LIssu: Bandari zote bara, DP World kauziwa

Siasa za majitaka?

Muulize zimeuzwa shilingi ngapi? Hela imeimgizwa wapi? Akuonyeshe na risiti
 
Mkuu msikilize mheshimiwa ally possi tujaribu kuangalia kajibu kilichoulizwa

Anayaita makubaliano ya kisiasa. Anatumia neno makubaliano na mkataba interchangeably kuuhusu. Anakiri rais kausaini kwa kumpa Mbarawa idhini ya kuusaini kwa niaba yake. Anakiri kuwa huu ndiyo utakuwa msingi wa mingine ya utekelezaji itakayofuata.

Hoja za msingi zinazozozaniwa ziko wazi:

1. Je, kuna kikomo kwenye mkataba huu?
2. Je, ni mkataba au ni makubaliano?
3. Je, Kuna tofauti baina ya makubaliano na mkataba?
4. Je, ni kuzihusu bandari zetu zote za bara?
5. Je, bandari za Zenji huko, hazihusiki?
6. Je, wananchi wameshirikishwa?
7. Je, ni kweli DP World hawana wajibu ila Tanzania kama nchi kwenye mkataba huu?
8. Je, mkataba huu ni wa hovyo?
9. Nk nk?

Kwa hakika hakuna jipya kutoka kwa mlamba asali huyu!

Nionavyo huyu kaja kamwongezea wakili msomi Mwabukusi ammunitions zaidi badala ya kuleta ufafanuzi kwenye lolote.

Kwa hakika wito wa Mwabukusi unaishi:

Wakili Mwakabusi atoa wito kwa Spika wa Bunge na Mbarawa wajiuzulu kutokana na mkataba wa DPW

Ni heri wangeuridhia tu mapema zaidi kuliko baadaye.
 
Kwani Tanganyika munayo serikali tunachojua sisi ni Serikali ya Muungano hata Mzanzibar anaongoza sasa kama mkataba ni wa kuiuza bandari basi itauzwa bandari ya Jamhuri ya Muungano na sio Tanganyika someni hio IGA wapi imetajwa Tanganyika.

Rais Samia ana mamlaka kwenye Serikali ya Muungano na sio Serikali ya Zanzibar sasa ukitaka ajumuishe bandari ya Zanzibar atajumuishaje kitu hana mamlaka nacho yaani princple ndogo kama hii huyo mwanasheria wrnu inamshinda.

Kwa hiyo kwa uelewa wako ewe nguli, Zanzibar hawayahitaji marupurupu ya uwekezaji huu kupitia DP World kupitia bandari zao, ila kupitia kwenye mwamvuli wa bandari za Tanzania tu ambako zao hazihusiki?!

Kwamba kumbe hii yako sasa itakuwa ndiyo akili au matope?
 
Kwani Tanganyika munayo serikali tunachojua sisi ni Serikali ya Muungano hata Mzanzibar anaongoza sasa kama mkataba ni wa kuiuza bandari basi itauzwa bandari ya Jamhuri ya Muungano na sio Tanganyika someni hio IGA wapi imetajwa Tanganyika.

Rais Samia ana mamlaka kwenye Serikali ya Muungano na sio Serikali ya Zanzibar sasa ukitaka ajumuishe bandari ya Zanzibar atajumuishaje kitu hana mamlaka nacho yaani princple ndogo kama hii huyo mwanasheria wrnu inamshinda.

..Tanganyika tumedhulumiwa serikali yetu.

..Na lawama kwamba Wazanzibari wanauza rasilimali zetu chanzo ni Tanganyika kunyimwa serikali yake.

..Mimi nilitegemea Wazanzibari mtuunge mkono Watanganyika ktk kupinga dhuluma dhidi yetu.

..Mtuunge mkono tunapodai kuundwa kwa serikali ya Tanganyika, na muungano wenye HAKI.
 
Yaan wanatak Tanganyika iwe Dubai
 
..Tanganyika tumedhulumiwa serikali yetu.

..Na lawama kwamba Wazanzibari wanauza rasilimali zetu chanzo ni Tanganyika kunyimwa serikali yake.

..Mimi nilitegemea Wazanzibari mtuunge mkono Watanganyika ktk kupinga dhuluma dhidi yetu.

..Mtuunge mkono tunapodai kuundwa kwa serikali ya Tanganyika, na muungano wenye HAKI.

Zawadini mwaiona je hoja hii ya kuungana mikono kwenye kupigania haki, ukizingatia sote tu wahanga tu wa mazingira?
 
Hoja za Dk. Slaa, LIssu, Prof. Shivji, wakili msomi Mwabukusi na wa namna hiyo siyo za kuingia kichwa kichwa. Waliko watakuwa wanachungulia na kujisemea hiiiiiiiiiii:

View attachment 2677059

Kama mapanya tu!
Mawakili wetu wamekua kama madalali tu Siku hizi

Wanaibuka na hoja na kusema nayo

Wabongo hamjifunzi
 
Mawasiliano ndiyo kina nani mjomba?
Mawakili jombaa

Wapo tu wanasubiri hit single na wao wanakwenda kupiga remix

Haohao kwshokutwa unasikia wanasifia waichokikandya

Ukiondoa wasemaji wa vilabu …. Wasomi wetu wengine wote tumekua kama mzee Mpili
 
Hao unaowaita mawakili kumbe nilikuwa nawasoma wapi jomba?

Kama ni kina Mwabukusi, Lissu, Slaa, Shivji, Lugemeleza au hawa waliotimba mahakamani mithili ya nyati aliyejeruhiwa kuwaweka majaribuni kina Samia, Tulia, Mbarawa au chawa wao, hao siyo size yako. Kwani wewe ni kipi ulichofanya mjomba?

Ukweli wa mambo ni kuWa, hao wanethubutu! Kumbuka yapo makundi mawili tu:

Screenshot_20230629-071736.jpg

Katika hayo wewe uko na ustaadh Mwaipopo?

Hiiiiiiiiiii bagosha!
 
..Tanganyika tumedhulumiwa serikali yetu.

..Na lawama kwamba Wazanzibari wanauza rasilimali zetu chanzo ni Tanganyika kunyimwa serikali yake.

..Mimi nilitegemea Wazanzibari mtuunge mkono Watanganyika ktk kupinga dhuluma dhidi yetu.

..Mtuunge mkono tunapodai kuundwa kwa serikali ya Tanganyika, na muungano wenye HAKI.
Katika hili sisi tulifanya ila ni nyinyi Watanganyika mulioshikilia mfumo uliopo kwa nia ya 'kuidhibiti' Zanzbar.

Rejea maneno ya Lukuvi kule kanisani, ambaye ni Mtanganyika halafu rejea msimamo wa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kwenye bunge la katiba mwaka 2014 ambaye ni Mzanzibari.
 
Zawadini mwaiona je hoja hii ya kuungana mikono kwenye kupigania haki, ukizingatia sote tu wahanga tu wa mazingira?
Mkuu brazaj; hili tumelifanya zamani ila tatizo, kwa maoni yangu, ni nyinyi. Rejea mchango wangu kwa jokakuu mchango wake namba 167 kuhusu hili.
 
Katika hili sisi tulifanya ila ni nyinyi Watanganyika mulioshikilia mfumo uliopo kwa nia ya 'kuidhibiti' Zanzbar.

Rejea maneno ya Lukuvi kule kanisani, ambaye ni Mtanganyika halafu rejea msimamo wa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar kwenye bunge la katiba mwaka 2014 ambaye ni Mzanzibari.

Yaliyopita si ndwele yaliyokuwa mapungufu yetu tuyasahau. Kutokea hapa tuwekeze kwenye muungano wa haki sawa kwa wote kwa kuzingatia maoni ya wengi.

Pana taabu gani hapo ndugu zetu?
 
Hao unaowaita mawakili kumbe nilikuwa nawasoma wapi jomba?

Kama ni kina Mwabukusi, Lissu, Slaa, Shivji, Lugemeleza au hawa waliotimba mahakamani mithili ya nyati aliyejeruhiwa kuwaweka majaribuni kina Samia, Tulia, Mbarawa au chawa wao, hao siyo size yako. Kwani wewe ni kipi ulichofanya mjomba?

Ukweli wa mambo ni kuWa, hao wanethubutu! Kumbuka yapo makundi mawili tu:

View attachment 2677944

Katika hayo wewe uko na ustaadh Mwaipopo?

Hiiiiiiiiiii bagosha!
Jombaa mbona wewe mwenyewe umeharibu

Sasa post huku ina mwijaku na huku ina shivji…. Huoni umewaweka wewe kwenye kapu?

Nilidhani utaweka Mawakili wa serikali waliohusika n kushindanisha na akina lissu

Umetukosea sana aisee
 
Zawadini mwaiona je hoja hii ya kuungana mikono kwenye kupigania haki, ukizingatia sote tu wahanga tu wa mazingira?
Kwa hili hatuwezi kukuungeni mkono kwa sababu nyinyi mnajiona sio wahanga wa mfumo wa muungano hadi leo katokea Rais mzanzibar ndio mnashtuka wakati sisi tuliyaona zamani tena tukakataa mfumo huu mbele ya Nyerere.
Rejea kitabu cha mzee Jumbe anathibitisha wazi wazi kwamba Zanzibar haijawahi kuridhia mkataba wa Muungano.
 
Kusema twasema leo kwa kuwa katokea rais mzanzibari, itakuwa kutokututendea haki mkuu.

Kwani kwa kauli yako hii mbona Mzee Mwinyi aliwahi kuwa rais na hatukupiga kelele hizi?
 
Back
Top Bottom