Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ikiondoka kwenye misingi iliyonifanya nijiunge nacho, nitaondoka. CHADEMA siyo mama yangu wala dini yangu

Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ikiondoka kwenye misingi iliyonifanya nijiunge nacho, nitaondoka. CHADEMA siyo mama yangu wala dini yangu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Ndio anaondoka hivyo, amejaribu kukinyofoa chama kutoka mfukoni mwa mtu ameshindwa. Sijui huyo jamaa mfuko wake ni mrefu kiasi gani.
 
Safi

Aliondoka Kaborou itakuwa Tundu Antipas Lisu wa NCCR Mageuzi? 😄😄
Dr. Aman Warid Kabouru, msomi mzaliwa wa ujiji , ambaye alishiriki kuianzisha chadema halafu lissu impact yake Kwa sasa ni ndogo na uungwaji mkono ni mdogo, aliondoka zitto enzi akiwa wamoto ije kua lissu ambae Kwa sasa hana ushawishi
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA- Bara, Tundu Lissu amsema iwacha CHADEMA itaacha misingi yake ailiyomfanya ajiunge na chama hicho basi ataondoka katika chama hicho na sio dhambi kufanya kuvyo kwani Chama cha Siasa sio mama yake wa dini yake

Akizungumza kupitia Mtandao wa Clubhouse amesema "Mwalimu Nyerere katika mojawapo ya kauli zake nyingi aliwahi kusema kwamba CCM siyo mama yangu na ikiacha misingi yake nitaiacha, ilikuwa kauli ya Mwalimu kuhusu chama alichokianzisha, kwa hiyo unataka mimi niseme kwa mazingira yoyote yale vyovyote itakavyokuwa sitahama CHADEMA? ni mama yangu?"

Ameongeza "Niliingia CHADEMA miaka 20 iliyopita na nimekuwa hapa miaka yote hii na Mungu anirehemu niendelee kuwa CHADEMA wakati nayo ikiendelea kuishi, lakini CHADEMA siyo dini na siyo mama yangu, ni chama cha siasa kikiondoka kwenye misingi yake iliyonipeleka nikajiunga nacho nitaondoka, nitakuwa sina sababu ya kubaki na hiyo siyo dhambi kwa sababu siyo dini na siyo mama yangu nikitumia maneno ya Mwalimu, ni chama cha siasa, vyama vya siasa huja na kuondoka, sisi binadamu tunakuja na kuondoka"

Jembe katika ubora wake:

Kujaribu kuwazodoa kina Mandela, Nyerere, Lissu, nk ni kujidhalilisha!

Wenye wivu hapo ni full kufura!

Viva TAL, ulipo tupo!
 
Usaliti unaumiza sana hasa kwa wapenda haki lakini katika maisha ya siasa Usaliti ni kawaida sana hivyo ni muhimu kufahamiana, kuchukuliana na kuvumiliana.

Wakati Lisu anasaliti watanzania kwa Acacia ulishangilia. Tulieni dawa iwaingie
 
Alichokiongea Lissu ndo uhalisia wa maisha ulivyo, vinginevyo utaitwa unafki.
Watu mnahofu na nini? Nothing is gonna change. Nafasi ya makamu mwenyekiti itashindaniwa lakini hatimaye Lisu ataibuka kidedea. Halikadhalika nafasi ya mwenyekiti this time itashindaniwa. Lakini bado jemedari mboee atashika hatamu, mark this note!
 
Binafsi naona Chadema itakuwa nzuri sana ikabaki na viongozi wenye msimamo wa kati na sio viongozi ambao wao kila kitu kinachofanywa na chama tawala kwao ni kibaya. Huwa namuona Mbowe ni kiongozi mzuri na mwenye busara nyingi mno hii inapelekea watu wengi wenye kutofautiana kimtazamo huko chama tawala kuona chadema kama ndio kimbilio lao. Tatizo linakuja kwa wale top wa chadema ambao ndoto zao ni kugombea urasi haijalishi wako popular au laah! wanamuona Mbowe ni kikwazo kwao kutimiza adhma zao, hapo ndipo Mbowe anaonekana mbaya. Kiuhalisia Chadema bado hakuna kiongozi wa kuitoa ccm madarakani hivyo Mbowe kwa kuwa yupo kwa maslahi ya chama anaona ni bora kiongozi wa kugombea nafis ya urais kupitia chadema akatokea ccm hivyo kusaidia chama an kifgalau kupata wabunge wengi. Kifupi kuna viongozi wakihama chadema chama kinaweza kuinarika sana sababu kitakuwa na image mpya ya kuvitia makundi yote katika jamii.
Una kapoonti kwa mbali
Waingereza husema " subtle'

Sijui kama wale wenye D mbili wataelewa
 
Kwamba Lisu aondoke cdm, kisha abaki Mbowe halafu cdm ivutie watu wa makundi mbalimbali? Utakuwa una homa boss. Akiondoka Lisu huko cdm, kitakachotokea kwa cdm itakuwa kama kilichoikuta CUF baada ya Maalim Seif kuondoka.
 
Back
Top Bottom