Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ikiondoka kwenye misingi iliyonifanya nijiunge nacho, nitaondoka. CHADEMA siyo mama yangu wala dini yangu

Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ikiondoka kwenye misingi iliyonifanya nijiunge nacho, nitaondoka. CHADEMA siyo mama yangu wala dini yangu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hata yule aliongea hivi hivi na mwisho wa siku Chama la wana.. Chama Tawala! Wakamchukua..
Tawala wanavyo kuwavutia subira tuu...
 
Hili jamaa bwege sana, ni huyuhuyu Lissu alitumika luwatimua akina Zitto Kitilla Kafulila, huyuhuyu lissu alimnyanganya form ya kugombea urais Dr Slaa, sasa wamemgeuzia jambia kaanza kubweka
 
👍💪CDM inaungwa mkono na watu wengi makini kutokana na misingi iliyojengeka ndani ya itikadi na sera zake makini. Nakubaliana 100% na Lissu, kuwa endapo viongozi watakwenda kinyume na misingi hii, basi mtu ajawajibika kutengana nacho.

Ukiwa chama chenye kujinasibu katika kauli mbiu ya demokrasia na maendeleo, ni vyema kikaishi kwayo. Yote haya yatatokea endapo CDM kama timu moja itafanya kila liwezalo kupata viongozi bora kwa njia zilizo bora, za kistaarabu, na pia zenye kuaminiana.
Wewe nafikiri unaizungumzia CDM ile ya enzi za Dr Slaa 2005 hadi 2015, na Lowasa 2015 hadi 2020. Baada ya hapo CDM kimekuwa chama cha hovyo ambacho hakina mbele wala nyuma. Watu wengi wameamua kuachana nacho baada ya kugundua kuwa viongozi wao wanaangalia matumbo yao tu badala ya masilahi ya taifa. Kumbuka 2015 wakati wanamkaribisha Lowasa waliesema kuwa ni fisadi namba 1 nchini na kisha kumpa ticket ya kugombea uraisi. Watu walishangaa mtu wanaosema fisadi wamkabidhi uraisi. CDM badala ya kuacha kumpa Lowasa ticket ya uraisi wao walitetea uamuzi wao na kusema kuwa CDM iko tayari kushirikiana na yeyote hata shetani ili mradi tu wawe na uhakika wa kuing'oa CCM madarakani. Kwa maana nyingine CDM haisimamii misingi yake, yani kwenye masilahi wanaweza kushirikiana na yeyote hata mwizi, mkimbizi nk ili mradi tu wafanikiwe mipango yao ya kujaza matumbo yao na ya familia zao.

Toka hapo watu wenye akili wakaanza kupukutika ndani ya chama baada ya kuona kumbe wanaopambana na mafisadi na wao wanaweza kuongozwa pia hata na fisadi kama Lowasa. Wasomi kama makamu mwenyekiti Profesa Abdallah Safari, Mabere Marando na wengine wengi wakajitoa kimya kimya na kuwaachia wenye biashara zao za siasa wabaki na chama. Haya nilioandika unaweza kujifanya kuyapinga mbele ya wana CDM wenzako, lkn moyoni unakubali kuwa nilichoandika kina ukweli wa 80%
 
The cracks are deepening, and I doubt if CHADEMA will survive the coming ordeal.

The biggest challenge for CHADEMA is fear of self-reflection, and failing to acknowledge that despite the enormous contributions of Mbowe, he has now turned that political party into his own fiefdom.

Hili linapelekea CHADEMA iwe na taswira ioneshanyo kwamba chama ni mali ya wachagga peke yao na kwenye maamuzi wao ndiyo wao.

Too bad kuona CHADEMA imefika hapa.​
Why all this English my fellow jobless? Usiharibu kiingereza cha kutongozea tutakapo pata ajira.please
 
Chadema fikiria nje ya box,hivi bila Mbowe na Lissu haiwezi kuwepo na ikawa imara?
Nadhani Chadema ni zaidi ya Lissu na Mbowe.
Tumieni katiba yenu kuhimarisha chama.

Tumeona Raisi Biden anajiondoa kwenye kinyanganyilo cha kugombea uraisi wa Marekani tena katika saa za majeruhi kwa tiketi ya Democratic na chama hakikuyumba bali kimeimalika zaidi.

Haya mambo ya bila mimi hakuna Chadema inabidi tuyafute akilini mwetu.
Kwani wanzilishi akina Barongo,Bob Makani na wenzake waliokipigania chama tokea uchanga wake hadi ninyimnatatka kuvuna ambapo hamkupanda komaeni kifikra sio kukomaa mwili.
 
Back
Top Bottom