipi?
Hawezi kuingilia mamlaka ya Zanzibar na hilo Lissu anajua kama mwanasheria. Sasa anapotokea mtu akasema maneno lazima upime kama ni mzima kiakili.
Rais anatumikia Jamhuri ya Muungano haijalishi anatoka upande gani.
 
Hatujaacha kutambua au kurejea alikozaliwa rais na hakuna jipya hapo. Hoja ya Lissu so alikozaliwa rais.

Bitiama, Lupaso, Msoga, Chato nk kupo kwenye rekodi tunakutumbua na haijawahi kuwa taabu.

Zingatia teuzi zilipojikita Kanda ya ziwa tulisema. Hapa tunasema aliyeuza bandari za bara ni mzanzibari labda kama wewe unadhani ni mtu wa bara?
Hata hao viongozi wa Chadema walipozaliwa hamna bandari kila mtu arudi mkoa wake.. Bandari ni za watu wa pwani si mnaleta ubaguzi.
 
Hoja za Dk. Slaa, LIssu, Prof. Shivji, wakili msomi Mwabukusi na wa namna hiyo siyo za kuingia kichwa kichwa. Waliko watakuwa wanachungulia na kujisemea hiiiiiiiiiii:

View attachment 2677059

Kama mapanya tu!
Wakija wataanza kuhamisha magori. Kushambulia pesonality badala ya hoja. hao wanakuja subiri
 
Sio kwamba bandari za Zanzibar hazina faida ila Rais Samia anaongoza nchi ipi?
Hawezi kuingilia mamlaka ya Zanzibar na hilo Lissu anajua kama mwanasheria. Sasa anapotokea mtu akasema maneno lazima upime kama ni mzima kiakili.
Rais anatumikia Jamhuri ya Muungano haijalishi anatoka upande gani.
Bahari ni jambo la muungano kasome katiba, hapo kuna kosa la kuvunja katiba live.
 
Hapa ndio najiuliza hoja ya Uzanzibar inakuja leo kwa kuwa tu rais ni mzanzibar au?
Maana kuna mambo mengi Serikali inaingia mikataba na hayasemwi kama huyu ni mzazibar au mtanganyika
Point. ! Na hiyo ndio inayopelekea pia baadhi ya watu kufanya conclution ya kwamba hii yote ni Udini Udini tu !!

Ni vyema tukatumia majina na vyeo vya watu tunaotaka ama kuwakosoa ama kuwasifu badala ya kutumia kabila au nasaba ya mtu au kule watokako !!

Baada ya muungano wa 1964 sisi sote tunatambulika kama Watanzania !! Haijalishi wewe ni mzanzibari au ni mtanganyika by origin !
 
Back
Top Bottom