- Thread starter
- #81
1-Hata Mwalimu Nyerere alishawahi kusema kwamba madaraka aliyopewa raisi na katiba yetu hii ni makubwa kama akipatikana raisi kichaa ataharibu nchi, lakini na yeye ndiyo alikuwa nayo.
2-Huwenda kukawa na mapendekezo hayo ya DP World kupewa kuendesha bandari zote za bara kwani ndizo zenye manufaa na faida kwa muwekezaji, bandari za Zanzibar hazina faida kwa uwekezaji kwani ukiwa na bandari za bara unaweza ukahudumia mpaka nchi za jirani, ndiyo maana hata njia za train zimetengenezwa zitakazo unganisha Tanzania bara na nchi za jirani.
3-Kwenye uwekezaji wa faida bandari za Zanzibar hazina faida sana ukilinganisha na za Bara hasa Dar.
4-Raisi ni mtanzania aliyezaliwa Zanzibar.
5-Maslahi kutoka DPW yatahusu Tanzania kwa ujumla ikiwa TZ Bara ni mnufaika mkubwa.
1. Ninakusoma kuwa #1 unakubaliana na Lissu kuwa hili ni hatari. Hili halina ubishi. Tuna Mungu mtu ikulu Kwa jina la Rais. Tulipo kaingia mkataba na DP World bila kutushirikisha.
2. #2 huna uhakika na yaliyomo, hivyo ni sawa kuchukua akisemacho Lissu kuwa mkataba umelalia kuwapa bandari zote za bara.
Ila hapa kwenye faida pana ukakasi. Bandari zote za kemondo bay, nansio ukerewe, ziwa Tanganyika, Nyasa, rukwa, Victoria huko ziwe na faida zaidi ila za Zanzibar?!
Kama ndivyo, kumbe wewe utaturejesha kwenye kuhoji huu muungano nini hasa faida yake?
3. #3 Haina tofauti kubwa na #2. Bado waongelea uwezekano wa tofauti za faida kwenye bandari bara na Zanzibar. La msingi kumbe litakuwa nini hasa faida ya muungano huu?
4. Rais ni mtanzania aliyezaliwa Zanzibar hata Lissu anasema hivyo. Kwamba hilo halina ubishi. Hilo ni kama Magufuli na Chato au Kanda ya ziwa. Hilo ni historical.
Ukakasi unakuja kunapokuwa na kuvutia nyumbani hapo hatuwezi kukaa kimya. Kumbuka daraja ziwa Victoria au Chato International airport.
5. Maslahi yatahusu Tanzania nzima na bara ni mnufaika zaidi. Hili linabishaniwa. Kwamba kupanga ni kuchagua na serikali ni mwakilishi tu, kulikoni kutaka kutulazimisha kama wana nzengo hatutaki?
LIssu anasema wenye nchi wananchi tusikilizwe. Zingatia msingi wa hoja:
"Walio wengi hawautaki mkataba huu."
Ni hayo tu ndugu mjumbe.