Pre GE2025 Lissu: CHADEMA ipo nusu kaputi, Mbowe hataki kupambana na Samia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Haahaa kasababisha yepi mkuu shujaa wa mtandao I?😂
 
Hili mtaruka mtatua lkn lipo wazi ya kwamba lissu anaendeshwa kama drone ktk swala hili na rafiki yake kipenzi msigwa wa ccm
Haahaa kama ni fact acha tu aendeshwe, lakini lissu ndo mpango mzima kwa sasa chadema
 
Hivi unajua maana ya makamu?😂😂😂
 


..Tundu Lissu hakupinga Chadema kuingia ktk maridhiano.

..Kilichotokea ni Lissu kupinga danadana na ubabaishaji waliokuwa wakifanya Ccm wakati wa maridhiano.

..Maridhiano yalikuwa yanahusu mambo kama Tume Huru, Katiba Mpya, etc na imethibitika kwamba Ccm walikuwa wanawapotezea muda Chadema kupitia maridhiano, na ACt na wengine kupitia kikosi kazi.

..Kwa maoni yangu chama kinahitaji kujipanga upya, na kurudi kwa wananchi kwa ari kubwa zaidi.
 
Kwamba Lissu anashikiwa akili na msigwa?
Unajua Mbowe anapewa support na dola ya kupambana na Lissu? Tulia uione show ya lissu
Kwenye sakata hili Mbowe anasapoti kutoka ikulu.. huyu sio kiongozi bali ni mpiga dili tu.
 
Lakini Wakuu hii Strategy ya "NO REFORMS NO ELECTIONS" yale Mafisiemu si yanashangilia?!

Mnaonaje Jemadari Lissu atufafanulie zaidi maana Uchaguzi ujao mimi nataka uwe Jino kwa Jino wakituibia tunaingia Mabarabarani.
Mwisho wako ni key board kamwe huwezi kuingia barabarani.
 
Nilipofika kwenye mass mobilisation nimeacha kusoma. Upinzani hasa Chadema wana kazi ya zaida ya kufanya ili kuitoa ccm madarakani. Ni vipi chama kitafanya mass mobilisation wakati tangu wameruhisiwa kufanya mikutano wameshindwa kuekeza sera zao kama chama badala yake wamekuwa wakiikosoa serekali tena kwa kejeli na kurukia rukia mambo. Karen hii ya 21 chama cha siasa kinafanya siasa kama za enzi za kudai uhuru, . Chadema ili ijikwamue hapo ilipo inataka viongozi wataoweza kuzungumzia sera zaidi kuliko mambo yao binafsi , watu wanahitaji kumuona kiongozi atakayeweza kuwasemea zaidi kuliko kiongozi anayepata nafasi na kuzungumzia mambo yake binafsi na kueneza chuki dhidi ya watu wengine.

Watanzania kwa asili ni watu wasiopenda fujo, na kama kuna kiongozi yeyote atataka kutumia njia hii atafeli mapema sana, nakumbuka Chadema ya Dr. Slaa na kina Zito Kabwe ilikuwa ni Chadema ya hoja zenye mashiko kwa taifa na ndio maana watu walikipenda sana chama walio wanachama na wasio wanachama viongozi wale walikuwa wakizungumzia mambo ya kitaifa zaidi na sio mambo binafsi, leo hii sioni mtu wa karba ya Dr. Slaa na Zito Kabwe ndani ya Chadema. Wasipoangalia kwa makini ACT atakwenda kunyakua nafasi yao. Tuwe wa kweli kwa hali ilivyo sasa Chadema ni vigumu mzaleondo kutoka chama kingine akajiunga nao, kutokana na wao kwa sasa hawana sera shawishi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…