Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ikiondoka kwenye misingi iliyonifanya nijiunge nacho, nitaondoka. CHADEMA siyo mama yangu wala dini yangu

Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ikiondoka kwenye misingi iliyonifanya nijiunge nacho, nitaondoka. CHADEMA siyo mama yangu wala dini yangu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Binafsi naona Chadema itakuwa nzuri sana ikabaki na viongozi wenye msimamo wa kati na sio viongozi ambao wao kila kitu kinachofanywa na chama tawala kwao ni kibaya. Huwa namuona Mbowe ni kiongozi mzuri na mwenye busara nyingi mno hii inapelekea watu wengi wenye kutofautiana kimtazamo huko chama tawala kuona chadema kama ndio kimbilio lao. Tatizo linakuja kwa wale top wa chadema ambao ndoto zao ni kugombea urasi haijalishi wako popular au laah! wanamuona Mbowe ni kikwazo kwao kutimiza adhma zao, hapo ndipo Mbowe anaonekana mbaya. Kiuhalisia Chadema bado hakuna kiongozi wa kuitoa ccm madarakani hivyo Mbowe kwa kuwa yupo kwa maslahi ya chama anaona ni bora kiongozi wa kugombea nafis ya urais kupitia chadema akatokea ccm hivyo kusaidia chama an kifgalau kupata wabunge wengi. Kifupi kuna viongozi wakihama chadema chama kinaweza kuinarika sana sababu kitakuwa na image mpya ya kuvitia makundi yote katika jamii.

Labda kuwavutia kina Mdee. Ila ukweli mchungu:

Kujaribu kuwazodoa kina Mandela, Nyerere, Lissu, nk ni kujidhalilisha!

Habari ndiyo hiyo.
 
Dr. Aman Warid Kabouru, msomi mzaliwa wa ujiji , ambaye alishiriki kuianzisha chadema halafu lissu impact yake Kwa sasa ni ndogo na uungwaji mkono ni mdogo, aliondoka zitto enzi akiwa wamoto ije kua lissu ambae Kwa sasa hana ushawishi
Binafsi mbowe(dictator)kwa Sasa ni adui namba Moja wa upinzani na democracy pamoja na vibaraka wake( hech'e, lem'a, wenje, na msingwa "ccm")..... Kwa momentums ya upinzani ya 2010-2015.. chadema ingekuwa mbali sana kama mbowe asinge badili GIA angani .... Sasa ngoja kimfie mikononi...... "Uzuri upinzani ni jadi ya Kila binadamu" Ila Dictator anaudhoofisha, pia ufinyu wa kufikiri wa watanzania wengi wanadhani mbowe na genge lake wana haki miliki ya upinzani Tanzania, nje ya wao wewe ni ccm B, Mambo ya kijinga kabisa.,.......
Siombei CDM kufa... Ila ikibidi basi, kwani sio chama Cha kwanza Cha upinzani kufa, kumbuka NCCR, CAF, TLP Sasa tusipo kuwa makini DJ atakiua, Uzuri ni kwamba upinzani ni jadi ya binadamu basi kitazaliwa chama kingine, tena chenye nguvu zaidi ya CDM.
 
Kauli hizi za Lisu zinaashiria kwamba hakuna utulivu ndani ya chadema.
 
Tatizo linakuja kwa wale top wa chadema ambao ndoto zao ni kugombea urasi haijalishi wako popular au laah! wanamuona Mbowe ni kikwazo kwao kutimiza adhma zao, hapo ndipo Mbowe anaonekana mbaya. Kiuhalisia Chadema bado hakuna kiongozi wa kuitoa ccm madarakani hivyo Mbowe kwa kuwa yupo kwa maslahi ya chama anaona ni bora kiongozi wa kugombea nafis ya urais kupitia chadema akatokea ccm hivyo kusaidia chama an kifgalau kupata wabunge wengi. Kifupi kuna viongozi wakihama chadema chama kinaweza kuinarika sana sababu kitakuwa na image mpya ya kuvitia makundi yote katika jamii.
Hizi ni fikra za ajabu sana.
Sijui kama Mbowe akisoma mawazo ya namna hii atajisikia vizuri sana kama kiongozi wa chama cha siasa!

Unamtwisha Mbowe aibu kubwa sana kama kiongozi wa CHADEMA. Yaani Mbowe awe kiongozi wa kuilinda CCM kuwa madarakani? Haya ni mawazo toka wapi?
 
Alichokiongea Lissu ndo uhalisia wa maisha ulivyo, vinginevyo utaitwa unafki.
Ukweli ni kwamba, Lissu amejipambanua wazi kabisa kuwa ni kiongozi mwenye 'principles', siyo hawa wengine wasiojuwa kuwa kiongozi ni jambo gani.

Ukiniuliza katika viongozi tulio nao sasa katika vyama vyote vya siasa ni nani mwingine mwenye msimamo usio yumba hovyo hovyo, simwoni popote.
 
akiondoka umaarufu unakufa instantly
Kwani hakuwa maarufu kabla ya CHADEMA?
CHADEMA inakuwaje maarufu bila ya viongozi wanao ifanya iwe maarufu?
Iliwahi kuwa maarufu kwa uwepo wa akina Slaa; sasa hivi inatazamwa kwa matumaini kwa uwepo wa akina Tundu Lissu. Hawa wakiondoka CHADEMA inabaki kuwa kama vyama vya akina Cheyo na wengineo!

Kelele zote hizi zinazopigwa kuhusu akina Lissu, ni kwa sababu wao ndio kizingiti kilicho baki kukiingiza chama CCM; kama ODM ya Raila inavyoingia UDA na Kenya Kwanza. Huo ndio mpango mahsusi unaoisumbua CHADEMA sasa hivi.

Wale mabinti wa COVID -19, ni kama ndiyo ilikuwa 'advance' ya mpango wenyewe.
 
ni muoga sana anapima upepo wa nguvu na ushawishi alonao nchini, anachodhani yeye ni kuhurumiwa na kuchangiwa tu...

kwa maoni yangu aondokoke au asiondoke, kisiasa mambo ya chama kile yanaendelea kua ni yale yale tu ya harakati, asifikiri ati akiondoka au akibaki taasisi ile dhaifu sana itabadilika bali itakuepo tu na udhaifu wake 🐒
Ukweli mnaujuwa vizuri sana. Hakuna anaye watia hofu kubwa sasa hiv CCM kamaTundu Lissu. Mmemnunua Mbowe, na sasa ndiye tegemeo kubwa kwenu kuwa atawaondolea hiyo hofu kubwa inayo wavuruga akili.
 
Aondoke hata leo! Huyu ameshaona nafasi ya kugombea urais haipo ndiyo maana ameanza chokochoko! Aondoke tu! Aliondoka Slaa mbona CHADEMA haijafa?
 
Binafsi naona Chadema itakuwa nzuri sana ikabaki na viongozi wenye msimamo wa kati na sio viongozi ambao wao kila kitu kinachofanywa na chama tawala kwao ni kibaya. Huwa namuona Mbowe ni kiongozi mzuri na mwenye busara nyingi mno hii inapelekea watu wengi wenye kutofautiana kimtazamo huko chama tawala kuona chadema kama ndio kimbilio lao.

Tatizo linakuja kwa wale top wa chadema ambao ndoto zao ni kugombea urasi haijalishi wako popular au laah! wanamuona Mbowe ni kikwazo kwao kutimiza adhma zao, hapo ndipo Mbowe anaonekana mbaya. Kiuhalisia Chadema bado hakuna kiongozi wa kuitoa ccm madarakani hivyo Mbowe kwa kuwa yupo kwa maslahi ya chama anaona ni bora kiongozi wa kugombea nafis ya urais kupitia chadema akatokea ccm hivyo kusaidia chama an kifgalau kupata wabunge wengi. Kifupi kuna viongozi wakihama chadema chama kinaweza kuinarika sana sababu kitakuwa na image mpya ya kuvitia makundi yote katika jamii.
Kwamba uzuri wa Mbowe ni huo ustaarabu wake unaofanya Upinzani usichukue Dola? Hivi una akili kweli wewe?

Taarifa zinasema Mbowe anakula Rushwa kutoka Kwa washindani wake, na hili kwako unaona ni sawa tu?? Si Bure ile Supu ya mbuzi wa Machame imewavuruga akili
 
Chama cha siasa kinapaswa kuwa huru kwa kila mtu, yaani mtu yeyote aisikie huru kuhamia na kuhama. Sasa inapofikia chama cha siasa kina kuwa na watu wanaojihisi wao ni bora au ni wazawa kuliko wengine hii inakuwa sio poa. Hata timu za mpira zinafanya usajili kila mwaka kutoka kwenye timu pinzani ili kuimarisha timu zao.

Inavyoonekana huko ndani ya chadema kuna watu hawataki wageni kuhamia kutoka vyama vingine wakihofia nafasi zao kuchukuliwa wao hawajui kuwa usajili mpya utaleta mashabiki wapya. Hii ni roho ya tamaa na uchu wa madaraka, binafsi huwa sioni sababu ya chadema kukataa kuwasamehe wakina Halima Mdee, kisiasa kuwasamehe kuna faida kubwa kuliko kuwaacha wakahamia chama kingine, siasa ni sayansi hivi kuna madhara gani chadema itapata ikiwasamehe hawa watu. Hapa nahisi mwenyekiti yupo tayari kuwa samehe kwa faida ya chama ila kuna ambao hawataki. Kuna watu wapo kwa malsahi yao binafsi yaani wao wawe maarufu kuliko chama tofauti na Mbowe ambaye muda wote anaoneka kutaka kukijenga chama kwa gharama yeyote pale nafasi inapojitokeza.

Tunataka upinzani wenye uhuru wa kupokea mtu yeyote kutoka ccm ila awe ni mtu mwenye rekodi safi na ana wafuasi wa kutosha hii itasaidia sana kuwafanya ccm wawe makini kwa watu wao hasa wale wanaofanyiwa figisu. Leo hii kutokana na kejeli na matusi yanayotolewa na baadhi ya wafuasi na viongozi wa chadema kwa viongozi wetu waliopo madarakani na wastaafu, mtu yeyote mstaarabu kutoka ccm hawezi shawishika kujiunga na chadema ya aina hii.

Ushauri wangu kwa mwenyekiti wa chadema, usihofu watu kuhama chsma haijalishi ni watu maarufu kiasi gani au ni wangapi. Chadema tayari ni brand kubwa ni kama tu timu ya mpira mfano Manchester utd, kila mwaka mastaa wakubwa wanahama na timu inafanya usajili mwingine na maisha yanaendelea. Nakuhakikishia kuna watu wakihama chadema, chadema inaweza kuimarika sana kwa kufanya maingizo mapya ambayo yanaweza kuleta fikra na mtizamo mpya wenye uelekeo wa kuleta upinzani wa kweli kwa ccm na sio hivi sasa upinzani uliopo ni wachuki na wakiuanaharakati zaidi.

Kuna kundi kubwa sana linachukizwa na aina ya siasa ambazo chadema inafanya kwa sasa tofauti na alipokuwa Dr. Slaa siasa zilikuwa za hoja zaidi na sio za vijembe, kejeli na lugha zisizo za kistaarabu. Ukifuatilia vijana wengi wa chadema kwa sasa wamejaa jazba, hasira na matusi sijui mwalimu wao ni nani, tofauti kabisa vijana kama John Mnyika, Wenje, Heche nk ambao mimi naamini ni wanafunzi wa Dr.
 
Kwamba uzuri wa Mbowe ni huo ustaarabu wake unaofanya Upinzani usichukue Dola? Hivi una akili kweli wewe?

Taarifa zinasema Mbowe anakula Rushwa kutoka Kwa washindani wake, na hili kwako unaona ni sawa tu?? Si Bure ile Supu ya mbuzi wa Machame imewavuruga akili
Akili huna wewe unaoshindwa kuonganisha doti. Hivi unashindwa kujiuliza kwa nini hizi tuhuma zije wakati huu? Halafu ukome kunihuhisha mimi na vyama vya siasa mimi ni fikra iliye huru natoa uchambuzi wangu kutokana na hali halisi ilivyo. Mimi ni mfuasi wa mwanasisa yeyote mzalendo haijalishi yupo chama gani.
 
Kama makamu mwenyekiti wa chama analalamika hivi hadharani. Maana yake mwenyekiti wa chama ana ‘kitchen cabinet’ yake ambayo makamu sio sehemu ya hiyo close network kwa sasa.

Sishangai kwa sababu statement ya Lissu ya kusema yeye ndio mgombea uraisi wa uchaguzi 2025 hata kabla ya vikao vya chama havijaamua aina tofauti na statement ya Dr Slaa 2015.

Karma is a bitch Lissu (kama alivyomkana Dr Slaa 2015 na yeye akubali matokeo).

Shida zaidi ya Lissu ni psychological impairment kutokana na ‘significant life events’ ya shambulio anaishi na hasira kwa kila mtu anaedhani alikubali offer za Magufuli. Wakati maamuzi mengine kama ya COVID 19 ilikuwa njaa (na hakuna malaya duniani kama mwanasiasa, tofauti yake na anaejiuza barabarani mwanasiasa ana bei kubwa).

Ndio maana kwenye siasa hakuna adui wa kudumu Iła kuna maslahi ya kudumu.

Mbowe na Lissu wote wanakiuwa CDM, Mbowe kutokana na tamaa ya hela na Lissu kutoweza kusamehe uongozi wa Magufuli.

Na tatizo zaidi ni Lissu kwa sababu hayupo tayari chama kirudishe wanachama wanaoweza kukibeba kwa hasira zake anataka kila mtu awe sympathy na madhira yaliyomkuta that’s not how life works. Familia nyingi tu duniani b matatizo yako hawataki kujua iwe associates (wanasiasa) hasira za Lissu kwa covid 19 ni childish.

Ndio mwanzo wa kuelekea mwisho wa CDM.
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA- Bara, Tundu Lissu amsema iwacha CHADEMA itaacha misingi yake ailiyomfanya ajiunge na chama hicho basi ataondoka katika chama hicho na sio dhambi kufanya kuvyo kwani Chama cha Siasa sio mama yake wa dini yake

Akizungumza kupitia Mtandao wa Clubhouse amesema "Mwalimu Nyerere katika mojawapo ya kauli zake nyingi aliwahi kusema kwamba CCM siyo mama yangu na ikiacha misingi yake nitaiacha, ilikuwa kauli ya Mwalimu kuhusu chama alichokianzisha, kwa hiyo unataka mimi niseme kwa mazingira yoyote yale vyovyote itakavyokuwa sitahama CHADEMA? ni mama yangu?"

Ameongeza "Niliingia CHADEMA miaka 20 iliyopita na nimekuwa hapa miaka yote hii na Mungu anirehemu niendelee kuwa CHADEMA wakati nayo ikiendelea kuishi, lakini CHADEMA siyo dini na siyo mama yangu, ni chama cha siasa kikiondoka kwenye misingi yake iliyonipeleka nikajiunga nacho nitaondoka, nitakuwa sina sababu ya kubaki na hiyo siyo dhambi kwa sababu siyo dini na siyo mama yangu nikitumia maneno ya Mwalimu, ni chama cha siasa, vyama vya siasa huja na kuondoka, sisi binadamu tunakuja na kuondoka"

Sisi wengine toka uchaguzi wa 2015 tulibadili kabisa mtizamo wa siasa zetu. Lissu atakuwa liability kwa Chadema na watakuwa wanamlia timing tu.

It's sad lakini upinzani Tanzania unatakiwa kuzaliwa upya kupitia CCM kupasuka kama alivyotabiri Nyerere otherwise mengine ni kivuli tu.
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA- Bara, Tundu Lissu amsema iwacha CHADEMA itaacha misingi yake ailiyomfanya ajiunge na chama hicho basi ataondoka katika chama hicho na sio dhambi kufanya kuvyo kwani Chama cha Siasa sio mama yake wa dini yake

Akizungumza kupitia Mtandao wa Clubhouse amesema "Mwalimu Nyerere katika mojawapo ya kauli zake nyingi aliwahi kusema kwamba CCM siyo mama yangu na ikiacha misingi yake nitaiacha, ilikuwa kauli ya Mwalimu kuhusu chama alichokianzisha, kwa hiyo unataka mimi niseme kwa mazingira yoyote yale vyovyote itakavyokuwa sitahama CHADEMA? ni mama yangu?"

Ameongeza "Niliingia CHADEMA miaka 20 iliyopita na nimekuwa hapa miaka yote hii na Mungu anirehemu niendelee kuwa CHADEMA wakati nayo ikiendelea kuishi, lakini CHADEMA siyo dini na siyo mama yangu, ni chama cha siasa kikiondoka kwenye misingi yake iliyonipeleka nikajiunga nacho nitaondoka, nitakuwa sina sababu ya kubaki na hiyo siyo dhambi kwa sababu siyo dini na siyo mama yangu nikitumia maneno ya Mwalimu, ni chama cha siasa, vyama vya siasa huja na kuondoka, sisi binadamu tunakuja na kuondoka"

👍💪CDM inaungwa mkono na watu wengi makini kutokana na misingi iliyojengeka ndani ya itikadi na sera zake makini. Nakubaliana 100% na Lissu, kuwa endapo viongozi watakwenda kinyume na misingi hii, basi mtu ajawajibika kutengana nacho.

Ukiwa chama chenye kujinasibu katika kauli mbiu ya demokrasia na maendeleo, ni vyema kikaishi kwayo. Yote haya yatatokea endapo CDM kama timu moja itafanya kila liwezalo kupata viongozi bora kwa njia zilizo bora, za kistaarabu, na pia zenye kuaminiana.
 
Back
Top Bottom